Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, alikabidhi Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Italy, Mhe. Giorgio Napoletano, hapo tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais (Quirinale) iliyopo mjini Rome. 
Katika hafla hiyo fupi, iliyoanza saa 11 kamili za jioni kwa kwa mapokezi rasmi yaliyohusisha pia gwaride la heshima, Balozi Msekela pia alikuwa na mazungumzo mafupi na mweneyeji wake baaada ya hati zake kupokelewa, ambapo pia alifikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi wa Tanzania nchini Italy pia ndiye mwakilishi wetu katika nchi za Ugiriki, Uturuki, Slovenia, Croatia, Serbia, Malta, Bosnia na Herzegovina, na Albania. Katika uwanda wa mashirikiano mapana ya kimataifa, Balozi huyu pia anaiwakilisha Tanzania katika FAO, WFP na IFAD, ambayo yote ni mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye makao yake makuu mjini Rome.
Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, akikabidhi Hati za utambulisho kwa Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy, jana tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais ijulikanayo kama ‘Quirinale’.
 Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy, akimkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, katika kasri yake iliyopo kati kati ya mji wa Rome. Kasri hiyo inajulikana kama ‘Quirinale’. Pamoja na Mh. Napoletano, walikuwepo pia; Mkuu wa Itifaki katika kasri hiyo, na washauri wengine wa Rais wa Italy.
Rais wa Jamhuri ya Italy, Mh. Giorgio Napoletano, akipitia Hati za utambulisho wa Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela. Baadaye Mh. Rais alimkaribisha Balozi ofisini kwake kwa mazungumzo mafupi. Picha zote na Quirinale, Rome.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2012

    Kweli SMT inajua kubana matumizi yaani balozi wa Italy anawakilisha nchi tisa pamoja na mashirika matatu ya UN.

    Hivi kweli utendaji ni wa kikweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2012

    Mdau wa Kwanza hapo juu Wed Jun 20, 05:12:00 PM 2012

    Huo mwendo wa SERIKALI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa ufanya hivyo ndio mwendo wenye tija zaidi achilia mbali sisi angalia nchi tajiri kama Canada imejaribu sana kufanya hivi mfano Hii Ofisi iliyopo hapa Dar Es Salaam ni CIDA (Canadian International Development Agency) zaidi ni Ofisi ya Shirika la Maendeleo la Canada inayohusika zaidi na Miradi yao hapa nchini wakati Ubalozi wa Canada upo Nairobi Kenya kwa nchi za Kenya,Rwanda, Burundi,Uganda, Ethiopia,Eritrea,Sudan,Tanzania, Seycheles,Congo, Mauritius na Malawi. (nchi 12).

    Pia kwa Kiutawala unawekwa Ubalozi kwa Misingi ya tija mfano nchi ambazo hatuna maslahi Ofisi zinafungwa ili kubana matumizi kama huko Ulaya Mashariki hizo nchi kama Ugiriki,Slovenia,Romania na nyinginezo hakuna kitu ndio kwanza wamefilisika kifedha na Kiuchumi hakuna sababu ya sisi kuweka Ubalozi ni gharama za bure tu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2012

    Anon wa pili umenena vizuri sana.

    Kwanza sisi ni masikini kwahiyo inabidi tusave pale inapowezekana. Pili kuwa na mabalozi wengi haimanishi ufanisi na wala haina maana ndo tutapata mikopo/misaada mingi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2012

    Anony wa kwanza kubana matumizi ndio msing wa maendeleo. Mtoa maoni wa pili amesema vizuri sana. Hata Australia in ubalozi Kenya, Afrika kusini na Misri kwa nchi zoooote za Afrika. Australia ni nchi tajiri duniani lakini inafanya hivyo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2012

    Mh. Mpya ombi langu ni hili-VYETI VYA NDOA NA VYA KUZALIWA VYA ZANZIBAR MTUPIGIE MIHURI KUHAKIKISHA MAANA KILA CHETI CHA ZANZIBAR UKIPELEKA UBALOZINI TUNAAMBIWA NI FEKI LAKINI CHA TZ BARA KINAKUBALIKA MOJA KWA MOJA.KIPINDI CHA KARUME TULIKUA TUNAPETA.
    MWISHO JE WALE WAFILIPINO BADO WAPO UBALOZINI MAANA UNAONGEA NA CONSULAR WAKO BASI HADI UONGEE KIFILIPINO NDIO UKUBALIKE.THANKS

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2012

    Ok, tunapongeza mahusianao na Jamhuri ya Italy. Msekela, hebu chakarika hapo Italy na pia hapo FAO kwa ajili ya KILIMO KWANZA. Tunahitaji kuongeza thamani mazao yetu, tuuze mvinyo hadi huko Utaliano.

    Hiyo Kasri inaonesha kujaa historia iliyotukuka. Panapendeza kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...