Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akikimbilia basi la Magereza mara baada ya kutoka kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili kwenye Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.

Maombi ya msanii wa filamu Elizabert Michael ya kuchunguzwa umri wake yameshindwa kusikilizwa leo Mahakama Kuu Kanda ya dare s Salaam na kusogezwa mbele hadi Julai 9, mwaka huu baada ya upande wa mashitaka kuomba maombi yasisikilizwe leo.
 
Wakili wa serikali Elizabeth Kadanda aliiomba Mahakama hiyo kuahirisha au kusitisha kusikiliza maombi hayo leo kwasababu wamewasilisha maombi mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa jaji anayesikiliza maombi hayo, Dk Fauz Twaib.
 
Uamuzi uliopingwa ni ule ambao Dk Twaib aliutoa Juni 11 mwaka huu kukubali kusikiliza maombi ya kuchunguza umri wa Lulu ili kujua umri wake halisi baada ya kuwa na utata upande wa mashitaka unadai Lulu ana miaka 18 wakati yeye anadai ana miaka chini ya hiyo.
 
Baada ya maombi ya wakili Kaganda kuomba maombi yasisikilizwe leo kwa sababu tayari amekatia rufaa uamuzi wa jaji huyo, mawakili wa Lulu, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama walisimama kwa nyakati tofauti na kuwasilisha hoja zao kuwa wanapinga vikali maombi ya Kaganda.
 
Walidai ni kinyume cha sheria kwa sababu hakukuwa na amri yoyote kutoka mahakama ya rufaa kuzuia usikilizwaji huo hata hivyo upande wa mashitaka ulionyesha kila dalili kuwa maombi leo yatasikilizwa kwa kuwasilisha viapo pamoja na vielelezo vyao kama mahakama ilivyowataka.
 
Walidai pia kuwa maombi hayo inaonyesha yameifikia mahakama ya rufaa asubuhi hiyo ingawa walikiri huwa yamesajiliwa na kupewa namba, walidai kuwa hiyo ni janja ya ofisi ya mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuchelewesha.
 
Baada ya kusikiliza hoja hizo, Jaji Dk Twaib alitoa nafasi kwa wakili kaganda kujibu hoja za upande wa utetezi hata hivyo Kaganda hakuwa na majibu ya hapo akaomba nafasi kama yadakika kumi kujiandaa na kufanya mawasiliano na aliporudi hakuwa na hoja zaidi ya kusisitiza maombi yake ya ahirisho kutoa nafasi kwa mahakama ya rufaa kusikiliza maombi yao.
 
Jaji Dk Twaib katika uamuzi wake alikubaliana na maombi ya Kaganda akisema kuwa kwakuwa maombi yameshapokelewa na mahakama ya rufaa na kusajiliwa, wakati wowote zitatakiwa mwenendo mzima wa kesi hivyo hana budi kuahirisha hadi Julai 9 mwaka huu.
 
Uamuzi huo haukumfurahisha Lulu alilia huku akifuta machozi baada ya kuona kuwa maombi hayo kwa siku hiyo yamegonga mwamba hayatasikilizwa mpaka kusubiri amri ya mahakama ya Rufaa.
 
Hata hivyo jaji huyo alitoa amri nyingine kuwa haitakiwi mahakama ya Kisutu kuendelea na kesi hiyo mpaka pale uamuzi utakapotoka mahakama hizo za juu, uamuzi ambao ulipuuzwa kama alivyodai wakili Fungamtama kuwa Lulu alipelekwa Kisutu na kesi ilitajwa katika jalada lililofunguliwa la muda.
 
Katika maombi hayo, tayari upande wa jamuhuri katika maandalizi ya kusikiliza ulikuwa umeshawasilisha Mkanda wa video aina ya CD, yenye mahohjiano kati ya mshtakiwa huyo na mtangazaji mmoja kuthibitisha kwamba umri wa Lulu ni zaidi ya miaka 18. Vingine ni maelezo ya mshtakiwa huyo aliyoyatoa polisi wakati alipohojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, maombi ya hati ya kusafiria (Passport) na maombi ya leseni ya udereva.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba aliyefariki dunia nyumbani kwake Sinza, April 7, 2012.  

Hata hivyo umri wake umezua utata baada ya mawakili wake wanaomtetea kudai kuwa bado ni mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama hati ya mashtaka inavyoonyesha.

Hivyo mawakili hao walilazimika kuwasilisha maombi mahakamani kuiomba mahakama iruhusu ufanyike uchunguzi wa umri sahihi wa mshtakiwa huyo na ikiridhika kuwa ni mtoto basi kesi yake iendeshwe kwa misingi ya kesi za watoto wanaokinzana na sheria ili kulinda maslahi.

Mawakili wa Lulu waliwasilisha viapo vya wazazi wake,
cha mama yake Lulu Lucresia Augustin Kalugila, mkazi wa  Dar eS Salaam na kiapo cha baba mzazi Michael Kimemeta, mkazi wa Moshi.

Viapo  vyote vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo alizaliwa April 16, 1995  katika kituo cha Afya Muhimbili na kupewa cheti cha kuzaliwa namba B.0318479 cha Julai 23, 2004.
Pia viapo hivyo vinaeleza kuwa baada ya kuzaliwa mshtakiwa,  mama yake alimpa jina la Diana Michael Kimemeta, lakini alimpeleka mtoto huyo Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndugu zake, walimpa jina la Elizabeth, jina la bibi yake Elizabeth Shikana.

Viapo hivyo vinaendelea kueleza kuwa baada ya majadiliano wote, yeye mama, baba na ndugu wengine walikubaliana kuwa wamuite Diana Elizabeth Michael Kimemeta. alibatizwa katika Kanisa la Katoliki  Chang’ombe Septemba 28, 1997 na alichukua majina ya ubatizo Diana Elizabeth Michael Kimemeta

Utata wa umri wa mshtakiwa huyo uliibuka Mei 7, 2012 katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya wakili wake Fungamtama kudai kuwa ana miaka 17 Mahakama ya Kisutu iliyakataa maombi hayo ikisema kuwa haina mamlaka ya kuyashughulikia na kushauri maombi hayo yawasilishwe Mahamaka Kuu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2012

    Mi naona haya ni mabishano ya kisheria tu. Ktk nchi zilizoendelea passport ndo msemaji wa mwisho kuhusu umri wa tu. Inaonekana kwenye siyo hivyo. Hata hivyo kama wanataka ukweli kamili waangalie vielelezo alivyowasilisha wakati anaomba passport (watakuta kopi ya cheti cha kuzaliwa au affidavit), vyote hivyo vinaonyesha mwaka wa kuzaliwa.

    Nina imani cheti cha kuzaliwa walichonacho mawakili wa utetezi tayari kimeishachakachuliwa, chezeya bongo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 26, 2012

      Na pia kwa upande mwingine inawezekana kuwa passport hyo iliombwa kwa vyeti visivyo sahihi....ukipewa nafasi ya kuthibitisha kimechakachuliwa, utaweza? Wacha watu wafanye kazi yao. Kitu ambacho wanaona ni sahihi.

      Delete
  2. AnonymousJune 25, 2012

    Lazkma tukiri kwamba ni uzembe wetu ndiyo umetufikisha hapa. Tatizo dogo tu la kujua tarehe halisi ya huyo msichana kazaliwa lini linatupa shida. Angalia tunavyopoteza muda, kitumia rasilimali nyingi kuanzia ulinzi na vinginevyo kushuhulikia hicho kitu. Gharama ni kubwa kuliko kama tunhekuwa na utaratibu wa kuweka kumbukumbu vizuri. Leo hii majaji, mahakimu , afisa mahereza na polisi wanatumia muda mwingi kwenye issue ndogo kama jii. Tunacjoma mafuta ya magari na menhineyo ambavyo vingetumika kwenye vitu vinavyohitaji hao watu na rasilimali hizo.
    Na huyo ni mtu aliyezaliwa hapohapo mjini Dar. Kama angekuwa amezaliwa kijijini mbali na ni mpakani mwa nchi ingekuwaje ?
    Serikali nayo inakuja na hija dhaifu kuwa kwenye maombi ya pasi ya kusafiria na uderva aliandika ana miaka 17 hivyo sasa atakuwa na miaka 18. Sasa kama alifanya kosa la kuidanganyajamhuri tokea huko kwenye maombi, je sasa mnataka kumuhukumu kwa adhabu ya mauaji badala ya kusema uongo ? Serikali ilitakiwa ijiulize iliwezekana vipi kama mtu alidanganya na akafanikiwa kupata hivyo vitu na jinsi gani ya kuzuia hilo. Na si kuja kuonyesha tena udhaifu wa kutofuatilia mambo kikamilifu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 26, 2012

      Bora gharama kuliko kuharikisha mambo na kufikia kwenye uamuzi ambao utakapokuja kugundulika kuwa si sahihi, utaleta madhara makubwa zaidi ya hzi pesa zinazopotea. Kumbuka hii ni kesi inayohusu mauji, na sio uvunjaji vyombo....umakini ni lazima.

      Delete
    2. AnonymousJune 26, 2012

      Talking about gharama ya kuupata ukweli sasa ni kubwa zaidi kuliko ambayo tungeingia kama tungewekeza kwenye namna ya kuweka kumbukumbu za uhakika mahospitalini na sehemu zinginezo tokea day one huyo mtoto anazaliwa. Kumbuka tonaongelea miaka ya tisini hapa, hata miaka ishirini haijafika. Siyo thirties or fourties hapa, it is 1990's !!
      Na vilevile haki haina gharama, soma tena maelezo kabla ya kujibu kimakosa.

      Delete
  3. AnonymousJune 25, 2012

    tz kila kitu fake, hata vyeti vya kuzaliwa feki. labda wawaulize majirani kama kuna mwenye kukumbuka alizaliwa lini. na kama mamake alikuwa kweli anafanya kazi sijuhi atc; basi waangalie faili waone lini aliomba leave kwenda kujifungua; ina maana hatuna wapelelezi? mbona issue simple hii.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2012

    Ninyi kina Kibatala mjitolee basi na kesi zingine zote za mauaji kuna watu wanasota huko rumande zaidi ya miaka mitano hata kuona wakili wakuwapa pole hawajawahi ila hii naona inakwenda kasi kweli kweli mbali na hiyo kuwa ni junior offender lakini chezeni fair basi ili hata wale ambao jamii haiwajui muwateetee

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2012

    Kwa kweli umma umepoteza mda mrefu sana kufuatilia suala ambalo halikuwa la msingi, mimi sioni ni kwa sababu gani umri utamzuia prosecutor kum-trial huyu Binti kama mtu mzima. To cut the story short, huyu binti hakumuua Kanumba kwa kukusudia, in order to charge someone with the first degree murder – the doer has to have conspired to kill, in this case the girl had no intension and no motive. In such an incident it is called a tragedy accident, and not a murder. Prosecutors have no case here, the girl should be let free, you can only charge her with intentionally neglect and fail to notify authority at the time of incident. The defense team didn’t need to use this age thing, the case is weak by itself.
    If a weapon was used, to inflict wounds that would be something else, but from the woman perspective, and her body physic she, could not through a punch to inflict that kind of injury. The man died from the concussion (brain hemorrhage) results from the back head fall.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2012

    Katika kesi zote zinazohusu kifo naona hii inakwenda vizuri sana. Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni sheria zetu ambazo hazitoa dhamana kwa kesi mauaji. Hii sheria ina mapungufu makubwa sana...Watanzania wengi sana wanasota rumande miaka na miaka kwa sababu tu WAMETUHUMIWA kwa mauaji. Ilitakiwa walau polisi/waendesha mashitaka wawe na ushahidi wa awali kuonyesha kwa nini wana amini mshitakiwa atakutwa na hatia, ndipo Jaji awe na maamuzi ya kumuweka rumande au la. Ilivyo sasa eti kwa kutuhumiwa tu ndio haki zote za dhamana zinatoweka sio sahihi kabisa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2012

    LULU KAZALIWA DAR MZUNGUKO NA GHARAMA ZA KUFATILIA UMEKUWA MKUBWA SANA. NENDA ALIPOZALIWA KUNA KUMBUKUMBU. KAMA ALISEMA KTK KIPIDI KUWA ANA 18 HUO NI UONGO WAKE. KINACHOTAKIWA NI KUMBUKUMBU ZA MAANDISHI. KUJUA TU UMRI IMEKUWA NENDA RUDI JE KESI YENYEWE ITAKUWAJE JAMANI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2012

    Wana akili zao kuiendesha kesi kama inavyokwenda, subirini tuu na tuombe uhai muone kitakachotokea mwishoni.
    Nilikua napita tuu.....

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2012

    Mwenendo mzima wa kesi hii unasikitisha sana. Mpaka sasa kiasi kikubwa sana cha fedha kimeshatumika hii ni pamoja na askari wanaoimarisha ulinzi, mafuta, muda na kadhalika. Tatizo linaanzia kwa huyu binti ambaye anajulikana kwa kutosema ukweli. Hivi hakuna hata kumbukumbu zake za shule alizosoma ambazo zitarahisisha swala zima la umri wake? Kwa sheria zetu za usalama barabarani lazima mtu atimize miaka 18 ili aruhusiwe kupata leseni ya kuendesha gari. Lulu aliwezaje kumiliki na kuendesha gari kipindi chote hicho? Mtoto wa miaka 17 aliwezaje ku sign mikataba yake ya kazi?
    Lazima tuelewe kesi hii ina mtazamo mwingine ukizingatia kwamba wahusika ni watu wanaofahamika. Hivyo basi si Tanzania tu bali dunia nzima inafatilia mwenendo mzima wa kesi hii. Itakua jambo la aibu kwa Taifa letu kama tutawekwa katika mkumbo wa nchi ambazo 'haki' za kisheria zinategemea umaarufu au pesa za mtu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2012

    Kwenye jamii yetu, wengi hawana ufahamu juu ya sheria, in particular sheria juu ya mauji yani Murder au Manslaughter (Voluntary au Involuntary Manslaughter). Kila kipengele cha kesi ya mauji lazima kichambuliwe ili ifahamike kesi hii inahangukia kwenye either Murder au Manslaughter then uchunguzi wa kina unaendelea, ila jamii tunaongea sana kisa tu tunamawazo yetu, lazima tutulize akili. Vithibisho walivyonavyo mashtaka au watetezi havijulikani kwetu sasa tunapiga kelele za nini? Na rudia kusema hii ni kesi ya mauji na uamuzi wake sio wa siku kadhaa. Fatilieni kesi zote zinazoendelea au zilizopita sehemu mbali mbali duniani ndio tutakapoona umuhimu wa kila jambo. Tuache watu wafanye kazi zao.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2012

    DNA ipimwe !

    Wanapoteza muda sana wakati suluhisho la Kisayansi lipo.

    Lulu apimwe chembe asilia ili kubaini umri wake halisi.

    Hiki kipimo hakina masihara kabisa wanaweza kujua hadi siku alizoishi Duniani tokea azaliwe, itakuja kuwa umri tena?

    DNA au kipimo cha chembe asili ndio mtatuzi wa suala hili la umri waisopteze muda bureee.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 26, 2012

    Hapa jamani alichofanya Lulu ni kutaka uhuru wa kufanya mambo yake kama sheria inavyotaka ndio maana akachakachua umri na kuwa miaka 18 ili aweze kwenda viwanja na mambo mengine ya kiutuzima. Limetokea hili wanaanza hoja ya kushusha umri but bado naungana na mdau mmoja ali-comment juu pale kwamba huu ni uzembe wa serikali ndio umetufikisha hapa tulipo kiasi kwamba kwa Mtanzania unaweza kutaja umri wowote unaotaka kwani watanzania wengi hawana vyeti vya kuzaliwa ila tunashukuru angalau sasa hivi serikali imeanza kuchukua hatua kwa mwanafunzi hawezi ku-join shule mpaka chuo bila kuonyesha cheti cha kuzaliwa hii nadhani itasaidia sana kufanya watu wawe na cheti.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2012

    Kama ni adhabu basi mtoto huyu Lulu ameshaipata. Inavyoonekana mawakili hawana njia ya kutokea kama huyu mtoto hakuua. Hivyo njia iliyobaki pekee ni ya umri tu.
    Adhabu aliyopata mtoto huyu inatosha sasa. Wanasheria toeni hukumu ajue yuko huru au mfungwa!.....Kizito!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 27, 2012

    kama amezaliwa miaka ya 90 basinendeni hospitali aliyazaliwa mtaje tarehe na mwaka kuna copy ya tamko rasmi la mtoto kuzaliwa copy moja inaenda msajili wa vizazi na vifo na ingine inabaki kweye kitabu cha hospitali original anapewa mzazi ili akaombee cheti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...