Ankel, Mzee wa libeneke, heshima yako. Tafadhali kama kutakuwa na nafasi katika blog yetu ya jamii nami nichangie mawazo yangu kuhusu Katiba mpya na Muungano wetu.
Najiunga na Mhe. Zitto na watanzania wengine kujadili jinsi ningetaka Nchi yetu Tanzania kuongozwa kikatiba. Hoja yangu kuhusu katiba na muungano ni kwamba; Tanzania ina tabia zote za nchi zilizoendelea duniani. Isipokuwa hatutaki kuwa kama nchi hizo. Unajua kwa nini?
Mfumo wa lugha na mpangilio mzima wa kuvumiliana ni kitu kizuri sana tulichoweza kukijenga kwa muda mrefu. Hivi sasa tunahitaji vitu kadhaa tu kusudi tuachane na hali ya umasikini tulionao kwa muda mrefu.
Teknologia yetu wenyewe ( Hisabati na sayansi), elimu kwa vitendo, kuboresha huduma za afya, kuanza kujenga miundombinu ya kisasa hii ni pamoja na kujenga mabarabara, umeme, kilimo cha kisasa, kuwang'oa na kutowachagua viongozi wezi na wala rushwa na kubwa kuliko yote udhibiti wa mali zetu za asili na tutakuwa tuko sawa. Wengi wanaotaka kuvunja Muungano ni wale wenye ujinga wa kuzaliwa na hawawezi kuelimishwa. Pengine njaa na umasikini uliokithiri miongoni mwa baadhi ya wananchi unachangia, kuanzisha mifarakano kwao wao ni faraja lakini ni hatari sana kwa nchi.
Maoni yangu ni kwamba wananchi watoe maoni yao juu ya Muungano na siyo wanataka kuuvunja kwa sababu zao binafsi. Ikiwezekana kiwepo kipengele katika katiba kinachosema;
“IKITOKEA MTU AU WATU WANATAKA KUIHARIBU TANZANIA NI WAWE WA KWANZA KUHARIBIWA”
Hii ni pamoja na wale wanaotaka kupindua serikali iliyowekwa madarakani na wenye nchi yao yaani Watanzania, ama kama kukitokea kiongozi aliye madarakani anataka kutumia nguvu zake za madaraka kubadilisha katiba kusudi andelee kuongoza kwa muda mrefu kinyume cha katiba inayoongoza nchi. Mfano majerani zetu hapo juu na Africa ya kati. Watanzania tupo pazuri sana tusitake kuharibu, Mzee Nyerere amefanya kazi nzuri sana kutufanya tuwe wamoja na wavumilivu. Bunge letu katika vyama vingi kwa muda mfupi tu limeonyesha kukomaa kisiasa na tuendelee hivyo kusudi tuwe taifa lenye nguvu baadaye siyo tu Africa bali duniani.
Napendekeza muda wa Rais kuongoza iwe ni MIAKA 4(MINNE) KWA MUHULA badala ya MIAKA 5(MITANAO) na ibaki muhula miwili kama ilivyo sasa.
Natanguliza shukrani zangu,
Mdau wa ndoto Tanzania itakuwa
Kivutio Afrika Nzima Miaka 10 ijayo.


Pumba 100%!!
ReplyDeleteKama huna cha kusema , ni bora ukakaa kimya tu, watu wasiujue 'ujinga' wako!
Naomba kuuliza swali dogo la nyongeza.Nimekuwa nikifuatilia sana hizi mada za muungano kwa muda sasa,nimesoma maoni,makala,mawazo ya watu,nk.
ReplyDeleteSasa swali langu la nyongeza ni hili hapa.'Hivi ikipigwa kura ya muungano na wanaoupenda wakashinda kutatokea nini".ISije ikwa watu wachahche wanahisi kwamba 99% hawaupendi muungano matokeo yakawa Tofauti.Inawezekana hata Zanzibar watu wengi wakawa wanaupenda muungano tofauti na tunavyohisi wengi wetu".Asanteni.
David V
mzee hauna point,watu washaona muungano hauna maana
ReplyDeleteYaonekana huyu mwandishi mwenyewe ndio mwenye ujinga wa kuzaliwa. Hafahamu kama huu unaoitwa muungano ni makubaliano ya nchi mbili tafauti. Sasa kama wadau wa upande mmoja wowote ule Zanzibar au Tanganyika wamechoshwa au hawaoni maslahi ya kuungana wana haki ya kujitoa katika muungano huu. Kinyume na hivi itakuwa sio muungano ulioundwa kwa ridhaa ya nchi husika bali. Katika dunia ya leo hakuna tena miungano ya kulazimishana kama hii. Ufahamu wangu ni kuwa wazanzibari walio wengi si kwamba wanakataa kuungana na Tanganyika bali ni mfumo wenyewe wa muungano uliopo ndio wanao ukataa. Na haitaki mtu mwenye akili timamu kuona hili.
ReplyDelete