Bendi ya Muziki wa dansi ya FM maarufu kama wazee WANGWASUMA pamoja na msanii wa vichekesho MPOKI watatoa burudani ya anina yake katika shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni City 2012' litakalofanyika Juni 15 mwaka huu katika ukumbi wa Navy Beach ulioko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu amesema kuwa bendi ya FM Academia inafahamika kwa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini.
Kuhusiana na msanii MPOKI, SOMOE amesema kuwa mchekeshaji huyo ambaye pia ni mkazi wa KIGAMBONI amekuwa ni kati ya waburudishaji katika sanaa ya uchekeshaji na kupendwa na watu wa rika zote hivyo mashabiki wa urembo wataweza kupata burudani ya uhakika.
Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L, alisema kuwa Jumla ya warembo 15 wanaendelea kujifua katika kambi ya mazoezi chini ya mwalimu wao miss TEMEKE HAWA ISMAIL ambaye anashirikiana na mshiriki wa miss TANZANIA mwaka jana BLESSING NGOWI.
Amewataja warembo hao kuwa ni pamoja na CAROLYNE DANDU,FATINA FRANSIS,EDDA SLYVESTER,AISHA MUSSA,ROSEMARY PETER,DOREEN KWEKA,CAROLINE PETER,AGNES GOODLUCK,SOPHIA MARTINE,ROSEMARY DEOGRATIUS,BEATRICE BONIFACE,JULIETH PHILIP na KHADIJA KOMBO.
"Kigamboni ni zaidi ya kitongoji, tunaamini shindano letu litakuwa na mvuto na hadhi ya kipekee kama eneo lake lilivyo," aliongeza.
Alisema kuwa warembo watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika mashindano ya kanda ambayo yatafanyika baadaye mwaka huu.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF,Hope country Motel,Norbro’s Collections,Screen masters,Global Publishers.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...