Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman aliongoza Ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano katika sherehe zilizofanyika tarehe 12 May 2012 katika Hotel ya Grand Hyatt Muscat, mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Mhandisi Khalid bin Hilal bin Soud Al Busaidi, , Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Oman . Mgeni rasmi alifuatana na ujumbe mzito kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman akiwemo His Highness Mohamed bin Salim Al Said, Mkuu wa Itifaki, Mheshimiwa Balozi Hamed Al Kiyumi, Mkurugenzi wa Idara ya Africa, Mheshimiwa Mohamed Al Khusaibi, Mkurugenzi wa Idara ya Amerika Kaskazini. Sherehe hii pia ilihudhuria na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Oman, wafanyabiashara, waoman na watanzania wanaoishi Oman.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman ( katikati ) katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mheshimiwa Mhandisi Khalid bin Hilal bin Soud Al Busaidi ( wapili kutoka kulia ) wengine katika picha ni Mheshimiwa Balozi Mohamed Al Khusaibi, Mkurugenzi wa Idara ya Amerika Kaskazini ( wa kwanza kushoto ), His Highness Mohamed Salim Al Said, Mkuu wa Itifaki, ( wapili kushoto ) Mheshimiwa Balozi Hamed Al Kiyumi, Mkurugenzi wa Idara ya Africa, ( wakwanza kulia )
Baadhi ya wadau Mbali mbali waliohudhulia Sherehe hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...