Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kimeandaa Mkutano Mkubwa wa Hadhara kwa wananchi wote, Siku ya Jumamosi, tarehe 09/06/2012, Katika Viwanja vya Jangwani Kuanzia saa 8 mchana. 

Maudhui;  “Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa. Hivyo Chama Kitatumia Fursa hiyo Kuelezea Watanzania Juu ya Msimamo Wake Katika Mambo yafuatayo:

1.     Hatma ya maisha ya Watanzania

  • Ajira, Miundo mbinu ya Barabara, Reli, Bandari Na Anga.
  • Bei za bidhaa mbalimbali.
  • Umeme
  • Rasilimali za taifa
2.     Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.

3.     Vurugu za Zanzibar.

Katika Mkutano huo, Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watakuwepo na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo yaliyoainishwa kama msimamo wa Chama Cha Mapinduzi.

Chama Cha Mapinduzi, kinawaalika wanachama wake wote, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuhudhuria katika mkutano huo mkubwa. Mkutano utafanyika kwa amani na utulivu na wote mnakaribishwa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na:
JUMA SIMBA
KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Swali langu kwa kuwa mimi nami ni mwanachama mkereketwa lakini mpenda nchi yangu: Je hao viongozi wa serikali watakuja na magari ya serikali wakati ni mkutano wetu wa chama na kila kukicha watu wanalalamika kuhusu matumizi mabovu ya mali za uma? Kwa ushauri wangu hili jambo liwekwe mbele ya meza na kujadili kabla ya siku ya mkutano ambayo ni kesho kwa kuwa tutawapa nafasi wapizani waweze kuongea. TAHADHARI KABLA YA HATARI!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Sawa ni Kikao cha Siasa cha Kichama lakini ktk utekelezaji wa Dondoo au Hadudi hizo muhimu,

    1.Hatma ya maisha ya Watanzania
    2.mchakato wa Katiba
    3.Vurugu Znz

    Inabidi muwe kivitendo zaidi kuliko propaganda!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Ahsante Katibu Mwenezi ktk hizo (3) hapo chini

    1.Hatima ya Watanzania
    2.Katiba
    3.Virugu Unguja

    Unesahau No.(4) Ambayo ni:

    4.Kuwawajibisha wezi na Mafisadi hasa wale ambao ni wana CCM wanaokibomoa Chama badala ya kukijenga!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    Nitafuatilia kwa Tv kama mtarusha na humko jamani, mi mvivu naona sitakuwepo, ila pa1 sana Chama Mama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...