Na Mwandishi Wetu

JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' ambalo litafanyika Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na bado milango iko wazi kwa warembo wengine wanaotaka kuwania taji hilo ili kutoa nafasi ya kupata mwakilishi atakayefanya vyema kwenye ngazi ya kanda na taifa hapo baadaye.

"Bado hatujafunga milango, tunawakaribisha wasichana wenye sifa kujiunga ili tuweze kupata mshindi atakayepeperusha kitongoji cha Kigamboni vizuri," alisema mratibu huyo.

Alisema kuwa kampuni yake ya K & L iliyopata baraka za kuandaa shindano hilo imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.

Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa Miss Temeke mwaka 2003 kuwa ni pamoja na Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili, Doreen Kweka, Agness Goodluck, Khadija Kombo, Lina David, Aisha Mussa, Edda Silyvester, Fatina Francis na Rosemary Deogratius.

Alisema kwamba shindano hilo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine, Screen Masters, Clouds FM, Times FM na NSSF.

Taji la taifa la shindano hilo linashikiliwa na Salha Israel ambaye alitokea katika Kanda ya Ilala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...