Ndugu zangu na rafiki zangu.
Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!
Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.
Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.
Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.
Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?
Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.
Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?
Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.
Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.
Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.
Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.
Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.
Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.
Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.
Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.
Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.
WASALAAM.
Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!
Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.
Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.
Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.
Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?
Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.
Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?
Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.
Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.
Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.
Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.
Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.
Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.
Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.
Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.
Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.
WASALAAM.
EZEKIEL MAIGE (MB)
Ni vigumu saaana kuahamini unayosema hapa mh mbunge. Kama ungekuwa 'clean' ungebainisha mapema. Mawaziri wako zaidi ya 50 ni sita tu ndo wamepoteza kazi. Kweli nyie ndo mnaonewa au mmejionea wenyewe either kwa kutokuwa waaminifu au kwa waaminifu zaidi ya wenzenu
ReplyDeleteMara Maige ameishakuwa mhubiri na yeye????!!!!
ReplyDeleteWanachekesha sana wanasiasa: wanapofanya udhalimu wao na majibu ya jeuri bungeni hawakumbuki Mungu wala Yesu. Wanaposhughulikiwa wao, mafungu ya Biblia mengiiiiiiii na kujifananisha na Yesu sana na kwenda makanisani kujifanya waumini na kudanganya kuchangia makanisani!!!!
Mbona hamumtaji huyo Yesu siku nyingine na hasa mnapokuwa mnatoa majibu ya dharau bungeni????!!!!!
Hata Lusinde akishughulikiwa leo kesho utashangaa anatumia Biblia na kujifanya mkristoo sana....kwendeni zenu huko. Mmetuchosha bwana.
too late Maige, kwanini sasa (why now?) ungekuwa na desturi za kutupa taarifa mara kwa mara kuhusu utendaji wako wakati ukiwa kazini basi wengi tusingekuwa na mashaka juu yako. Hii tunaiona ni kujaribu kujikosha, Umechelewa umeshatupwa nje. Na ni aibu kwa wabunge wetu vijana kustaafishwa mapemaaa kwa tuhuma za ubadhilifu na pia utendaji mbovu, je future iko wapi, (I am only 42, I have already been a minister, milionaire and was fired). alexbura dar
ReplyDeleteNani kakuomba maelezo? kwani wewe ulizaliwa waziri hivyo kuachishwa ni jambo la ajabu, kwanza ungekuwa mjanja ungewajibika kwa kujiuzulu na usingesubiri kupigwa chini na Mh.huna haja ya kujisafisha maana tayari uwaziri hauna tena wewe fanya mambo yako binafsi. Ama kweli kitumbua kilikuwa kitamu.
ReplyDeleteToo late to apologize.
ReplyDeleteAcha uhuni! umesalitiwa na nani? walikuona mwizi nao wakaiba kama wewe sasa walalamika nini? tuambie basi hizo dola 700,000 ulizipataje kama sio wizi? TAKUKURU tunaomba majibu ya huyu mtu! Sijui kikwete alikuokota wapi!
ReplyDeleteKama kawa, majuto mjukuu! Alikuwa wapi kutueleza hayo? Acha hizo bw maige, umeshaingia kikaangoni ngoja wakusafishe wenzako!
ReplyDeleteMICHUZI NAOMBA UNURUSHIE HEWANI HII COMMENT YANGU TAFADHALI....!
ReplyDeleteMICHUZI NA WADAU WENZANGU HIVI HUYU COMEDIAN WA IFM BADO ANA LALAMIKA NINI SI AENDE SEMINARI AKAHUBIRI, KILICHOTOKEA HAPA NI KWAMBA WABUNGE NA WANA NCHI HAWAKUWA NA IMANI NA HUYU MTOTO SASA KUNA UBAYA GANI KAMA AMETIMULIWA? KAMA HAYO MADUDU ALIPOYAKUTA WAKATI AMEKUJA 2011 KWA NINI HAKUYA SEMA BUNGENI NA KWA MTUKUFU RAIS KIKWETE? SASA ANAKUJA NA JANJA YA NYANI ETI MUNGU ATANISAIDI HII MIMI NAONA NI JANJA YA KUOGOPA KWENDA UKONGA. MTU KAMA UNA AKILI TIMAMU WEWE NI WAZIRI KWA NINI UKOPE DOLA 400,000 ZA NYUMBA? MBONA JANUARY MAKAMBA KAZITUMIA HELA ZA MKOPO KUJENGA KAOFISI KAZURI BUMBULI? MHESHIMIWA MAIGE MUNGU HAJAKUTUPA BADO WEWE NI MBUNGE SALI ROZARI KUTWA MARA TATU USITUPWE UKONGA HUKO NDUGU YANGU HALI SI SHWARI KABISA. KWELI KIKWETE HAPA NIMEKUSHANGAA SANA NA PIA NAKUPONGEZA, NAKUSHANGAA HUYU BWANA ULIWEZAJE KUMCHAGUA WAZIRI? NAKUPONGEZA KUMPIGA CHINI. HAYA MAMBO YANANIKUMBUSHA HIGH SCHOOL KULE SKONGE TABORA UNAIBA MACHUNGWA UKIKAMATWA UNA LIA UNASEMA HAKI YA MUNGU NIMEKUTA YAMEANGUKA CHINI NIKAWA NAYAOKOTA TU YASIHALIBIKE JAMANI NAOMBA MNISAMEHE MIMI SIYO MWIZI WA MATUNDA, UKIULIZWA KILICHOKUPELEKA SHAMBANI NI NINI UNAKODOA MACHO. WABUNGE WAMEHOJI BUNGENI HUKUTOA HII SIRI SASA KARIBU TUNA KWENDA UKONGA OOH WAKISTO MUNGU HIVI YESU VILE OOH NAONEWA MIMI MCHAPA KAZI MIMI SIKUGUSWA NA CAG SIJUI. TULIA MBONA NGOMA BADO HII NI MWANZO TU UTATUAMBIA EXACTLY WHAT HAPPENED. MICHUZI ASANTE SANA.
Maige mambo yameshasemwa ila nimeshangaa sana uliposema kuwa sasa UNAANZA kuwatumikia wananchi wa jimbo lako..... kweli mpaka uondolewew uwaziri ndio unakumbuka kuwa ulikuwa mbunge, I hope wananchi wako wameona na kukuelewa. umejionesha mwenyewe jinsi ulivyo.
ReplyDeleteDa kweli hii ndio picha halisi ya wabunge/viongozi/ watendaji/ wetu wa Tz wanayokumbana nayo tukubali tukatae wadau, kweli Maige imekuuma sana tena sana, lakini wakati ukuta na ukishindana nao utaumia , pointi tu ni kwamba mfumo mzima wa uendeshaji wa wizara na mashirika yake umeshikwa na mafisadi , while your on duty ahh they will praise you na kukupa madili kibao na bahasha/bakishi but when you go agaisnt them kaka watakushungulikia ( that is what happen) wewe unanyima vitalu mafisadi what do you expect???
ReplyDeleteMajizo
hehehehehehehehe
ReplyDeleteMhe maige unajimaliza mwenyewe na unakimaliza Dhaka chako, kila aliyejerihiwa akitaka kujisafisha basi athari. Zake ni km maoni yaliyotolewa hapo juu. Chapa kazi jimboni kwako watu wataakuamini kwa vitendo vyako.
ReplyDeleteMhe. Mbunge Ezeckiel Maige:
ReplyDeleteKWA NINI USIANIKE UKWELI HUU HAPO KABLA?
bora ungekaa kimpya...hapa ndio unajifunga kabisaaa
ReplyDeleteKwenda zako huko mnafiki mkubwa wewe, michu hakikisha zizi comments huyu Maige anazizoma ajione alivyo mjinga.
ReplyDeletejamani ni mimi tu mbona sijaona SIRI YOYOTE ALIYO ITOA huyu mtu vipi kweli nakubaliana na anoy hapo juu ezekiel wewe ni bonge la msanii,kajiunge na Ze Comedy. Hakuna ulicho sema pumba tu sijui hii ni sign ya kuchanganyikiwa? Uwaziri ni cheo tu leo upo kesho haupo hakuna anayekuchukia wewe hujui kazi na hii siri sijui umeitoa wapi maana sioni hata ulicho toa kama siri mimi naona umelalamika tu kama mtu yeyote anaye tapatapa ama amechanganyikiwa. Unamuaibisha President Kikwete kwa kweli kama mawaziri ndiyo nyie kazi ipo na ni aibu kubwa sana.
ReplyDeleteOPEN LETTER TO ZEKEY MAIGEEEEEEEE..
ReplyDeleteezekiel maige njoo DC ubebe box mbona bado mdogo una miaka mingapi? hapa kiwandani wana hire 3rd shift kuna bonus poa mwisho wa mwaka tuna pewa bonus $ 425.00 kila mtu halafu uzuri mwingine kuna overtime za kumwaga, kuna dada mmoja ila sema ni mnene sana ni mzungu anatafuta bwana nilimwambia kuna cousin wangu anakuja kafurahi sana sasa mimi nitamwambia kabisa ni wewe kwa hiyo ukija wewe sema unaitwa Zekey usiseme Ezekiel utaonekana umbongo mbongo wewe jifanye mnugu ila umekulia bongo. Toboa maskio yote tena weka heleni za Gold, mambo poa tuta banana kwenye bedroom moja wewe utalala kwenye kochi maana room mate wangu wanne 2 kutoka Nigeria 1 mchina na 1 ni kutoka Congo wote poa tuna piga box ila mimi na wewe tutakuwa 3rd shift. kupika ni kupokezana wewe utakuwa unapika juma tano na kusafisha bafu jumanne landrod mkali sana anakuja hata usiku kucheck kama tunasafisha pango. Nitakutafutia social na kukufundisha mtihani wa kuendesha gari siyo mgumu sana lakini wageni wengi huwa wana dunda mara 2 ama 3 hivi wote ni maltiple choice hakuna fill the blanks kuendesha siunajua? huyu dada anaitwa Laura Higgins ana miaka 39 ana watoto 3 wote kazaa na wanugu 2 tofauti anapata child support kwa hiyo unaweza kuzikandamiza tu ukimweka fresh. Fikiria kama unaona vipi basi mchizi nikutumie mapepa esign unakuja kuanza shule haafu nakusukumiza kwa laura mchizi unakomaa naye unapiga ndoa paper zinakuja unaingia mtini unamleta mamaa wako wa bongo siunajua mchizi wangu Box hapa na over time unapata kama dollar 1500 kwa week ukikomaa vizuri mpaka 2000 kabla ya tax poa kabisa jioni Debe kuku wengi tu bei poa mfuko dollar 5 tu. Mchizi nipe feedback basi kama unakuja, watu wazuke airpoooortttt...
Pole sana Mr."Do something right no one remembers,Do something wrong no one forgets".so let it go U'll find peace somewhere else.
ReplyDeleteNdugu yetu Maige, POLE SANA NA MAJUKUMU ya kununua nyumba ambayo siku si nyingi itakuwa ni ofisi ya TAKUKURU kanda ya wilaya ya KINONDONI.Unadai hukuguswa na ripoti ya CAG,Je,mwaka 2010 ulikuwa wapi wakati hayo madhambi yanafanyika?Nimefurahishwa na maneno yako kua sasa unarudi kututumikia wapigakura wako wa Msalala,kwani ni ukweli usiopingika kuwa ulikuwa unajishibisha kwanza!!!NJOO 2015 utuombe kura tena
ReplyDeleteManagement Accounting bado ni somo linalotahiniwa na NBAA achana na siasa kijana rudi kafundishe MA. Wewe unaacha professional yako unakimbilia kitu ambacho kinaitwa Si HASA, pole sana. Ningekuwa mimi ningejiuzulu na ubunge na kurudi kwenye professional. Tamaa za utajiri wa haraka zimekufikisha pabaya kijana. Mida hii ndio unamkumbuka mungu ndugu. Mungu anasema lakini kuwa TAJIRI KUUONA UFALME WA MBINGU NI SAWA NA NGAMIA KUPENYA KWENYE TUNDU LA SINDANO. Kwa Mtanzania unayemiliki nyumba ya sh 450M tayari ni tajiri.
ReplyDeletehuo ndo tunaita unafiki mkubwa na usaliti kwa taifa unaofanywa na viongozi wetu. wewe ni mmoja wao. inakuwaje hata hatujawahi kusikia ukiwakemea hao wabaya wako? mbona Magufuli anasema wazi wazi? wewe unachofanya ni kujuta tu, huna lolote kafie mbali. Ona magufuli anasema wazi wazi na kila mtu anajua msimamo wake. sasa wewe msimamo wako uko wapi. eti unaweka vifungu vya bible kujifariji, ama kweli umekwisha. uliwalinda sasa yaliyokukuta ndo hayo.
ReplyDeletemdau (ukweli unajidhihirisha wenyewe, by mm, 2012)
Kweli sasa ninakubaliana na wale waliosema huyu Bwana Maige hana sifa ya kuwa waziri, achilia mbali mbunge. Sasa ndio unaanza kuwatumikia wapiga kura wa Msalala. Kweli? Hivi na sisi wapiga kura, ni kitu gani kinatufanya tuwachague hawa watu? Ninadhani tuna uzoefu wa kutosha na hawa watu. Sasa, we are almost half way, ndio anatuambia anaanza kuwatumikia wananchi wa jimbo la Msalala. Labda sijaelewa. Labda anamaanisha kuwa sasa anaanza kazi ya kuibua uozo wa serikali. Labda hili ndilo analomaanisha. Kama ndivyo, safi. Ndicho tunachotarajia mbunge afanye. Godspeed.
ReplyDeleteAhhh wapi!
ReplyDeleteMhe. Maige Ezeckiel kama ni Uchungaji kwa namna ya Uchungaji wako wa kuwatosa Watanzania hapo kabla huku ukiyajua hayo unayoyasema sasa utakuwa SI MCHUNGAJI MWEMA bali utakuwa ni KIBWETERE!
''Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo'' By Ezekiel Maige ; Kimsingi nakushangaa kwamba mpaka sasa wananachi wa Msalala ulikuwa hujaanza kutuwakilisha, ila umetolewa Uwaziri ndio unasema Unaanza kutuwakilisha. Mimi ni Mwana-Msalala natokea kijiji unachotoka wewe Kijiji cha Segese (jijrani na Mzee Makune), wewe si kiongozi bali unalako jambo. Unataka kutuambia kuwa Tanzania yenye watu zaidi ya Milioni 40 wewe tu ndio unafaa kuongoza kiasi cha kusema kuwa hapakuwa na haki wewe kuondolewa wizara hiyo? Hata kama utendaji wako ni mzuri kumbuka cheo ni dhamana na inapotokea dhamana hiyo unanyang'anywa huna budi kuiachia. 2015 tutakutana Jimboni, lazima nikung'oe ubunge.., nadhani hata nyumba uliyonunua utaweka rehani kupambana nami katika nafasi hiyo lakini lazima nikung'oe kwani nina nguvu isiyo kifani na siwezi kushindana na wewe.
ReplyDeleteHuo Ulokole wako wa kuficha ukweli na sasa umwemwaga unga ndio useme utakuwa ni wale wale wa 'Ulokole wa Kisasa'!
ReplyDeleteMH MAIGE UNA KIPAJI CHA KUHUBIRI, USHAURI WA BURE ANZISHA KANISA LAKO HUKO NAKO KUNALIPA KWELI, I CAN SEE UNA POTENTIAL KWENYE FANI YA MAHUBIRI MAANA UMEANGUSHA MISTARI SI MCHEZO.
ReplyDeleteOhoooo!
ReplyDeleteMwakei!
Mhe. Maige wewe utakuwa ni Mukirisito wa Kimujini mujini!
Pole mheshimiwa maige, sasa umejifunza kuwa next time be proactive not passive kama ulivyofanya.
ReplyDeletepole ndugu yangu.
Mdogo wangu Maige, asiyejua maana aambiwi maana,haya yote ni kama unapoteza muda na unataka kuzidi kuukwaza moyo wako. Kumbuka hii ni dunia hakuna haki, haki iko tu mbinguni, tupo watu kama mimi tunaojua for sure kuwa wewe na baadhi ya wenzio mlijitahidi kwa hali zote kuchapa kazi kwa ajili ya watu wa taifa hili,lakini hakuna anayeona wala ku appreciate. Ninachokushauri kaa kimya fanya mambo yako,mtetezi wako anayeona yaliyo sirini yu hai na asinzii wala halali usingizi, na yeye ndiye anayetuambia vita si yetu bali ni yake,mtumainie yeye naye atakujibu. soma Zaburi 35 kwa kusudi hilo uone Mungu atakalokufanyia achana na kutaka sifa toka kwa mwanadamu.
ReplyDeleteMimi sioni sababu yoyote ya wewe kuweweseka.Cheo cha uwaziri sio cha milele umefanya upuuzi umeondolewa sasa unalia nini??
ReplyDeleteJuzi nimekuona kwenye pick-up kumbe unajua kuendesha?? Land cruiser la WM liko wapi??
Rudi kwa wananchi wako uwaombe msamaha kwa yote uliyofanya.
NANI KAMWOMBA HAYA YOTE,UKWELI UNAKUJA PALE PALE KWANZA HAO TWIGA NA WANYAMA WENGINE HAWAKUTOROSHWA WALIKUWA NA VIBALI,HUYU MAIGE KALIDANGANYA BUNGE NA WAZIRI MKUU,WATANZANIA WENGI HAWAJUI BIASHARA YA VIUMBE HAI 100% INAFANYWA NA WAZAWA TENA SIO MATAJIRI WAKUBWA KAMA WAWINDAJI WA KITALII,HUYU JAMAA KAWAINGIZA WAZAWA HAWA KWA KUSEMA UONGO BUNGENI KWENYE UMASIKINI WA KUTUPWA WAKATI WAKIWA NA VIBALI NA LESENI HALALI KWA KUWAFUNGIA BIASHARA YAO,WAKATI WANA KILA KITU TANGU LESENI NA VIBALI HALALI WAMELIPIA SERIKALINI KODI ZOTE ,AMEWAINGIZA KWENYE UMASIKINI WA KUTUPWA WAZAWA HAWA,HAPA ANATAKA KUJISHAFISHA NINI??? NA KUINGIZA BIBLIA WAKATI KUNA USHAHIDI WA KUPOKEA FEDHA ZA VITALU AMBAO HAUPO KATIKA HATA HIZO REPORT ZA KAMATI YA MALI ASILI AU CAG,ANATAFUTA KUJISHAFISHA KWENYE MAGAZETI IS TOO LET WE HAVE ALL EVIDENCE
ReplyDeleteEeee Baba wa Kanisa,
ReplyDeleteEeee Baba Paroko,
Eeee Baba wa Imani,
Ulikuwa wapi Mch. Ezeckiel Maige (SIO Mhe. Ezeckiel Maige) hapo zamani huku ukituachia wana Kondoo Watanzania tukizama kumchanga, Kaburini?
Hivi uwaziri ni haki ya kuzaliwa ya huyu bwana? Kuteuliwa na kufukuzwa ni mambo ya kawaida sana kwa mawaziri, lakini huyu bwana anataka tuamini kuwa hakustahili kufutwa kazi. Jamani, nobody is indispensable. Tena Maige ashukuru kuwa alidumu kwa muda wote huo. Huyu alitakiwa kufukuzwa zamani kutokana na uozo katika wizara aliyokuwa akiiongoza. Ikumbukwe kuwa Rais anaweza kuwawajibisha mawaziri kwa kuwaondoa kutokana na utendaji mbovu wa wale walio chini yao na si lazima mawaziri hao wawe wamehusika moja kwa moja katika mapungufu hayo.
ReplyDeleteMhe. Maige, usijitie aibu bure kwa kusema hovyo, usifikirie watu hawakujui toka ulipokuwa kwenye maisha ya kawaida hadi kwenye utajiri wa kutisha ilionao sasa katika kipindi kifupi mno cha miaka miwili tu ya UWAZIRI WAKO
ReplyDeleteWewe si mtu wa kumtaja Mungu hata kidogo kwa UKATILI WAKO....
mwaka 2011 wewe ukiwa waziri wa mali asili na utalii huwezi kukwepa kuwajibika kwa nafasi uliyo kuwa nayo ,na kama ulikuwa unajua kuwa kwa nafasi hiyo huna kazi wala jambo lolote la kufanya Wizarani , kwanini hukujikataa nafasi hiyo tokea mwanzoni..??? Biashara ya wanyama pori ipo kisheria tena kwa sheria ya bunge na imekuwepo hata kabla hujazaliwa, hivyo kuifunga na kujisifu wakati kitendo hicho kimewanyima ajira watanzania kwa maelfu,na kuinyima nch fedha za kigeni
Hilo siyo jambo la kujisifu hata kidogo...
Ulijipa tabu ya nini kuingia ktk Siasa na Ubunge?
ReplyDeleteUmeyaona matokeo yake?
Mhe. Maige ungalitambua ya kuwa una uwezo mzuri wa Kiroho ni bora ungalifungua Kanisa badala ya kujikita ktk SIASA!
Jamani na yeye ni binadamu anaelezea hisia zake, inawezekana kuna ukweli katika hayo. Nchi hii ni ngumu sana lolote linaweza kutokea katika serikali yetu hii iliyojaa rushwa na ufisadi wa kutisha. Hata hao waliobaki sio wasafi, serikali yote imeoza.
ReplyDeleteBwana Mkubwa Mhe. Maige kwa kutokuwa muwazi kwa masuala yaliyojiri hata hiyo 2015 ni vigumu ukawashawishi hao Wapiga kura wako Jimboni kwako!
ReplyDeleteMAFAO YAKO KTK KAZI NI 'WIZI' ULIOUFANYA NA NYUMBA YA US$ 700,000 ULIYONUNUA, IMEBAKI SASA UKAFANYE KAZI YA UWINDAJI PORINI AU UKALIME MAHARAGE MSALALA.
NI KUWA UMESHAPOTEZA!
Hehehehenhe!
ReplyDeleteKutoka kwenye Uwaziri hadi kwenye Uchungaji.
Hii ndiyo Bongo Tambarale!
Ohhh
ReplyDeleteKumbe Walokole wengi?
I think your family or relatives should consider taking you to a mental specialist before it is too late.
ReplyDeleteMilioni 290 kila mbunge alikopeshwa! Analipa kwa dhamana gani? Sisi watumishi wengine tukiomba hata milioni tano tu tunazungushwa na mwisho hatuzipati. Mh Maige kwa hili usimshirikishe Mungu kwani kitendo cha kukubali kukopeshwa milioni 290 wakati Muhimbili kuna watu wanakufa kwa kukosa huduma ni dhambi kwa Mungu. Hivyo basi kama umetendewa wewe usilalamike kwani na wewe umeshiriki kuwakandamiza wanyonge.
ReplyDeleteNaamini ni msomaji mzuri wa Biblia, na kama ndivyo ilikuwa huna sababu ya kujitakaswa kwa wanadamu kwa sababu kuna huna ulichokifanya (unajua wewe na mungu wako) ukweli utakuja kuwa wazi kinachotakiwa ni kuwa mvumilivu tu kwa sababu imeandikwa vita si dhidi yako mwachie mungu afanya kazi zako
ReplyDeleteViongozi wengi wa Tanzania mnaamini sana uongozi mzuri ni wewe kuwa waziri, but your very wrong Jamani watendaji wenu wa chini ni wabovu sana, wanawaangusha ni watendaji wa chini na wewe kama kiongozi ni lazima uubebe huo mzigo, hata YESU alikubali kusurubiwa kwa ukombozi wa dhambi zangu mimi na wewe, Uwaziri mbele za mungu is NOTHING. Na kwa jinsi ulivyoandika maelezo yako bado inaonyesha una roho ya Uchungu kwa yaliyotoke which means unajiweka wewe mwenyewe kwenye vifungo. Omba mungu akuondolee roho ya Uchungu, na akusamehe ili uwaachane na yote yaliyotokea. HUNA HAJA YA KUSEMA YOTE HAYA.
Huyu jamaa kasahau anaongea naa watanzania, sio wakristu, kachemsha eti ndo anaenda kuwakilisha jimbo sasa, ina maana hakufanya huo uwakilishi kabla ya hapa, analeta janga ya kuincorporate emotions ili apate support kasahau bongo watu wanakwenda shule so wanataka facts. get matured and then talk.
ReplyDeleteHuyu anajaribu kujisafisha kwa kwa makali ya kisu,hamna jipya analolisema,kama kweli hakuwa yeye kwa nini hakuwa tayari kuyasimamia na kuyatangaza tangu awali,baada ya kupigwa chini leo ndo aje na maneno yake hapa ya kujifanya yeye ni mwana mtiifu wa mungu....MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI,wale wanyama kwenye zile ndege kwenda nje ndo ilikuwa bonance yako,kajipange upya na umuogope Mungu kumshirikisha kwenye dhambi haswa kama ulizozitenda
ReplyDeletehahahahahaha Ezakiel wewe ni sehemu ya madudu ya miaka ya nyuma 2010 kwasababu kipindi hicho ulikua naibu waziri katika wizara HIYO, na kama kweli wewe ni msafi hayo madudu ungeyaanika kipindi hicho kuonesha haukubaliani nayo na hapo ungekuwa shujaa. It is too late huo ni utetezi dhaifu wala hatuuhitaji kwakweli. Fanya mambao yako uliingia kwa mbwembwe sana pale ukaona watu woote wachafu sasa utajua nani mchafu kati yao au wewe TAFAKIRI.
ReplyDeleteBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wako zaidi ya 300. Tukiwakopesha wabunge 300 kila mmoja milioni 290 tunapata: 290 x 300 = 87,000,000,000/=. Je fedha hizi zisingejenga flyovers hata kwenye junction moja Dar na kupunguza msongamano? Na bado kila mwezi wanapata mshahara. Wakihudhuria vikao vya Bunge wanapata allowances zisizopungua laki moja. Hawa kweli ni watetezi wa wananchi?
ReplyDeleteEzekiel, sema ulichofanya hapo wizarani kiliko ambavyo hukufanya. Maelezo yako ya kumaliza nishati yako kupambana juu chini etc... yana jitegemeza (subjective), Labda nishati yako ndogo! acha wenye labda uwezo zaidi yako waendelee. Kurudi sasa kuwahudumia wa Msalala inaonyesha bayana uwezo wako mdogo wa kuhimili wizara na jimbo lako kwa hiyo maamuzi ya rais kukurudisha kuwatumikia wa Msalala ni sahihi kabisa. Punguza nadharia za kidini; utumishi kwa umma wahitaji sala na kazi, ungefanya kazi pia acha kusali tuu.
ReplyDeleteGURUDUMU LA MAISHA YA SASA KULISUKUMA:
ReplyDeleteMlishashauriwa maisha ya sasa zimebaki 'SACCOS' tatu (3)
1.Siasa
2.Michezo
3.Dini
Sasa Bwana Muhishimiwa, Uchumi ungalipo kama Saccos No. 1 IMEKATAA UNANGOJA NINI?, MOJA KWA MOJA NENDA SACCOS NO.2 AU NO.3 HAPO JUU.
ZAIDI YA USIHANGAIKE SANA, WEWE NENDA SACCOS NO.3 (Dini)...Kule kuna Fedha za Haraka kama Vodacom M-Pesa za kukusanya hakuna Ukaguzi wa Wahasibu...KWA MANENO YAKO ULIYOTOA HAPA NDIO UTAPIGA BAO!
hakuna lolote unatafuta sympathy no more ulaji kwishney, kilichobaki nenda jimboni kwako katekeleze ahadi ulizowaadi wananchi wako vinginevyo utakosa na hiyo kiti ya ubunge huko mbeleni. hi hayo tu. aliye juu mngoje chini ...oops mpandie hukohuko!
ReplyDelete...ANAJIKOSHA NINI? AENDE ZAKE HAKUNA CHA KUONEWA KAVUTA CHAKE MAPEMA
ReplyDeleteUsijifanye "MWENZETU" kwa kutumia mgongo wa KI-DINI DINI. Wewe si MWENZETU. Unapenda KUJINEEMESHA wewe na familia yako. Kwa kipindi kifupi umenunua HEKALU la dhamani kubwa. Huyo YESU unayetumia mgongo wake hakumiliki MAHEKALU kwa hiyo acha kutaja jina lake. Na kama hizo hela za kununua HEKALU ulipata kwa MKOPO na inabidi ulipe kwa rIba kubwa kila mwezi, uta ni-convince vipi mimi mtanzania kwamba hautavutika kupotea RUSHWA ili ulipe huo MKOPO? Hii ni obvious; greedy, lavish life breeds corruption.
ReplyDeleteNdio maana Nyerere alishauri watu wachapwe bakora washike adabu. Vijijini umasikini unaendelea kupamba moto siku hadi siku wakati wengine wanajifikiria wao na familia zao kwa kuishi kitajiri na MAHEKALU. Please give us a break!
By Nyerere lover
Spokesperson - Nyerere Club.
Hii yote inaonesha incompetence walio nayo viongozi wengi tunaowategemea eti watuendeshee nchi. Hebu jamaa wanaobaini vyeti vya kugushi wafanye kazi yao! Nafikiri watapatikana wengi. Sitegemei mtu kuwa na attitude ya hivi kwamba "kamuhogo" kakichukuliwa ndo unajifanya mtu wa watu.
ReplyDeleteInabidi tufike sehemu hawa watu wachujwe kwa vigezo vya kielimu na uelewa na si kusoma na kuandika tu au alama nzuri kwenye vyeti.
Mh. Mbunge umewadhalilisha wananchi wako na uwaombe radhi kabsaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
wewe unataka kujenga beef na CCM sababu unaona huna fyucha tena kwenye siasa za CCM. U have nothing to look forward to within CCM!!!!!!!
ReplyDeleteSasa unajifanya critical halafu baadae uingie upinzani!!!!U want to change game with your cards. Janja yako wewe.
Kaka Maige onyesha ukomavu wako kisiasa ufanye mambo yatakayokufanya ukumbukwe. Hali yopita yaache hiyo ndiyo Si-Hasa.
ReplyDeleteMAIGE HEBU TUAMBIE NA ILE BENZI MPYA PALE DT DOBIE S350 NAYO UMEKOPESHWA NA BENKI GANI NA MODALITY YA MALIPO! KWANINI ULIWAAMBIA WAITOE SHOWROOM? ACHA STORY NDUGU!!! MADARAKA MABAYA SANA BAADA YA KUPATA UWAZIRI HATA WASHKAJI WA IFM UKAWA HUTUKUMBUKI TUKIKUSALIMIA! MALIPO HAPA HAPA!
ReplyDeleteTunachoshuhudia hapa ni matokeo ya kuweka mbele maslahi ya wanasiasa kuliko ya wanataaluma. Tumeshuhudia wanasiasa wengi waanavyolalama pale wanapotetereka kwenye na kuachuia nafasi walizonazo. Ama kweli wanasiasa ni wanafiki, hawamjui yesu wala Muhammad (SAW) hadi wapate misukosuko. Kawatumikie watu wa jimbo lako kwa amani kwa kipindi hiki kilichobaki na baada ya hapo upumzike siasa. hatuhitaji uzandiki huu!!!!!
ReplyDeleteMfamaji haishi kutapatapa. Nani alikwambia kwamba ulipewa uwaziri wa maisha, cheo ni dhamana ngosha, umeshindwa kuitumikia dhamana uliyopewa sasa kaa pembeni wenzako waitumikie. Mimi nilitabiri haya mapema tu tangu Magige alipopewa Uwaziri full wa Maliasili. nilijua kuwa utamshinda. We mtu unamtoa shamba na kumleta mjini na kumpa dhamana ambayo ni ngeni kwake atahomola tuu.
ReplyDeleteAhaaa
ReplyDeleteWewe Mhe. Maige unaielewa Biblia vizuri tu halafu tena ndio mwenyewe unaikiuka kwa kutenda wizi?
Au ndio yale yale ya fuateni Neno nilisemalo na msifuate niyatendayo?
Mwadela Maige. ule Mola? Pole sana ndio siasa hizo.
ReplyDeleteni nani huyu?keshawahi kuwa waziri?duh sijawahi kumsikia
ReplyDeleteMnyonge nyongeni lakini haki yake mpeni.
ReplyDeleteKwani nani ni Abel na Cain ni nani?
ReplyDeleteWITH ALL THE RESPECT WADAU,MAIGE IS HOPELESS I WONDER MTU KAMA HUYU RAISI ANAWEZAJE KUMCHAGUA KUWA WAZIRI,AM DISSAPOINTED ,REALY I AM.HAYO MAELEZO YAKE HAPO YANANIPA HASIRA TU KWA KWELI,NCHI YETU NI MASKINI SANA JAMANI,WE ALL KNOW THAT,HAKUNA KUMUONEA HURUMA MTU JAMANI ,HUYU JAMAA KAIBA PESA NYINGI SANA,NA HAKUNA ALICHOKIFANYA KAMA ANAVYOONGEA COZ MIMI NI MTANZANIA NAISHI NJE YA TANZANIA,WAZIRI WA UTALII NA MALIASILI ANAPOFANYA KAZI SISI HUKU NDIO WATU WA KWANZA KU DETECT ,,MAIGE PLZ STOP TALKING
ReplyDelete''Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo'' By Ezekiel Maige ; Kimsingi nakushangaa kwamba mpaka sasa wananachi wa Msalala ulikuwa hujaanza kutuwakilisha, ila umetolewa Uwaziri ndio unasema Unaanza kutuwakilisha. Mimi ni Mwana-Msalala natokea kijiji unachotoka wewe Kijiji cha Segese (jijrani na Mzee Makune), wewe si kiongozi bali unalako jambo. Unataka kutuambia kuwa Tanzania yenye watu zaidi ya Milioni 40 wewe tu ndio unafaa kuongoza kiasi cha kusema kuwa hapakuwa na haki wewe kuondolewa wizara hiyo? Hata kama utendaji wako ni mzuri kumbuka cheo ni dhamana na inapotokea dhamana hiyo unanyang'anywa huna budi kuiachia. 2015 tutakutana Jimboni, lazima nikung'oe ubunge.., nadhani hata nyumba uliyonunua utaweka rehani kupambana nami katika nafasi hiyo lakini lazima nikung'oe kwani nina nguvu isiyo kifani na siwezi kushindana na wewe.
ReplyDeleteNimeipenda hii "waiba machungwa shambani, ukiulizwa, nimekuta yameanguka nikayaokota ili yasioze, mimi si mwizi', sasa shambani umefuata nini??? Kweli, dont mess up with people...
ReplyDeleteMwacheni ajieleze,mpeni haki yake.Kwa nini mnamhukumu.
ReplyDeleteChunguzeni kwani majungu duniani hayapo?Labda kweli kaonewa na kakaangwa na mafisadi je!
Chunguzeni anayosema pengine ni kweli.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Chunguzeni kwanza badala ya kumzika mtu mzima.Hajafa bado.Akidanganya si atakamatwa kama Mhe.Nalaila Kiula!
Mh Maige umeona Watanzania ni wadanganyika kiasi hicho? Kwa kusema "Waziri gani aliyefikisha makampuni yaliyosafirisha twiga..." ni kuwadhalilisha Watanzania; kuwaona Watanzania ni vilaza.
ReplyDeleteMimi mweneywe nilishudia ukikana usafirishaji wa twiga nje ya nchi, kwa kusema twiga hawezi kusafirishwa kwa ndege kwa kuwa twiga ni mkubwa sana.....
Au umeyasema haya kama kipima joto? Omba Mungu kuna urasimu na kupeana madaraka ki-kada, pia kuna mapungufu makubwa sana katika Katiba ya sasa, MAKAZI YAKO YANGEKUWA UKONGA TANGU SIKU NYINGI. Je umewahi kwenda kumtembelea Mramba na Yona??
nazani baada ya miaka kadhaa Tanzania itakua haina wanyama hai bali wafu na mapori tupu tukiendelea na huu mchezo wa kuwauza iwe kinyume na sheria au kisheria sidhani kama Serikali inafanya jambo la maana kuwauza hao twiga, tembo etc...ndio maana tunarudi nyuma watalii hawaji tena kwetu natamani wanichague mimi niwe waziri wa mali asili na utalii yaaani Tanzania ingekua ya kwanza Africa nzima. kikwete wafukuze wote wasiotenda haki ...na kama wewe Maige hukutenda kosa basi omba Mungu tu akusaidie na hakuna haja ya kuwaonesha watu kuwa huna kosa kwani hawatakuamini Mungu na wewe mwenyewe ndio mnajua ukweli na uongo uko wapi sanasana watu watakuponda na kukuvunja moyo wewe bado ni kijana so endelea kulitumikia taifa ipasavyo na kurekebisha yale mabaya uyaonayo ....
ReplyDeleteAti nini?
ReplyDeleteMwanzo 4:1-15?
Ebo?
Angalieni matatizo yetu sisi binaadam.
Mtu wakati unafanya wizi haupo kabisa na Mwenyezi Mungu!,,,inatokea unabumbulukiwa ndio sasa unazinduka unarejea kwa Muumba!
Hivi ulivyokuwa unapanga ule wizi wa zile DOLA LAKI 7 ulianza kwa kusema 'Mwanzo 4:1-15???
Bwana Mkubwa, ktk kipindi choote cha Uongozi wako Wizarani sijawahi kusikia ktk vyombo vya Habari wala ktk Runinga kama hapa ukinukuu Mistari ya Kitabu Kitukufu!
kama ulikua mzalendo wa kwelii maige naamini usinge yafumbia macho maovu eti kwa kuwaogopa wenye nguvu,mwanahalakati wa kweli haogopi hata kupoteza maisha yake kwa kutetea haki za watu anaowaongoza, ni bora hata ungetupigania mpaka ukafa,tungekukumbuka daima kama:mkwawa,sokoine,nyerere n.k sasa ona umeshindwa kua mzalendo tutakuzarau mpaka ukome ,eti mtumishi bora unaboma maghorofa kafie mbali
ReplyDeletewewe ni mfano tosha wa judgement na weledi wa watu wanaotuongona kwenye ngazi za juu. huu waraka ni purely childish. kwani wewe ulikuwa waziri kama "volunteer?" si ulikuwa unapata mshahara mnono tu kwa wewe kutekeleza wajibu wako? hujui kama nafasi za kisiasa unaweza kubadilishwa wakati wowote? au ulitaka ubaki waziri maisha? wizara ni kampuni yako? au ulitaka uagwe kwa sherehe ya kitaifa? kwa nini unakuwa so desperate? una business gani unfinished kwenye wizara?
ReplyDeleteEti poleni kwa mshituko nani kakuambia tulishtuka, sijui wenzangu ila mimi niliposikia mmeenguliwa nilienda kusherehekea kwani yalikuwa maombi yangu maana mnaitafuna nchi hadi inatia aibu. Hivi mkiapishwa kuwa mawaziri/wabunge hamuapishwi tena kwa maandiko matakatifu? Mbona hamjui mshahara wa dhambi kuwa ni mauti? Na bado usipoangalia vizuri na ubunge utavuliwa soon. Chadema itawapindua soon msipokaa sawa
ReplyDeleteMheshimiwa,
ReplyDeleteSijakubaliana na mantiki ya waraka wako huu. Waraka wako haonyeshi kuwa ulielewa kuwa cheo ni dhamana. Na hili ni tatizo kubwa tulilo nalo Tanzania. Wizara yako ililamikiwa na wabunge na hata kwenye vikao vya ndani vya CCM. Na hata kama huna makosa Rais anamamlaka kukuachisha kazi. Kwa hiyo ulitakiwa kuchukua responsibility na kukaa kimya. Mimi nadhani kama uliyoeleza ni kweli ungeshukuru mungu kuwa umetua mzigo na sio kulalamika. Mbona watu kwenye private sector wanaachishwa tena may be kwa makosa lakini hatuoni wakilalamika. Mshahara wa Waziri wa halali ni mdogo sana. Kwa Elimu uliyonayo you can make more money nje ya Uwaziri so kwa nini unalalamika?
Mheshimiwa Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige ni kwamba lazima utambue kuwa za mwizi ni siku arobaini. Uliyokuwa unafanya na unayofanya ni miongoni mwa watu hivyo wanaona yote. Ni mengi umefanya ambayo si mema na ni tofauti na unavyojisifu kwenye maelezo yako.
ReplyDeleteKwa ndugu wasomaji, huyu bwana Maige ni muongo na ni fisadi mkubwa. Nina mambo mawili napenda wasomaji myajue na ni ukweli mtupu.
(1) Huyu Mbunge ana nyumba nyingine mjini Mwanza mtaa wa Rufiji karibu na Hospitali ya Kilonzo ambayo in ghorofa nane na ambayo ndo inaisha sasa lakini ametumia jina la Kilawa ambaye ni ndugu yake. Hivyo wakati mnaendelea kuhangaika na nyumba ya hapa Dar es salaam, mjue pia kuna nyingine ambayo ndo inaisha sasa Mheshimiwa hiyo kataa nayo!
(2) Mheshimiwa alikuwa ni msimamizi mkuu wa Sheria ya Wanyamapori. Jambo ambalo linawasikitisha watu wengi ni pale wewe unapoamua ng'ombe zako nyingi ambazo umezipata kwa njia ya ufisadi pia kuhakikisha zinachungia ndani ya hifadhi ya Moyowosi. Taarifa zinaonyesha kuwa ulikuwa unatumia nafasi yako kwa kuhakikisha hazifanywi chochote.Pia wafugaji wa eneo lako wamekuwa wanakutumia wewe kama kinga na hivyo kujaza mifugo humo. Niliposikia umeitisha mkutano uliofanyika Iringa kuhusu mikakati ya kupambana na mifugo ndani ya hifadhi zetu ndipo nilipoamini wewe ni mnafiki sana. Sasa tunasubiri itakuwaje baada ya kuacha madaraka. Nini kitatokea, sijui.
Ndugu wasomaji, msidanganywe na huyu mshirikina. Nguvu zake zimeisha za kishirikina na amekiuka masharti ya kazi yake kwa kiasi kikubwa tokana na madaraka aliyopewa.