Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Wabunge wa Chadema Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.
Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)


Mhe. balozi Mwanaidi S. Maajar, hakikisha wana Chadema wote(akiwemo Joshua Nassari) watoke Ofisi kwako Ubalozini wakiwa kila mmoja na kadi mkononi ya CCM !!!
ReplyDeleteJAMANI MBONA ZITTO HAONEKANI KWENYE HIZI PICHA? BAADA YA KUCHANWA SANA KAONA ATOKOMEE??? YEYE AMEJIHARIBIA MWENYEWE KW AKUWA MROPOKAJI. NYOTA YAKE IMECHUKULIWA NA WAKINA MASHAKA. ILA USHAURI WANGU KWA WANACHADEMA NI KUMUOMBA JANUARY MAKAMBA NA JOHN MASHAKA WAHAME CCM WAENDE CHADEMA KWANI WAO NDIO MAWAZO MBADALA NA CHACHU YA KIZAZI KIPYA
ReplyDeleteVijana wa Mbowe mnapendeza ndani ya suti. Inabidi muachane na magwanda yanayowafanya muonekane kama wana mgambo.
ReplyDeleteHahahaha Magwandazzz ukivaa Marekani unaonekana mtu wa Joseph Kony Mpiganaji wa Msituni!
ReplyDeleteKwa hivyo unaweza kukamatwa kimakosa ukifananishwa na Mfuasi wa LRA -Lord Resistance Army Uganda ya Joseph Kony!
Ndio maana Chadema wakiwa Marekani wanachomoa magwanda wanayaweka ktk mabegi Airport wakifika wanavaa suti!
Upo hapo?
na hapo ubalozini watu wanaingia wamevaa kama wanaenda beach?
ReplyDelete