Pikipiki ikiwa imelala ubavuni baada ya kugongwa na hio gari maeneo ya Namanga Best Bite jijini Dar es salaam jioni hii
Mwendesha pikipiki hio (mwenye fulana ya njano) na abiria wake (mwenye nyekundu, aliyeketi) wakiwa wamepigwa butwaa baada ya kurushwa pembeni ya barabara baada ya kugongwa, wakiwa wameumia miguuni na kichwani. Bahati walivaa helmet. Sehemu hiyo ni hatari sana hasa ukizingatia kuna barabara ndogo inayoingia barabara kuu ya Bagamoyo yenye magari yaendayo kasi kutokea mataa ya Namanga. Haipiti wiki bila kutokea ajali sehemu hii...




WAENDESHA PIKIPIKI NAO HUWA HAWAKO MAKINI. WANATUKWARUZIA MGARI YETU KWA KUPENDA KUPENYA SEHEMU ISIYOTOSHA UPANA WA PIKIPIKI ZAO
ReplyDeletePOLENI. LAKINI MJIFUNZE UMAKINI
Wengi waendeshao pikipiki hawazijui sheria za barabarani, na wahajui haki yao barabarani, lakini na waendesha magari nao wajeuri, hawataki kumpisha mwendesha chombo kingine, iwe gari, pikipiki au baiskeli mbao nao wana hakui ya kutumia barabara, hata waenda na miguu wana haki ya kutumia barabara. Unapomuona mwenzio anahangaika kuingia au kajitokeza, dereva wa gari anajukumu la kumpisha...... Courtesy iko wapi, au give the person on your right the right iko wapi... tujifunze sheria sio tuuu kuendesha...
ReplyDelete