Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa kuwa kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.

Jaji wamahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifuarahia Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward Rutakangwa (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya Rufani Mussa Kipenka na Jaji Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).
Mh. Rufani Mussa Kipenka akipongezwa na baadhi ya ndugu waliohudhuria hafla fupi ya kuapishwa kwake kuwa jaji wa mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es salaam.
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwaanatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria,kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    hebu cheki hii picha vizuri na niambiye inakupa twashira gani?
    wadanganyika waislamu wenzangu jamani msidanganyike tena,piganieni haki zenu jamanii na kama nihoja kusoma basi hakuna katika dini yeyote iliyo sisitiza kusoma kama yetu basi fanyenyi hima hima msome jamani wasitujie juu na hoja ya kisomo chao na sisi kukosa nafasi hizo.Please wadanganyika waislamu wenzangu please hima hima kisomo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...