Makamu wa Rais MCC Idara ya Utekelezaji Bw Andrew Mayock (wa pili kushoto) akimuleleza jambo Mh. Naibu Waziri wa Maji Dr Benelith Mahenge alipmtembelea ofisini kwake Ubungo Maji kwa mazungumzo.Anayemuangalia ni Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Bw.Jakson Midala
Na Nurdin Ndimbe
Naibu Waziri wa Maji Dr Bernelith Mahenge amekutana leo na Makamu wa Rais wa MCC Idara ya Utekelezaji Bw.Andrew Mayock ofisini kwake Ubungo Maji jijini Dar Es Salaam.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na MCC kwa upande wa Wizara ya Maji Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Inj.Christopher Sayi alimueleza mgeni huyo kuwa, kwa sasa Millennium Challenge Cooperation (MCC ) wanafadhili upanuzi na ujenzi wa chujio la maji katika matambo wa Maji Ruvu Chini.
Na ujenzi wake unategemea kukamili mwanzoni mwa Aprili 2013. Utakapokamilika utaongeza uwezo wa kutoa lita milioni 90 kwa siku ukilinganisha na lita milioni 182 kwa sasa.
Kuhusu ujenzi wa Bomba la kuu la pili toka Ruvu Chini hadi Dar Es Salaam Inj. Sayi alisema kuwa, tayari Wizara imepata fedha ya kugharamia ujenzi huo.Mradi huu utakapokamilika utagharimu dola za Marekani 82.5 na utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika jiji la Dar Es Salaam.
Pamoja na hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji alimuomba Makamu wa Raisi kungalia uwezekano wa MCC kufadhili ujenziwa bwawa la Kidunda kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mtirirko wa maji katika mto Ruvu unakuwa kwa majira yote.
“ pamoja na miradi mingine kuendelea tungependa wenzetu wa MCC kuangalia uwezekano wa maeneo mengine wanayoweza kutusaidia kama ujenzi wa bwawa la Kidunda na Farkwa kule Dodoma michakato yake iko tayari lakini tunakosa fedha’’ alisistiza.
Kwa upande wake Bw Andrew Mayock Makamu Rais wa MC,alifurahishwa na kasi ya maendeleo ya miradi yote ya MCC hapa Tanzania na kueleza kuwa Serikali ya Marekani inaridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa hivyo inafikiria kuiongezea misaada zaida Tanzania katika Sekta mabalmabali ‘’Tanzania ni moja ya Nchi inayofanya vizuri kwenye miradi ya MCC hivyo Marekani ina nia ya dhati kabisa ya kuiongezea misaada zaidi ‘’alisema


.png)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...