Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kulia) akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,Mh. Juma Kassim alieongozana na ujumbe wa Wajasiriamali wanaofuga Nyuki katika Kisiwa cha Pemba,Zanzibar waliofika Ofisini kwake leo.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TASAF,Ladislaus Mwamanga. kikundi hicho kipo Mkoani Dodoma kwa mafunzo ya ufugaji nyuki.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (mwenye kaunda suti) akizungumza na Mwita Marwa ambaye ni mlemavu aliefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kumshukuru Mkurugenzi huyo kutokana na TASAF kuwasaidia walemavu wa chama cha DIPEDEA ambacho kilisaidiwa na msaada wa kutengeneza baiskeli za walemavu katika miaka mitano iliyopita na mpaka hivi sasa wame weza kutengeneza baisikeli 60.chama hicho kimeweza kutengeneza baiskeli inayo tumia injini yenye uwezo wa kwenda spidi 60 na kutumia mafuta kidogo.Kulia ni Meneja Rasimali Watu wa TASAF,Bi. Thekla Makundi.picha na Chris Mfinanga.
Ufugaji Nyuki:
ReplyDeleteHii ndio sekta muafaka ya kimasiha kwa Wastaafu!
Badala ya kubuni biashara zisizo na tija kama biashara ya bidhaa kuagiza kutoka China, kuendesha Baa, Pub na mipango mingine isiyo endelevu