Waandishi wa habari wanapata shida sana wakati wa kuripoti habari za Bunge. Eneo walilotengewa ni dogo, kiasi kwamba wanalazimika kuketi chini. Wanapata usumbufu mkubwa wa kuingia katika chumba hicho kwa sababu wanalazimishwa kupanda na kushuka ngazi nyingi, huku wakipita katika vyumba vingi kabla ya kugota eneo walilotengewa. Huu ni unyanyasaji ambao ofisi ya Bunge imeufumbia macho. Ukumbi ulipojengwa waandishi wa habari hawakukumbukwa kabisa. Kamainakuwa hivi kwa wanahabari, hali ikoje kwa walemavu wasiokuwa na wa kuwasemea? 
Picha ya mdau Manyerere Jackton, Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2012

    Huyu aliyeketi chini mbona hana hata mpango wa ku take note ama kajaza tu huo ukumbi????Poleni sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2012

    Siku zote binadamu kuna wakati tunalazimisha kuongea maneno ili tuonewe huruma hata kama jambo lenyewe hata bila kuliongezea maneno linajitosheleza.Kwa hali hiyo tunajikuta tunatamka maneno ya kuudhi bila kujua,unaposema walemavu hawana wa kuwasmea unaongelea walemavu wapi?nani kakwambia hatuna mtu wa kutusemea,kutusemea nini maana usilete madai yako kupitia mgongo wetu,unachodai ni kweli lakini usishike usifanye walemavu ikawa ajenda ya kupitia!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2012

    Wanalibeneke,

    Zaidi ya hali hiyo ya mazingira ya kikazi hapo Bungeni na fedheha kubwa mnayokabiliana nayo kazini.

    Kwa kuwa BUNGE huo ni mfereji wa Mabilioni ya Fedha watu wanalipana haikustahili mahali panapochinjwa mnyama mengine wasiambulie hata manyoya?

    Hii imekaa sawa wandugu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2012

    Lakini umepita muda mrefu tangia ukumbi huu uanze kutumika na haswa sijawahi kusikia malalamiko. Jitahidini kupaaza sauti, mtasikilizwa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2012

    Ipo haja ya mtoa hoja kurejea historia ya kwa nini waandishi wanakaa pale walipo. Nadhani suala si gumu kama linavyowekwa, ni suala la wao waandishi kuiarifu Ofisi ya Bunge rasmi ili warejeshwe katika ukumbi wao wa awali, ambao ni mkubwa sana ukilinganishwa na huu wa sasa. Nadhani kwa sasa ndio suluhisho linalowezekana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2012

    SOMA POST JUU KUNA MDAU AMEJIBU KWA KUONYESHA SEHEMU AMBAYO WANAPASWA KUKAA KWARAHA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2012

    Manyerere unalako jambo, mbona maelezo yako hayaendani na ukweli uliopo Bungeni! upande wa kuingilia wageni Gate C mbona kuna hata mashine ya kutumia walemavu wa miguu kuingia Bungeni, alafu kuhusu waandishi hapo mlipo ndio sehemu yenu? na wote kweli hapo mnaandika story? kama ulikosa siti si ungetumia njia nyingine sio kutumia migongo ya wenzio.... Hoja yako haina mashiko

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2012

    Hivi wote hao ni waandishi au wengine wamekwenda kuuza sura?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2012

    Mdau sasa anzisha NGO ya walemavu ili uweze kuwa msemaji wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...