Mkuu wa Jeshi la Magereza mkoani Ruvuma,kamishina msaidizi wa magereza (ACP) Mohamed Litundu akimvalisha cheo ofisa wa jeshi hilo Asumin Abdala kutoka mkaguzi msaidizi hadi kuwa mkaguzi kamili,katika sherehe fupi iliyofanyika katika ofisi za jeshi hilo mjini Songea jana.
Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Ruvuma,Kamishina msaidizi wa magereza,Mohamed Litunu (kushoto) akimpongeza mkaguzi wa magerza Asumin Abdala baada ya kupandishwa cheo kipya kutoka mkaguzi msaidizi hadi mkaguzi kamili wa magereza.
Msaidizi wa Mkuu wa Gereza la Mahabusu Songea,Patric John (kushoto) akimpongeza mkewe mkaguzi Asumin Abdala baada kupandishwa cheo kutoka mkaguzi msaidizi hadi kuwa mkaguzi kamili.
Mkuu wa Magereza mkoani Ruvuma,ACP Mohamed Litunu akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa jeshi hilo pamoja na askari baada kumaliza zoezi la kuwa pandisha vyeo maafisa kadhaa wa jeshi hilo jana mjini songea.PICHA NA MUHIDIN AMRI.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...