Wajumbe wa Kamati ya Bunge la Tanzania ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Edward Lowasa (wa tano kushoto) wakikaribishwa kwenye Kikao na Spika wa Bunge la Seneti la Nchi ya Morocco,Mheshimiwa Mohamed Yatim (kulia).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Edward Lowassa (wa nne kulia) na Makamu wake,Mh. Mussa Zungu (wa tatu kulia) katika kikao cha pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Wawakilishi la Nchi ya Morocco. Kamati hii ipo ziarani nchini Morocco.
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Edward Lowassa wakiwa kwenye kikao na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati za Bunge la Wawakilishi wa Nchi ya Morocco.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Nchi ya Morocco,Mh. Mohamed Yatim (kushoto).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Seneti la Nchi ya Morocco,Mh. Mohamed Yatim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    Tujiulize hii kamati imekwendaMorocco kufanya nini? Tanzania ni watu wa mdomo tu na kupiga picha na kutumia pesa za walipa kodi. Hawa wote wamesafiri na busines class kila mmoja na nauli si chini ya dola alfu 7 kila mmoja wao na maposho juu. Jmani Tanzania imekosa mwelekeo. Wanasemwa kina MAIGE LAKINI wANASIASA WOTE WA BONGO NI KAMA MAMBA WA MTO NILE . Yaani nchi hakuna linalokwenda huoni tija ya kazi tunazofanya.Mvua ikinyesha kidogo tu jiji lote linaele ndani ya maji wakati bahari iko pua na mdomo kuweko miundo mbinu ya maji kwenda baharini.Badala yake ni waandishi wa habari kupata news za kuandika kutokana na mvua. Yaani nasema kwamba Tanzania inanuka na sisi wenyewe ndio waokozi.Vyama vingi mbali ya kufanyika kwa uchaguzi havijaleta tija. Kamati za Bunge zinaegemea masilahi binafsi na kushinikiza tenda apewe nani.Jee hatuna utaratu wa dhati wa kufikia maamuzi?. Inatia uchungu kuona kwamba nchi yetu imekuwa ziko la misumari. Tunahitaji mabadiliko ya kifikra kwa viongozi wetu. Mwendelezo wa uongozi kununukiwa kwa fedha inamfanya mwanasiasa ajione ana jukumu la kulipia gharama zake kwanza.Hao kina Zito na wenzake washike nchi leo tuone kiama chetu. nI WALAFI KULIKO HAO WA CCM. Hebu jamani tumuogopeni Mungu. Jaii nayo imekubali kufuga wezi wa mali za Uma.Mtu anaeiba na kutembea kwa madaha mitaani naonekana ni mjanja na mwenye mafanikio namambo yake ni mazuri. Wahalifu wanafugwa na Serikali kwani haichukui hatua yeyote. Jamani hali inatisha. Watu wanamnyooshea JK kidole basi bora tangaze hali ya hatari na kutwala kwa iron fist na kuagiza Bandari ijengwe,ATC ndege ziruke na reli zijengwe. Tutamlaumu Rais mpaka TUNACHOKA SAWA NA KULAUMIWA KINA MAXIMO NA PAULSEN. Badala ya kuangalia root cause ya matatizo tunataka tuone matokeo tu. Intisha.JK Tunakupenda ila ndio hivyo yanayokufika wewe ni kama ya kina Maximo na Paulsen. Pole sana ndio mambo ya Dunia hayo unajifunza mambo. Wanaokulaumu hawajui wanasema nni ni wazuri wa kulaumu kama watazamaji uwanjani wanayolaumu wachezaji wakati wao kukimbia dakika tano pumzi juu. Jipange upya, weka timu yakovizuri umalize slama na Mungu atakusaidia lakini kusema kweli collective leadership hakuna. Na jingine hawa maprofesa na madokta warudi vyuoni wakafundishe.Nadharia na vitendo ni vitu vwili tofauti na wataendelea kutuyumbisha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2012

    We anonymous wa 1. Naona unachanganyikiwa maana ulichoandika hakina flow. Soma mwenyewe kisha ufanye evaluation ya ulichokiandika kama kinaeleweka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2012

    Morroco wana ujuzi mkubwa wa kuchonga/kungarisha madini kama almasi ili kuongezea thamani ya mali ghafi kama almasi zetu.

    Tatizo hakuna uwazi wa shughuli za serikali au kamati za Bunge ingawa Tanzania juzijuzi ilikuwa Brazil kukazia haja ya uwazi wa shughuli za serikali au taasisi kama kamati za bunge 'Open-Govt'aka transparency.

    Ipo haja ya vyombo vya habari, bunge kuhoji ziara hizi mara wanaporejea nchini ili kujua tija ya ziara hizi za 'kikazi' ngambo.

    Pia ingekuwa jambo bora kuwataarifi wananchi juu ya ziara hizi kabla 'viongozi' hawa hawajakwea pipa kwenda ngambo ili kuondoa 'usiri' wa ziara hizi maana wanatumia kodi za walipakodi ambao ni wananchi wa Tanzania.
    Mdau
    mfuatiliaji wa ziara.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2012

    Ehee bwana hano juu nenda shule kasome elimu haina mwisho.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2012

    What if? Just what if MKUU chose to open a new WELL-FUNDED, stand-alone Ministry of Performance (Wizara ya Utendaji) led by a CHIEF PERFORMANCE OFFICER (a new position that answers directly to the Raisi) RESPONSIBLE for helping the rest of the Ministries and all public institutions to continually raise their performance levels? What if? Just what if Raisi chose . . .?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2012

    Nalia Mimi! Hivi hawa wakoloni wa ndugu zetu wa Sahara ya Magharibi leo wamekuwa maswahiba wetu? Hawa jamaa hata wamejitoa kwwnye Umoja wa Nchi za Afrika! Tunakwenda huko kusema nini? Nakubaliana na annony kwamba safari hizi ziwe na maelezo kabla hazijafanyika. Kwa nchi ambayo miaka mingi tumeipigia kelele Western Sahara haiingii akilini kwamba leo tuna ujumbe mkubwa wa Wabunge wetu unaoweza kwenda Morocco bila wananchi kupata maelezo ya wazi! Ama Serikali ina sera yake ya mambo ya nje na Bunge linayo nyingine ya kwake!! Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2012

    Mimi huwa nashangaa watu wanavyolalamika wakati mipaka haina senyenge wala miba. Kuna aina mbili za walalamikaji wa kwanza ni wale waliotoka bongo wakabahatisha kwenye Marekani au Uingereza na hawajawahi kwena nchi yoyote, watu hao mara nyingi wanachotaka Tanzania iwe kama Marekani au Uingereza. Haina ya pili ni wale ambao hawajaenda popote, mawazo yao ni kwamba ukitoka nje ya bongo basi umeula. Kwa mawazo yangu Tanzania inafanya vizuri kuliko nchi nyingi duniani nilizotembelea.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2012

    Wed May 02, 05:51:00 AM 2012
    umeandika vizuri sana.Nimeipenda article yako.

    David V

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2012

    Sasa annony wa May 1,2012 07:51 PM amesema nini? Hana upeo wa chochote. Ametaka kueleza tu kwamba yeye katembea duniani!! Hajajibu hoja zinazodai tija ya safari lukuki za wabunge hawa wakati ambapo wananchi wetu wanalilia maisha bora na viongozi wakijitanua tu. Hata kama waliopo Maerkani na Uingereza wanataka tuwe kama nchi hizo haoni kwamba kuna bora katika hilo ambapo nchi hizo zina Serikali zinazowajibika kwa wananchi wake! Hili kwake ni upungufu! Na anadai ana mawazo baada ya kusafiri sana duniani! Kheri angekaa kijijini kwake na kukatia mifugo nyasi tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...