Wadau wa michezo wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya mada mbalimbali katika Kongamano la Michezo kwa Maendeleo na Amani lililoanza leo katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar es Salaam. Aliyekaa mbele ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Taasisi za Right To Play na British Council kwa lengo la kuwapa fursa wadau wa Michezo kubadilishana uzoefu na kujadili ni jinsi gani michezo inavyoweza kutumika kuhamasisha maendeleo na amani katika jamii.
Mkurugenzi wa British Council nchini, Bibi Sally Robinson akiongea na Wadau wa michezo (hawako pichani) wanaoshiriki katika Kongamano la Michezo kwa Maendeleo na Amani leo katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Concilia Niyibitanga- WHVUM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...