Assalaam alaykum kaka michuzi ,nimeletewa picha na mdau alikuwa safarini kuelekea mbeya alipata picha hii ya negligence overtaking ambayo ilifanywa na madereva watatu kwenye kona na mlima mkali maeneo ya iyovi iyovi. 
Nilichokuwa napendekeza ni kuwa kama kuna utundu wowote ili watu wa usalama barabarani especially afande Mpinga kama atakubali picha hii ikapata bango kuubwa pale ubungo terminal huenda ikasaidia abiria ku-notice kampuni ambazo zina madereva wazembe kama ambavyo hayo magari yanaonekana hapo basi iwekwe.
Naamini na wamiliki wa ma-bus nao pia wataona jinsi ambavyo madereva wao wanavyoendesha wakiwa safarini maana hilo eneo mbali ya kuwa na kona na mlima mkali lakini pia lina 'two solid lines' ambazo haziruhusu ku-overtake na picha iko clear si ya kuchora bali ni picha halisi.
asante kaka kazi njema ya kuliendeleza libeneke
jfour mdau wa UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2012

    kwa kweli inasikitisha sana, kosa sio la hao madereva tatizo ni system yote ya hiyo nchi madereva hawajapewa darasa kuhusu road marking hawajui what that solid line mean. labda hawajui hata kusoma leseni zenyewe walipewa kabla hata hawajajua kuendesha hayo mabasi kwa hiyo mdau wa uk inabidi sisi turudi huko tuka ombe tender ys kuwaelimisha madereva kuhusu usalama barabarani. tutafika lini jamani

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2012

    Yaani asilimia kubwa ya madereva wetu ni wazembe sana yaani hati mtu unapata woga kusafiri

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2012

    Tatizo ni ule mgawo wa kila mwezi/mwaka kwa mabosi. Hakuna anayetaka upungue.

    ReplyDelete
  4. Mdau SUMATRAMay 02, 2012

    Mdau asante sana kwa picha hii na kwa kuangalia tu mabasi yote na kampuni husika zinafahamika na binasfi nitawasiliana na kamanda Mpinga ili 'kazi' ifanyike.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2012

    HIYO PICHA MIMI MPAKA IMENITETEMESHA

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2012

    exlent capture, nimezipenda sana hoja za alieposti hii picha. kwa kweli itasaidia kuonesha uhatari wa uzembe unaofanywa na madereva wawapo safarini. biggerup

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2012

    Du, ahsante sana mdau kwa picha nzuri lakini ya hatari! Basi kwa asiyeijua Bongo, vitu kama hivi ni vya kawaida kabisa hasa kwa safari kama hizi za Dar - Mbeya, Dar - Arusha, Dar - Mwanza na kwingineko. Tukiwa safarini uhai wetu huwa tunauweka reheni! Mwenyezi Mungu atunusuru.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2012

    Kama kaburi haliwatishi utawatishia na nini tena, we waache tu ninachosikitia tu kwamba wanaua ndugu zetu, lakini na hao ndugu zetu ni wapumbavu kwanini wasimchape makofi dereva mpumbavu huyu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2012

    Mdau wa UK, wewe ni tafiki? ni mwalimu wa madereva? eti ukafundishe kwa sababu tu umeishi UK, hiyo ni dharau na wewe hauna tofauti yeyote na hao madereva wazembe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2012

    safi sana ..hawa ndio madereva tunaowataka hasa kwani kifo cha aina hii hakina msekule, inajulikana kuwa ni ajali ya gari

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2012

    madereva wanajua yote hayo ila ni ubishi na misifa ya kushindana wakati wamebeba roho za watu.
    Abiria walio garini hawaoni hatari hiyo mpaka yatokee yakutokea.
    Picha ndo hiyo.
    vyombo vya usalama vijenge imani na vitu kama hizi blog then wachukue hatua. ushahidi ndo huo hapo.
    NI HAYO TUU.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 02, 2012

    Wewe mdau wa namba moja madereva hao kwa siku hizi ni lazima wawe wamekwenda VETA ili waruhusiwe kuendesha magari, kwa hivyo siyo kweli kwamba hawajui maana ya hiyo mistari.

    Ni dharau na uzembe tu ndiyo unaotusumbua. Na vile vile abiria kutojali dereva anaendesha vipi alimradi wao wamo tu. Ikitokea ajali ndiyo wanakuwa mabingwa wa kulalamika eti dereva aliovateki kweenye kona kali. Too late

    Wakianza kupigwa faini kali kali watajirekebisha.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 02, 2012

    Hivi hujui kuwa wananchi ndio wanashabikia ga vitendo kama hivyo? Jiulize humo ndani ya mabasi abiria walikua hawajui kinachotokea?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 02, 2012

    Kifo hupangwa na Mwenyezi Mungu lakini wacha tuseme tu,

    Pia life Expectance (Umri wa kuishi) kwa Mtanzania unapungua kwa (miaka 10 chini au zaidi) kutokana na mambo kama haya!

    Hii ndio mwanzo wa chinja chinja za mabarabarani kila kukicha!

    Tanzania ni kama tuijuavyo!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 02, 2012

    Mdau picha hii ni nzuri sana na kwa maoni yangu, kuiweka katika bango haitasaidia lolote kwani utagundua kuwa si madereva wa mabasi yaliyo pichani tu ndio wazembe bali hata wa mabasi mengine pia huwa wana mtindo huohuo. Mimi naona muda umefika kwa jeshi la polisi kutumia picha kama hii kuwa ni ushahidi tosha kuwachukulia madereva husika hatua za kisheria.

    Ukitafakari kwa undani zaidi utagundua kuwa akili za madereva hawa hawawezi kuwa katika hali ya kawaida. Inawezekana kabisa kuwa wametumia aina fulani ya kilevi kinachowafanya washindwe kuona hatari iliyo mbele yao.

    Kuna msemo "kama hujui kusoma hata picha huoni?" Mtu huhitaji kwenda kufundishwa kuwa ku-overtake katika mlima au kona ni hatari, bali ni kitu ambacho hata mtu ambaye hajaenda shule anaona. Alama za barabarani zimewekwa ili kuondoa ubishi kuwa kitendo kinachofanyika katika eneo husika ni hatari au la.

    Sina hakika kama kamera iliyotumika inaweza ku-zoom tuone license number-plates za mabasi haya. Ingekuwa ni vizuri kama namba zingeonekana kwani zitaondoa utata juu ya basi lililohusika.

    Kamanda Mpinga, hii inawezekana. Mara nyingi huwa nasikia ukizungumzia polisi jamii. Huu ndio msaada unaoweza kuupata kutoka kwa jamii. Naamini iwapo utakuwa tayari kuzifanyia kazi picha kama hizi, utazipata nyingi tena zenye ubora wa hali ya juu. Tena hata video utawekewa hapahapa katika globu hii.

    Mimi nashauri wadau wote tuendelee kutuma picha au video za matukio kama haya kwa wingi na tuendelee kupiga kelele iko siku, kama sio kamanda Mpinga, atakuja mwingine atakayekuwa serious kufanyia kazi ushahidi huu. This is an incriminating evidence.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 02, 2012

    Napinga kabisa maoni ya mtu wa kwanza hapo juu kuwa madereva hawajui maana ya solid line. Madereva wa bongo wanajua kabisa maana yake ila kwa kuwa hakuna mtu wa kuwakamata hapo ndio maana wanavunja sheria. Tabia ya kuvunja sheria ipo kwa watu wengi hasa wakiona hakuna Polisi hiyo sehemu. Tabia nyingine ya makusudi ni kutanua barabarani. Watu wanafanya haya mambo makusudi kabisa kwa kuwa hata ikitokea ajali hachukuliwi hatu yeyote ya maana na utamuona anaendesha gari tena kama akipona. Hakuna cha kunyang'anywa leseni wala nini tena tunasema ni kazi ya Mungu...

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 02, 2012

    Yote tisa mimi nimezimia LAMI ni ya ukweli bongo tambarare!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 02, 2012

    Wamiliki wa Mabasi ambao ndiyo mabosi wa hawa madereva ni Mabosi pia wa Chama fulani cha Siasa wakati wa fundraising campaign, hivyo Chama hiki kikishinda uchaguzi unatakiwa kupata ridhaa ya CHAMA ili kuwakamata, kinyume chake , afisa atakayethubutu atakuwa amehatarisha ajira yake. Akisamehewa sana atahamishwa , wengi wamepoteza kazi hata maisha katika kusimamia SHERIA. Hata Mohamed Mpinga SACP ni mteule wa Wanasiasa naye anjua hilo ndiyo maana haya yanatokea barabarani. Mbona leo wanaotanua asubuhi na jioni wapo na maisha yanaendelea? Tena hawa wanfanya hivi kwenye mboni ya jicho la si Kamanda Mpinga peke yake bali Said Mwema IGP. Mungu aihurumie nchi na watu wake!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 02, 2012

    Mimi natafakari maoni ya wadau! Inaonekana kwamba tuna maneno mengi na mawazo mengi lakini elimu ni muhimu sana kwa abiria, derevaz (au niseme jamnii kwa ujumla) Kwa kweli baada ya kuona mahali pengine tofauti na Tannzania tunaishia kulaumu nchi na mfumo wake. Ni sisi tufungamane tulete haya maneno na mawazo katika matendo. Hongo imezidi. Hata ukienda ukiwatishia wenye makampuni polisi ni huko huko wanaenda kuhongana na kesi inajiishia kisailensa. Sijui kwa kweli tukae na hasira, mawazo na maneno hadi yatakapofumuka basi kutakuwa na ma(badiliko).

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 02, 2012

    David V sijakuona hapa kaka...au ndio no comment,

    hatari lakini salama maana sijasikia kama kuna ajali imetokea njia ya mbeya zaidi ya ile ya kihaba juzi baada ya mdau mmoja kulalama sana humu kuhusu uzembe wa dereva mmoja wa basi.

    nina imani tunaweza tukiamua, mimi najiuliza huyu jamaa kaipataje hii picha maana ni ya ushahidi wa kipekee pale mahakamani...

    tukiziweka hizi nyingi mara kwa mara na michuzi asizibanie basi watakoma tu endapo jeshi la polisi barabarani litazifuatilia

    ni mtazamo tu

    ahsante
    hsm

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 02, 2012

    Tanzania inatakiwa kuanzisha leseni zenye point 12 kila dereva akifanya kosa anakatwa point 3 nafikiri kila mwenye leseni ataendesha gari kwa adabu zote mmmmm!! nimesahu kuwa kuna rushwa kibao bongo naona haita saidia kitu

    ReplyDelete
  22. Mimi naomba niseme hivi hii inachangiwa na abiria. Ilikuwa mwezi wa tatu mwaka huu nilisafiri kutoka Dar kwenda Iringa tulipofika maeneo hayo hayo Dreva alikuwa akiendesha kizembe hivyo na overtake za kijinga! Mimi mwenyewe nilisimama nikaenda kumwambia dreva tafadhali punguza mwendo na uendeshe kwa uangalifu! Cha ajabu baadhi ya abiria wenzetu waliniona kituko wakidai wao wana haraka kwa sababu watachelewa kufika. Dereva alichofanya alipunguza mwendo akawa anaendesha mwendo wa ajabu yaani too slow uzuri kwa kuwa mimi nilikuwa nafika Iringa tu haikunisumbua sana nilipofika Ipogoro nikatelemka zangu wao wakaendelea lakini lililokuwa dhahiri wakati nashuka baadhi ya abiria walishukuru kwamba nimeshuka si ajabu hata Dreva.

    Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kiburi wanapewa na baadhi ya abiria wapuuzi kama hao Madreva. Mindset za watanzania nadhani iko tatizo katika kusimamia sheria sijui tumelogwa? Angalia hata miji yetu ilivyo michafu utaona mtu ananunua maji akimaliza anatupa chupa popote yaani wala haimpi shida kabisa yaani tuna tatizo kubwa! Hebu jaribu kumsemesha mtu kama huyo atakavyokutolea matusi ya nguoni? Ni mambo ya ajabu yaani mimi sielewi na ndiyo maana nchi hii kila kitu kinakwenda hovyo hovyo! We are not responsible, we are not serious! Use any language you would like but we have a very big problem MUNGU ATUSAIDIE JAMANI MIMI SIELEWI YAANI TUNATOKAJE HAPAAA....?

    ReplyDelete
  23. Mimi naomba niseme hivi hii inachangiwa na abiria. Ilikuwa mwezi wa tatu mwaka huu nilisafiri kutoka Dar kwenda Iringa tulipofika maeneo hayo hayo Dreva alikuwa akiendesha kizembe hivyo na overtake za kijinga! Mimi mwenyewe nilisimama nikaenda kumwambia dreva tafadhali punguza mwendo na uendeshe kwa uangalifu! Cha ajabu baadhi ya abiria wenzetu waliniona kituko wakidai wao wana haraka kwa sababu watachelewa kufika. Dereva alichofanya alipunguza mwendo akawa anaendesha mwendo wa ajabu yaani too slow uzuri kwa kuwa mimi nilikuwa nafika Iringa tu haikunisumbua sana nilipofika Ipogoro nikatelemka zangu wao wakaendelea lakini lililokuwa dhahiri wakati nashuka baadhi ya abiria walishukuru kwamba nimeshuka si ajabu hata Dreva.

    Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kiburi wanapewa na baadhi ya abiria wapuuzi kama hao Madreva. Mindset za watanzania nadhani iko tatizo katika kusimamia sheria sijui tumelogwa? Angalia hata miji yetu ilivyo michafu utaona mtu ananunua maji akimaliza anatupa chupa popote yaani wala haimpi shida kabisa yaani tuna tatizo kubwa! Hebu jaribu kumsemesha mtu kama huyo atakavyokutolea matusi ya nguoni? Ni mambo ya ajabu yaani mimi sielewi na ndiyo maana nchi hii kila kitu kinakwenda hovyo hovyo! We are not responsible, we are not serious! Use any language you would like but we have a very big problem MUNGU ATUSAIDIE JAMANI MIMI SIELEWI YAANI TUNATOKAJE HAPAAA....?

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 02, 2012

    Tanroads watanue njia hizi kwenye kona ili kuongeza uonekano wa mbele ya dereva, sumatra au polisi waiwezekani kuwa kila mahala kudhibiti uendeshaji hatarishi kama hivi. Zile sehemu zilizokua sugu kwa ajali za uso kwa uso hasa maeneo ya bwawani pale morogoro hii idea ya kutanua njia imeleta manufaa sana. Sio kwamba madereva hawajui sheria hapana wanajua sana ila kiukweli huwezi safiri na basi spidi kama ya hilo roli haiwezekani jamani tuseme ukweli

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 02, 2012

    Huyo wa mwisho scania marcopolo nyeupe ni dhahili anakwenda kwa nguvu ya BANGI tu he is just anticipating kwamba hakuna gari inayokuja mbele yake. Bangi tuu hapo

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 02, 2012

    Hapo Mwenye roli hakua fair angepunguza kidogo mwendo basi la kwanza jeupe linalomaliza kuovertake lingeweza kuwahi huo mstari ulioishia hapo kabla ya hizo double solid line ila hiyo Abood na wanyuma yake walishachelewa walitakiwa kusubiri hapo. Palikua na haja ya tanroad kutanua njia hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...