Hali ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.Ulimboka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Kitengo cha mMifupa (MOI) aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru Kama aonekanavyo pichani juu. Taarifa zinasema kiasi cha Dola 40,000 (kama 64m/-)  zinahitajika kwa ajili ya usafiri na matibu zaidi  ya Dkt Ulimboka nchini India.  

Jana ulifanyika Mkutano wa Madaktari Bingwa wa MNH, Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ocean Road (ORCI) na kuazimia kukusanya Dola za Marekani 40,000 (Sh64,000,000) ili Dkt. Ulimboka asafirishwe kwenda India kwa matibabu zaidi.

Taarifa za maazimio hayo zilitangazwa kwa waandishi wa habari na Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitega, kuwa afya ya Dk Ulimboka haikuwa nzuri hivyo zikipatikana fedha hizo angepelekwa nje ya nchi.

Dk Chitega aliwataka wanataaluma hao na wananchi kwa ujumla kuchangia safari hiyo ili kuokoa maisha ya daktari huyo, huku akitaja namba za mawakala wa simu za Vodacom na Tigo, ambazo zitatumika kukusanya michango hiyo. 
Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii

==================
Dear all,

Thank you very much for your candid support in this.

I would like to bring to your attention that we had a meeting this afternoon between myself and a team of specialist to discuss modalities of collecting contributions.

In order to efficiently coordinate contributions it was agreed to use m-pesa agent number 31915 belonging to Christine Hobokela and and tigo pesa agent number 05416 belonging to Hedaya Stephen Mwaitenda.

For those who want to send foreign currency (USD) please send to Dr. Hobokela Stephen, Stanbic Bank Tanzania Limited Account number: 024003849360, SWIFT CODE: SBICTZTX

The reason I'm sending this is because I have been asked several times to clarify on this and after consuling with MAT president, he advised me to provide this clarification.

Below are some steps on how to send money to m-pesa and tigo pesa:
 


M-pesa

1. piga *150# OK
2.Chagua 2, toa pesa.
3.Ingiza namba ya wakala ambayo ni 31915
3.Weka kiasi cha pesa unachotaka kuchangia eg 50000
4.Weka nambari ya siri - namba yako ya siri
5. Bonyeza 1 kuthibitisha muamala

Utapata ujumbe kuwa mefanikiwa kutoa pesa kwa Christin Hobokela 


Tigo pesa


1. piga *150*01# OK
2.Chagua 3, kutoa pesa.
3.Ingiza namba ya wakala ambayo ni 05416
3.Weka kiasi cha pesa unachotaka kuchangia eg 50000
4.Weka nambari ya siri - namba yako ya siri
5. Bonyeza 1 kuthibitisha muamala

Utapata ujumbe kuwa umefanikiwa kutoa pesa kwa Hedaya Mwaitenda 
----------------
Once again we thank you very much for your support.

Hobokela Stephen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2012

    Namtakia matibabu mema ili aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida!

    God bless him!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2012

    Hakuna kwenda India wala Mtwara na yeye akae hapo hapo muhimbili ili aonje ile adha ambayo wagonjwa wanaipata kwa migomo anayoiitisha kila siku ya madaktari, watu wanakufa eti kisa wao wanataka marupurupu yaongezwe...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2012

    Wewe wa saa 10:55 Sat.30 June Mungu akusamehe maana hujui ulisemalo.
    Naomba kujua kwa ambao nje ya nchi tunaweza kutuma hela kwa njia gani? make hizo mpesa na tigo pesa sitaweza ila ningepata jina la muhusika ili nitume kwa western union ama money gram. Mungu akujalie afya njema Dr. Ulimboka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2012

    Wewe mdau wa pili, unafikiri mfanyakazi anatakiwa akubali kufanya kazi, hata kama malipo anayopata hayatoshelezi mahitaji ya kwake na familia kwa ujumla? Kazi ya udaktari ni ngumu sana. Wanaambukizwa magonjwa mengi na wagonjwa. Kwa hiyo inabidi wapate pesa ya maana, ili wapate lishe nzuri ya kukabiliana na matatizo kama hayo.

    Ushauri kwa madaktari: Mpango wa kumsafirisha kwenda India ni mzuri. Lakini je akiwa India mtaendelea kumwekea ulinzi kama mnavyofanya hapa Tz? Maana mkizubaa wabaya wenu watammaliza, kwani wanajua kuendelea kuishi kwake ni mwiba kwa wabaya wake, kwani wanajua kuwa aliweza kukariri sura zao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2012

    Kinyozi wa Bongo hataki kunyolewa hapa kwetu?Hii inatia unyonge kuwa jamaa hana imani na wataalam wenzake wa hapa kwetu.What message is he sending to the rest of us.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2012

    kwa maantiki hiyo huo mgomo ni wa kuongeza huduma ama marupurupu.. yeye mwenyewe kiongozi wa mgomo anatakiwa akatibiwe india... je inaleta maana na mgomo wao...???? kwanini wasigome kuwa huduma ni duni watie shinikizo la kudumisha huduma... kwa sisi tusio kua na uwezo wa kupelekwa india ndio mnatufikishia ujumbe gani?????

    fubulous!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2012

    Kumbe mnatuua makusudi mkijua nyie mtatibiwa India? Malipo ni hapa hapa duniani. Hayo maumivu wanayopata wazazi wako na sie tuliyapata kwa ndugu zetu wakati ulipohamasisha wenzio wagome na kuwaacha jamaa zetu wakifa kwa shida mawadini, lakini mungu hakujaalie usife ila ujifunze.Amina.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2012

    Wabongo mnageuka kuwa wanyama pori. Mnashangilia binadamu kupigwa japo kuwa ana haki ya kugoma kazi ili kuongezewa mahitaji yao.


    Shame on you. Once upon a time your country was the model of peace and stability but it seems those days are long gone. Whats left is angry people who quickly resort to violent and aggression to settle scores.

    Chadema influance seems to have taken over your country

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2012

    Hao mabingwa tena wengine maprofesa wanachanga kumpeleka India, Mantiki ya kuongezewa marupurupu na mishahara hapo mie siioni kabisa!!!!! ikifikia hata daktari mwenzao hawawezi kumtibu hao MABINGWA gani. Nasikia hata wakipelekwa India wanarudi na sifuri. Leo haohao wangemtangazia kifo mtanzania wa kawaida bila ya kuweko mgomo. Ndio zao hao labda utoe chochote. Nasema hivyo kwa sababu yamenikuta, madaktari bila ya chochote hakufanyiii operation ambao kwa kuwa anajua kwamba ili uvuke na maisha wewe au jamaa yako utatoa tu na kisha utanyamaza. Nesi kama hujampa chochote mgonjwa wako akiwa wodini atawanyanyasa mpaka mkome. Hiyo haipo Muhimbili au hospitali za bure bali hata hospitali za kulipia. Bila la lugha nzuri (ya kifedha) huko kwenye pesa ndio kabisa na huwa wanalipwa vizuri. Tatizo sio pesa ni rushwa imekithiri kote. Mabingwa ndio wanaongoza katika hili. Tuseme tusiseme.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 30, 2012

    Kwanza pole sana kwa maumivu,hapa mimi siungi mkono mgomo wa madaktari wala hao waliokufanyia kitendo hicho ila udaktari ni wito sio kuangalia maslahi zaidi kama ulitaka maslahi basi mlitakiwa kuingia kwenye sekta ya baishara,ili mpate faida ya kupindukia.Uwalimu,unesi,udaktari ni wito toka moyoni na maslahi yanakuja polr pole sio kwa mgomo ila kwa maelewano na kwa kuokoa maisha ya wananchi.Kwa waliomfanyia kitendo hicho wana sababu zao labda kuna waliofiwa ndugu wengi kwa mpigo na wakaona sura wanaijua ndio kisa cha kulipiza kisasa,ni mtizamo wangu ila mgomo kwa madaktari sio jibu la kutatua matatizo yenu,polisi wakigoma itakuwaje?walimu je?nchi itasonga kama kila sekta wanagoma?Madaktari sasa mtoe kidogo mlichonacho ili mkuu wenu akatibiwe India,then mdai malipo ya ziada kisa mmechanga.


    Ni yule yule
    Duke of Kimbiji

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 30, 2012

    Madaktari wa Tz mngekuwa kweli mnafanya kazi kwa haki, uadilifu, weledi tungewaunga mkono sana. Lakini kazi mnafanya kwa ufisadi unaotisha, wala rushwa wakubwa, wazembe&walevi (mkampasua mtu kichwa badala ya mguu),etc...mnataka mlipwe hela zaidi kwa kipi hasa mnachozalisha?kwa kazi gani hasa yenye uadilifu mnayoifanya?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 30, 2012

    wanaosema sijui madokta wanapigania huduma bora kwa wa-tz nataka kuwauliza je ni sekta gani tz isiyo na mapungufu?

    elimu - watoto wanakaa chini,hakuna maabara&maktaba&walimu&madarasa ya kutosha,walimu wanalipwa vibaya sana.

    usalama - hakuna vituo vya kutosha vya polisi,polisi wachache,magari ya patrol hakuna,wanajeshi wanalipwa vibaya sana.

    magereza - magereza ni mabovu tena sana,wafungwa kulundikana,kesi za kubambikiwa,kesi kuchukua miaka kusikilizwa.

    Michuzi nikiendelea kuorodhesha nitajaza gazeti hapa. Sasa pata picha kila sekta ikaamua kugoma kushinikiza kuboreshwa kwa huduma je nchi hii si itakuwa kama SOMALIA? Acheni unafiki jamani kama mnataka salary nzuri si mwende nje (kama kweli mna-ujuzi&kufanya kazi kwa makini) mtuachie tanzania yetu yenye amani tele

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 30, 2012

    Ninyi mnaoshabikia madaktari ni wala rushwa mlitegemea wale nini kama wanachodai hawapewi? hivi mbona mnakuwa na mawazo mgando kiasi cha kushindwa kuchambua mambo kwa kina? wengi wenu hapo hata ukiona mtu kapasuka kichwa mnakimbia lakini daktari ndo anashinda anashika hivo vidonda na maiti. Wabunge wanalala tu huko bungeni mishahara na marupurupu kibao. Mimi ni mwalimu lakini siwezi kusema eti nafasi yangu ni sawa na daktari NEVER tukubali ukweli kuna fani zingine ni za hatari na ngumu sana zinahitaji motivation la sivo watu watakufa wengi tu na wameshakufa kama serikali haitakubali kubadilika. Unafikiri ndugu zenu kufa ni kwa ajili ya madaktari tu? KAA CHINI UTAFAKARI NI VITU GANI VYAWEZA CHANGIA MTU KUFA KISHA UTAPATA JIBU

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 30, 2012

    It is better to keep quite if you don't know what you are talking about and it's source!

    Ni bora ukae kimya kama ujui unachosema na chanzo chake!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 30, 2012

    Sababu moja wapo ya mgumo huu ni kupatiwa vitendea kazi. Kama mngeweza kufuatilia huu mgomo kwa karibu madai Yao ni ya msingi sana. Leo imebidi apelekwe regency kusudi akafanyiwe dialysis. Imagine hospital ya muhimbili Nzima Hamna huduma ya dialysis. Na ndio Maana wanaomba akatibiwe India, Lkn serikali ingekuwa imeweka kipaumbele Madai Yao Tangia mwanzo. Hamna mtu angeenda kutibiwa India kwa sababu kila kitu kingekuwepo hapa hapa nchini. Mimi Naona jambo la msingi kwa sisi wananchi ni kuishinikiza serikali kuwasikiliza madaktari na kuwapa madai Yao ya msingi. Na hayo madai yakitekelezwa it means good for both of us walalahoi cause vitendea kazi vitakuwepo na wao watakuwa hawana sababu ya kutokutoa huduma bora kwa wananchi kama waauguzi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 30, 2012

    Pole sana Dr. Lakini kitu nimegundua madaktari wa Bongo hasa wa kiume hawana utu hawa kizazi kipya. Wale wa zamani Mungu awatie nguvu. Madaktari wa kike Mungu awatie nguvu.

    Tunajua pesa mtapata kwa vile mnanjia nyingi za kupata pesa lakini mnachofanya sio utu... Leo Ulimboka kesho mwingine atadai hizo hizo 64,000,000 na kumbuka waliofanya kipigo hawajulikani azma yao yaweza kuwa vita vinaendelea. Je kwenda India au Afrika Kusini ndio dawa... TAFAKARINI VIJANA MNAKOTUPELEKA SIKO... MGOMO WENU NI SIASA NA UKABILA NDIO UNAONEKANA

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 30, 2012

    WEWE UNAWAFUNDISHA WAFANYAKAZI KUGOMA WAKATI WAGONJWA WANAKUFA HUNA HURUMA WEWE,KAA HUKO WODINI UJUE WENZIO NI VIPI TUNATESEKA.HAWA WALIOKUKAMATA NINGEWAJUA NINGEWAPA POSHO KUBWA.DOCTOR WAPENDE WANTANZANIA WENZAKO KAMA UNAVYOJIPENDA WEWE,TAMAA YA PESA ITAKUPELEKA PABAYA SANA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 30, 2012

    UNAJUA WATU MNASHINDWA KUFKIRI HUYU JAMAA KWA SABABU YUKO KWENYE TV NA BLOG NDIO MAANA MNAMUONEA HURUM KIASI LAKINI MNGEWEZA KUONA WALE WALIOKUFA AMBAO HAWAJWEKWA HUMU KWENYE BLOG NA SIO TU WALIUAWA NA MADACTARI PIA WALICHUKUA NA HELA ZAO WAKAKATAA KUWARUDISHI YAANI HAWA NDIO WANYAMA ZAIDI UKIKOMPEA NA HAO WALIO MPIGA HUYO BWANA, HATUPENDI HAYA MATUKIO ILA MIMI SIMCHANGII MAANA HANATOFAUTI NA NDUGU ZETU WENGINE WALIOKUFA KWA AJIRI YA UCHOCHEZI WAKE HELA IMEONGEZWA KIDOGO LAKINI HAITOSHEKI HII MIDUDU SIJUI VIPI, TENA UKO LUCK HATA UNAPATA MATIBABU MAANA NDUGU ZETU HAWAKUPATA HATA HAYO MAPOKEZI NA MADAKTARI. ALL IN ALL I DONT FEEL SORRY AT ALL.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 30, 2012

    Mengi yaliyoandikwa yanaweza kuwa kweli lakini ukichunguza mzizi wa matatizo ni mazingira mabovu ya kazi pamoja na malipo duni....hata dokta kupelekwa india ni kukosekana kwa mazingira na vifaa bora hapa nchini.... Serikali amkeni kwenye hili na muwe wasikivu. Kila kazi ni wito hata ubunge nao na uongozi wa aina nyingine pia, sasa inakuwaje wito nyingine zina maslahi na wito nyingine ni kandamizi. Hii definition ya wito tumeitoa kwenye maandiko yapi kwanza!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 01, 2012

    madakitari rudini makazi mwenzenu anaenda tibiwa ulaya

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 01, 2012

    Dr Ulimboka - The Killer umetuulia nduguzetu umetuachia yatima kibao. Tuchange kuwasaidia wale yatima na wajane aliotuachia kwa migomo yake katili. Yeye Bwana Yesu amsaidie aponee, tupo naye kwenye maombi.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2012

    Hapana Hapa Big NO!
    Ana mshahara mkubwa kuliko sisi walimu wake, walinzi wake tunaofuatilia kipigo chake nk. Kama anaona analipwa kidogo aende huko wanakolipa vizuri yuko huru asishawishi wengine nao wagome. Milioni 64 zinunulie majokofu ya kuhifazia miili ya wale wanokufa kwa ukatili wake.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 01, 2012

    Pona salama , mna haki ya kugoma ili huduma za afya ziboreshwe. Hospitali zetu zingekua bora na vifaa vyote muhimu hata wewe ungetibiwa hapa ila hapa. Tuna maprofesa na madaktari bingwa lakini dawa hakuna vifaa hakuna. Mliobaki msiache mateso na damu ya mkombozi wenu ipotee bure. Kwa mateso ya Ulimboka sekta ya afya ikombolewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...