Shaban Maranda na binamu yake Farijala Husein kesho mahakama ya hakimu mkazi kisutu inatarajia kuwasomea hukumu nyingine ya wizi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) kesi inayowakabili katika mahakama hiyo.
Hiyo ni hukumu ya pili kwao baada ya ile ya kwanza waliyosomewa Mwezi Mei mwaka jana na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano ambacho wanatumikia hadi sasa.
Kesi hii ni ya pili katika kesi za EPA kufikia hukumu kati ya kadhaa zilizofunguliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuiba Sh2.2 bilioni, katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa), iliyoko katika Benki Kuu ya Tanzania.
Hakimu Catherine Revocate aliiahirisha Mei 23 mwaka huu alisema kesi ilifikishwa mahakamani kwa lengo la kuwasomea washtakiwa hukumu lakini kwa bahati mbaya, mahakimu wawili hawakufika kazini kwa kuwa wanaumwa.
Aliwataja mahakimu hao kuwa ni kiongozi wa jopo, Jaji Fatma Masengi na Projestus Kahyoza. Alisema angeweza kuipanga kesi hiyo wiki ijayo lakini mmoja wa mahakimu hao atakuwa hajiwezi.
Alisema kwa msingi huo, anaahirisha hukumu hiyo hadi Juni 26, mwaka huu.
Maranda na Farijala, wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh1.8 bilioni za Epa.
Hatua hiyo iikuja baada ya Maranda na Farijala kumaliza kujitetea na wakili wao Majura Magafu kufunga ushahidi. Maranda akiongozwa na Magafu katika utetezi wake, aliiomba mahakama itupilie mbali ushahidi wote uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwa madai kuwa yeye hakuwahi kuiba wala kughushi.


Hivi bado mabo ya EPA yanaendelea; mpaka nilishaga sahau
ReplyDelete