Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kuwakaribisha wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka makampuni 13 ya nchini Afrika Kusini ambao wamekuja Tanzania kwa ajili ya matembezi ya kujifunza mbinu mbali mbali za kilimo na kuangalia fulsa za kuikwamu Tanzania katika mpango wa kilimo kwanza.
Katibu Mtendaji wa Tanzania Youth Agriculture Foundation (TYAF) Bw. Gasper Mahekula akitoa maelezo machache ya taasisi yao mbele ya wakulima kutoka nchini Afrika Kusini pamoja na waandishi wa habari ambapo aliwakaribisha wageni hao kuwekeza katika kilimo.
Mkutano wa waandishi wa habari pamoja wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka Afrika Kusini.
Wageni wakifuatilia mkutano huo.
Wa kwanza kulia ni Mtaalam wa Mambo ya Utawala wa Kilimo wa Kampuni ya IIQ ya Afrika Kusini Bw. Ockie Olivier ambaye ameongozana na wenzake wakifuatilia mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. Braam Coetnee (kushoto) akiwa na mmoja ya wenyeji wao (katikati) pamoja na Kiongozi anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. John Luscombe jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2012

    Halhala wasijetuletea ya Zimbwabwe, manake tungeshughulikia kuwakuza wakulima wetu kabla ya kuleta wageni. sioni mwisho mzuri wa sera hii ya kilimo kwanza

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2012

    KUMBE MDAU TUKO PAMOJA WATATULETEAJE WATU WA NJE? MBONA ZAMANI CHAKULA KILIKUWA KINATOSHA? AU NDO 10% MAKE WATANZANIA HATUCHELEWI

    JAMANI TUSIUZE NCHI YETU KWA MAKABURU

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2012

    Jamani huu ni uwenda wazimu kabisa. Watanufaika makaburu na wajanja wachache wa kitanzania. A very bad idea. Kaburu matata! Hawa watu hawajabadilika kichwani wala moyoni. Ila watanzania kuwakumbatia bila kufikiria. Hatujasoma ya Mbarali yaliyoandikwa kwenye Raia Mwema? A very bad idea. Tutalia kilio cha kusaga meno! Ifutiliwe mbali hii tabia ya kuwakumbatia tu hawa watu wabaguzi. Tujenge chetu sisi wenyewe. Tanzania haina wajomba jamani tujitegemee!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2012

    The Boers look most unimpressed by whatever has been presented to them by their Tanzanian hosts. The body language does not augur well. Tatizo la watanzania kuangalia mambo juu juu tu! Kaburu bado hajasamehe mswahili kutwaa madaraka kule bondeni na watanzania hamjui bado maana ya kisasi mpaka mtakaogutuka Kaburu anawafanyia nini. Kisasi cha Kaburu kinaendelea kimykimya hata hivi ninavyoandika. tanzanite si yenu tena, benki kubwa iliyokuwa yenu si yenu wameichukua tena kwa bei ya chini mno, Mwalimu wenu mpendwa hamnaye tena na bado.... sasa na ardhi yenu mtawapa. Wake up guys msidanagnyike na lawalawa na visoda. Mnauza nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...