| Kiongozi wa Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiislamu (JUMIKI), Sheikh Farid Ahmed |
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiislamu (JUMIKI) imepinga uvumi uliosambazwa nchini kuwa leo kutakuwa na maandamano ya Jumuiya hiyo na kudai kuwa propaganda hizo zinaendeshwa na baadhi ya watendaji katika jeshi la polisi na usalama wa taifa ambao hawaitakii mema Jumuiya yao.
Hayo yamesemwa na Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Ahmed wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo Zanzíbar kuhusiana na tuhuma ambazo wamezitoa kwa Jeshi la Polisi dhidi ya Jumuiya yao.
Amedai kuwa Jumuiya haijapanga maandamano kwani ni taasisi inayofanya kazi zake kisheria nakwamba hata ikitokezea kufanya maandamano basi watafuata taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulitaarifu rasmi Jeshi la Polisi.
Aidha amedai kuwa kuna mkakati wa muda mrefu wa kutaka kuwabatiza viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kesi za ugaidi hususan Amir Mkuu wa jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed ili kuzima vuguvugu la kudai Zanzibar huru.
Shekh Faridi amedai kuwa inasemekana kuna mahusiano makubwa baina ya watendaji ndani ya Jeshi la polisi pamoja na baadhi ya wageni wanaosadikiwa kuwa ni raia wa Marekani juu ya kuutekeleza mkakati huo baada ya kuwa tayari umeshakamilika.
Amedai kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za kirai ambao umekuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kuwanyima haki ya kufanya mihadhara yao ndani ya Misikiti ambapo Juni 17 mwaka huu wananchi mbalimbali walijeruhiwa kwa mabomu katika vijiji vya Donge,Mkwajuni na Mahonda.
Ameliomba Jeshi la Polisi kufanya kazi zake za kulinda usalama wa wananchi na mali zao na kuacha kufanya kinyume chake kwani huko ni kuchochea chuki kati ya Jeshi hilo na raia.
Amesisitiza haja ya wazanzibari kuungana na kuachana na Itikadi zao za kivyama katika kudai hadhi ya Rais na mamlaka ya Nchi ya Zanzibar ndani na nje ya Zanzibar pale tume ya mabadiliko ya Katiba itakapoanza kazi zake.
Kwa upande wake Naibu Naibu Amir Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiisilam Sheikh, Azan Khalid Hamdan amewaomba wanahabari nao kuwa makini katika taaluma yao kwa kufanya usawa wa taarifa ambazo wamekuwa wakizitoa.
Hivi karibuni Jumuiya hiyo ilitangaza rasmi kushiriki kikamilifu katika zoezi zima la kutoa maoni yao katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kubadili msimamo wao wa awali wa kuisusia Tume hiyo.


Nawaunga mkono kwa ufafanuzi huo mzuri...hata sisi wananchi tunajua kuna hujuma huwa zinafanywa na police na baadhi ya wanausalama kuwabambikizia kesi..ama utaitwa gaidi au hata wanaweza kufanya tukio wao hata la ulipuaji na kuwabambikizia watu wengine kwa nia ya kuzima hoja yao ya msingi. Hata kule Iraqi wamarekani na wahisani wao wanafanya hivyo...wanatega bom kwenye msikiti wa shia halafu wanawachonganisha na suni kuwa ndio wamelipua kupitia vyombo vya habari wanavyovimiliki wao wenyewe wamagharibi.
ReplyDeleteMadai ya Zanzibar huru ni lazima. Hizo njama za kuwahusisha viongozi wa Uamsho na ugaidi kweli zipo, tena siku nyingi. Lengo ni kuzima harakati za Zanzibar za kujikomboa na hatimaye kuleta mustakabali mwema katika maisha halisi ya Kizanzibari kimila, kiutamaduni, kisilka, kidesturi na kubwa zaidi kidini. Akina David Scott wanatafuta kila mbinu chafu ili kufanikisha mipango yao. Kwa uwezo wa Mungu Inshaallah hawatofanikiwa.
ReplyDeletewala hakuna haja ya mjadala, polisi kama wote kabisa, wasilete vurugu. na kwa ujumla wanaoongea wote kuunga mkono uamsho ni 'vilaza" wa kutupwa... kila siku naomba CV za viongozi wa uamsho lakini sizipati.
ReplyDelete