Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Bi. Diane Corner (kulia), akisisitiza jambo kwenye kikao alichofanya na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (shoto) baada ya kufanya ziara kwenye Wizara. Anayeangaliana na balozi  ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen  Maselle. Lengo la ziara yake ilikuwa ni kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza hususan katika sekta  za nishati na madini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Mbona hawa mabalozi wanatembelea wizara ya madini sana, nini agenda yao ???

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2012

    wewe ulitaka waende wapi? Geza ulole?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2012

    hawataki kutupa visa zao ila madini yetu wanayataka

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2012

    Yaani ninyi mnauliza majibu???
    Uingereza hali ya uchumi iko kwenye tundu la choo, na Ulaya nzima.
    Wako hali mbaya sana, kwasasa wanatafuta kila kona kuchuma, kuiba nk, ili waokoe uchumi wao. Watajifanya marafiki kumbe wanawavizia wawakate vichwa.
    Exactly the same wakati ule wa ukoloni walipotuibia rasilimali zetu.
    Tanzania iwe makini sana na urafiki huu feki, tulinde mali zetu, tusilaghaiwe kama mababu zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...