Malkia wa mipasho na mshindi wa tuzo za Tanzania Kili music Awards 2012 Khadija Kopa  (pichani) anategemewa kuwa kivuto kikubwa kwa kutoa burudani ya kipekee katika shindano la kwanza la kumsaka mlimbwende wa MISS lAKE ZONE INTERCOLLEGES 2012 mnamo  Juni 23, 2012 katika ukumbi wa Linuz Club mjini Bukoba mkoani Kagera.
  Mwandaaji wa shindano hilo Bw.Joseph Rwebangira amesema kuwa asilimia kubwa ya maandalizi yameshatimia,hata hivyo Rwebangira aliongezea kuwa mshereheshaji wa siku hiyo atakuwa mchekeshaji maarufu afrika mashariki na kati Mpoki wa the origina comedy.
   Miss Lake zone Intercolleges 2012 inayoandaliwa na kampuni ya Angles Real Entertainment ya jijini Dar es salaam chini ya Mkurugezi wake Joseph Rwebangira imejipanga vya kutosha kuleta mabadiliko ikiwa na lengo la kumfikisha mrembo wake katika ngazi ya fainali kitaifa.

  Siku hiyo pia  kutakuwa na burudani za ngoma za asili na wasanii wa mkoa wa Kagera. Mchango getini utakuwa Tsh 10,000/= kawaida na V.I.P ni Tshs 15,000/=

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...