Unajua kama mtu huna historia na swala la waandishi wa Bunge ni bora ukanyamaza, labda manyerere amesahahu swala la ukumbi wa waaandishi wa habari Bungeni lilivyokuwa. Nimekua nikija kuandika habari Bungeni na najua historia ya Ukumbi wa Waandishi wa Habari, Jengo hilo la kisasa limejengwa kwa kuzingatia mahitaji ya kila mtu, waandishi wa habari ukumbi wao upo juu na una mpaka vimeza vya kisasa vya kuwawezesha kuandika vizuri, lakini cha kushangaza wakati wa mhe.
Mhe. Sitta akiwa Spika, mmoja wetu akaleta hoja na kutu Convince waandishi wenzie ili tuamishiwe gallery ya maafisa wa serikali (sehemu ambayo ni ndogo kuliko tulipotengewa awali) kwa madai eti tuwe karibu sana na vioo kupenyeza vimemo kwa wabunge.... tukashauriwa udogo wa eneo wenzetu wakadai panatosha.. enzi hizo tulikuwa tukifika bungeni waandishi takribani 15 hadi 30.
Sasa mkutano huu wa Bunge tupo waandishi wa Habari zaidi ya 90 kutoka, kila aina ya vyombo vya habari na blogs, na kila mmoja wetu anang'ang'ana kukaa pale chini tulipojazana eti kuchati huku gallery ya juu ambayo ni hasa iliyo designiwa kuwa press kukiwa empty!!! Ndio maana kelele haziishi na kila saa watu wanapiga story badala ya kufanya kazi. leo hii madai kuwa tunanyanyaswa sio kweli tuliyataka wenyewe na kwa kuwa kila mtu anania yake tofauti hata uandishi wetu sasa umekuwa full magumashi tu ..... Jamani manyerere ungeuliza wakongwe kabla hajapiga picha. Penye ukweli tusifie jamani jingo lilijengwa kwa kukidhi mahitaji, sehemu yetu ipo tuliikataa wenyewe…. Tusiwe domo kayaaaa jama.
Kwa kuwa nipo hapa, nakuletea fotooz za ukumbi wetu na jinsi palivyo empty huku watu wamejazana hapo chini.
Mwandishi Mzalendo, Bungeni



wewe ni mnafiki, manyerere kaweka jina lake mbona wewe unatumia kivuli cha mwandishi mzalendo?
ReplyDeletena ukongwe upi unauzungumzia wewe wakati manyerere amekuwa katika fani kwa zaidi ya miaka 15?
AISEE NAMSHUKURU SANA HUYU MWANAHABARI MZALENDO KWA KUTUFUMBUA MACHO...MAANA NAJIULIZA HABARI ZA KIZUSHI AINA HII ZIKO NGAPI NA ZINA ATHILI VIPI UELEWA NA MTAZAMO WETU KWENYE MAMBO MENGI. KWAKWELI WAANDISHI KUWENI MAKINI JAMANI.
ReplyDeleteHuyo alioleta habari za uongo blogini Mungu amuangaze. Yote hayo ni kutaka kuipaka matope serikali ya Kikweti eti dhaifu. Haya oneni wenyewe mnaazirika. Mnataka akupigeni vigongo na maji ya kuwasha ndio mtajua Kikwete ni commando bahati hamkuzaliwa mkamkuta Nyerere yupo hata hiyo sehemu ya waandishi msingepewa na mgelitoa domo lenu ndio mngelifukuzwa kabisa, mnaleta fujo. Nasikia mnagombea nafasi kama watoto wa chekechea huko kumbe nafasi ipo ya wasaa. Enhe huko mnapata posho??? maana waandishi wa habari kwa posho mhhh hamjambo. Michuzi ukiibania utakuwa umeninyima haki ya kutoa maoni yangu kwa wenzako. Nasikia hata habari mnadesa as a result kila gazeti linaandika habari hiyo ila sentensi ya mwanzo inawekwa mwisho na ya mwisho inakua mwanza, na sio wote wanaoweza sasa kufupisha, wenzao wengine wajanja wanaadika uongo halafu wakipasia kwa wenzao ambao hawana akili (uninteligent) wana-paste hivyo hivyo. Iko siku mtaipeleka hii nchi vitani. Picha ya vugugu Morogoro mnasema ya Zanzibar!!!!!! that is serious.
ReplyDeleteWaandishi tuwe japo na shukrani. Mabunge mengine hawadumiwi kama tunavyofanyiwa sisi japo kuna mapungufu ya hapa na pale. Kaka manyerere huu si uungwana.
ReplyDeleteJamani pengine manyerere ni mlemavu. Mimi sinjui naombeni mnijuze. Ndyo maana hawezi kupanda ngazi Maana Bunge ukifika na akawakuta akina Owen, Zulu na Minja shughuli zetu hupata unafuu mkubwa
ReplyDeleteKutoka kwa Raia
ReplyDeleteNdg Waandishi wa Habari wa Tanzania, mimi ni msomaji wenu mvivu. Leo nimejaaliwa juhudi kidogo kusoma malumbano yenu hapa pasipo hoja, mkionesha tabia isiyo na ubora unaostahili waungwana. Mmeonekana kuwa wachache wa shukrani.
Uwezo wa wengi wenu wa kuandika ni wa chini, hafifu, duni bin dhoofu kabisa. Uwezo wa wengi wenu katika lugha ya Kiswahili ni wa kutia hasira, huku istilahi ikiwa inawapiga kanzu na wala hamna mtiririko wenye mantiki kiasi cha kuelewesha wasomaji wenu kwa urahisi.
Mmejisema wenyewe kwamba baadhi yenu mmejijengea tabia ya kudai vibahasha, kiasi cha kukubuhu kama Mafisadi nambari wahedi. Ni aibu, aibu, aibu.Duh, tupeane pole wasomaji wenu.
Mmoja wenu kasema sahihi kwamba, siku moja mtaliingiza Taifa hili vitani. Ninaamini mawili tayari mmefanikiwa kuyatekeleza - lile la kupoteza imani ya wasomaji wengi, nikiwamo miye pia, na la kuharibu lugha adhimu ya Kiswahili.