TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania itakua moja ya nchi za mwanzo barani Afrika, kunufaika na mpango wa pamoja wa Kilimo kwa nia ya kuongeza na kulinda usalama wa chakula na lishe kwa watu wake.

Rais Barack Obama wa Marekani aliyasema hayo jana (18.5.12) katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano kuhusu Kilimo na usalama wa chakula (Global Agriculture and Food Security) lililoandaliwa na kituo cha Masuala ya Kimataifa, Chicago Council on Global Affairs jijini Washington.

"Nimeona kuwa kuna umuhimu pia wa kuangalia changamoto zinazoikabili dunia, changamoto ya usalama wa chakula, tutatangaza ushirikiano mpya na nchi tatu zitakua za mwanzo kuanza ushirikiano huu ambao tutatangaza kwenye kushughulikia usalama wa chakula" Rais Obama amesema hayo mbele ya viongozi wa Afrika, ambao nchi zao zitakua za mwanzo kunufaika na uhusiano huo ambazo ni Ethiopia, Ghana naTanzania.

Rais Obama amesema ushirikiano huu mpya utatangazwa rasmi katika Kikao cha Nchi 8 tajiri zenye viwanda duniani maarufu kama G8 unaofanyika tarehe 19 May, 2012 katika makazi ya kupumzikia Rais wa Marekani na wageni wake maarufu kama Camp David.


Kikao hicho cha nchi tajiri duniani kimeweka katika agenda yake swala la chakula duniani kutokana na umuhimu wake katika kipindi hiki.

“Tumeliweka suala la kupiga vita njaa, Marekani ina wajibu wa kupiga vita njaa na pia suala la usalama wa chakula ni suala la kiuchumi" amesema na kuelezea kuwa Bara la Afrika linaweza kujitosheleza kwa chakula na pia katika kuuza nchi za nje.

Ushirikiano huu utakaotangazwa na Nchi 8 tajiri utahusisha serikali, watu binafsi na wafadhili ambapo mwito umetolewa kwa nchi tajiri kutimiza ahadi zao.

Kikao cha kila mwaka cha Nchi 8 tajiri zenye viwanda duniani ambazo ni Canada, ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Urusi, zingine ni Uingereza na Marekani.

Katika kikao cha mwaka huu, Tanzania imealikwa kuhudhuria kikao hicho kutokana na mpango wake wa Kilimo Kwanza, ambapo nchi tajiri zimeuchukua kama mfano ambapo juhudi na mikakati iliyomo katika Kilimo Kwanza, itatumika na kuendeleza nchi zingine barani Afrika.

Rais Obama amesema nchi hizi tatu za kwanza zimechaguliwa kunufaika na ushirikiano huu kwa vile zimeonyesha kufikia katika Kilimo na usalama wa chakula.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tayari yuko jijini Washington kuhudhuria kikao hicho ambapo anategemewa kuelezea matarajio na muelekeo wa Tanzania katika ushirikiano huu.

Akizungumza katika kongamano hilo la siku moja, Rais Kikwete ameelezea umuhimu wa ushirikiano huu unaohusisha serikali, wafanya biasharabinafsi na wafadhili.

"Tunahitaji msaada zaidi katika Kilimo na pia Kilimo hakiwezi kuachwa kwenye mikono ya serikali na wafadhili peke yake, hata Sekta binafsi ina mchango mkubwa" amesema na kuelezea kuwa amefarijika sana, ana matumaini na anategemea yanayozungumzwa yatatimizwa"

Mkutano wa G8 pia utahudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambapo Mwenyekiti wake, Rais Yayi Boni wa Benin anatarajia kuhudhuria pamoja na Rais John Mills wa Ghana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.

Rais Kikwete ataondoka Marekani Jumapili usiku kurudi Dar-es-Salaam.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Washington.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2012

    Tuna mshukuru mheshimiwa raisi Obama kwa ushirikiano wake na upendo wake anao uonyesha kwa watanzania na kwa bara la africa kwa pamoja. Pia mzee wetu Kikwete naye tunampongeza maana naye jitihada zake ndio zimefanya Tanzania kupewa kipaumbele. Tuko pamoja, mungu ibariki Tz , mungu ibariki Africa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2012

    good sign ,tumeonesha nia ila kuna challenge kubwa , mpango wa Kilimo kwanza haujaleta IMPACT kubwa kwenye kilimo chetu ,tunahitaji kurudi kwenye drawing board ku re-strategize kama tunataka kufufua kilimo kweli ,tuingize technologia ,umwagiliaji na mikopo kwa wakulima na kufufua vyama vya ushirika nk.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2012

    Haters mpo? wale bendera fuata upepo wa jamii forums kimyaaaaa!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2012

    mhhhhhhhh haya si bure

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2012

    i doubt if any mwananchi will gain anything from this, hizo hela zitaliwa na, TUKURU inawalinda mafisadi. G8 countries economies are struggling, I wonder where will all these monies come from?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2012

    NAOMBA TUZIOMBEE HIZO PESA KABLA CHEQUE HAIJAANDIKWA JAMANI KUNA HATERS WANASUBIRI KUZITAFUNA AIBU IWE KWA SERIKALI NAOMBA TUOMBE MUNGU ATAKAE KULA HATA SUMNI TUMBO LIPASUKE HADHARANI. WAKULIMA WANAPATA SHIDA SANA

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2012

    Ni jambo zuri...lakini ukweli ni kwamba bila usimamizi wa hizi fedha hakuna lolote litakalofanikiwa, sekta ya kilimo ni kati ya sekta yenye miradi mingi na hela zimekuwa zikimwagwa na wafadhili pamoja na serikali lakini nenda Halimashauri uone zinavyotafunwa utatoa machozi. Uzalendo hakuna kabisa Tanzania kwa sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...