Mtoto Rukia akiwa kitanfani pake.Ikumbukwe kwa hali ya mtoto huyu kuwa na majeraha makubwa huwa anahamishwa na kitanda chake mpaka sehemu husika.
![]() |
ST.WALBURG'S HOSPITAL NYANGAO mkoani Lindi ndipo mtoto RUKIA amelazwa. Chini ni siku alipowasili hospitali hapo kwa misaada ya wasamaria wema toka ndani na nje ya nchi |
NA ABDULAZIZ VIDEO, LINDI
KWA NIABA YA FAMILIA YA MTOTO RUKIA TUNAWASHUKURU SANA WOTE MLIOGUSWA
NA KUMSADIA RUKIA KUMUDU MATIBABU.
HUWEZI ELEWA LAKINI PIA NI FARAJA SANA MIMI NA RAFIKI YANGU VICTOR KWA JINSI AMBAVYO MMEPOKEA MATATIZO YETU YA JAMII...ZAIDI YA YOTE MUNGU ALIPANGA NA NINA IMANI MUNGU YUPO PAMOJA SANA NA MTOTO RUKIA....TULIWAOMBA KUPITIA FB NA MITANDAO MINGINE KUMSAIDIA SHABAN HASSAN KALEMBO BAADA YA KUKOSA MASOMO YA KIDATO CHA NNE KWA KUKOSA TSHS 45 ELFU...TULIPOWAOMBA MLIJALI NA KURIDHIA KUMCHANGIA KWA IMANI YENU KWETU MLIMCHANGIA SANANA KWA HARAKA LAKINI MSAADA WENU KUMSAIDIA KIJANA HUYO.
KUMBE MUNGU ALITOA NURU NA UWEZO KUBAINI MATESO YA MTOTO RUKIA AMBAE ALIUNGUA MOTO BAADA YA KUANGUKIA SUFURIA YA MAJI YA MOTO ILIYOKUWA JIKONI.....RUKIA NA SHABAN IWANAISHI KATIKA NYUMBA MOJA...MSAADA WENU ULIFANYA AGUNDULIKE RUKIA ALIEKAA ZAIDI YA WIKI TATU AKITIBIWA KWA MITI SHAMBA KWA KILE KILICHOELEZWA UKOSEFU WA PESA KUFIKA HOSPITAL....VICTOR ALIGUSWA NA HILO NA KUAMUA KUSAIDIANA NAMI TENA KUWAOMBA KUMSAIDIA MTOTO HUYO...MLITUAMINI NA MLIGUSWA RUKIA AKAFIKISHWA NYANGAO HOSPITAL....HAKIKA NAWAHAKIKISHIA MTOTO HUYO ANAPATA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VEMA KWA UWEZO WA MUNGU
ATAPONA....MICHANGO YENU NCHINI NA NJE YA NCHI IMEFIKIA TSH 1.5 MILION.....NA AHADI NYINGI...
NAWAOMBEA MUNGU MUONGEZE PALE
MLIPOTOA...AMEEN
Pole sana Mtoto mzuri Rukia. Kwa kweli TUMSHUKURU MUNGU, inatilisha imani. INSHA ALLAH, Mwenyeez Mungu atakuafu na kukujaaliya upone haraka na urejee katika hali yako ya uzima na siha iliyo njema - AMEEN. Pole sana.
ReplyDelete