Mimi nimesoma katika shule moja ambayo ipo maeneo ya Boma Road Morogoro. Jamani, nimesoma katika kipindi cha miaka 9 katika shule hiyo na mpaka namaliza shule hiyo nakumbuka kuna miti miwili tu iliyokatwa, mmoja ulipunguzwa matawi wakati nikiwa shuleni hapo na mwengine nilipata taarifa kuwa ulikatwa sababu ya kuongeza madarasa.
Sasa sasa hivi kuni hii sijui style au dili inaendelea hapa, sielewi kama Mkuu wa Mkoa ana vibali vya kuhusian ana haya, maana ndio njia anayopita daily.
Hii barabara ya boma ina miti iliyopandwa urefu wa si chini ya kilomita mbili (kama picha inavyoonesha). Sasa hivi ninayoongea mti wa Sita kama sio 8 umeshakatwa katika eneo la shule ya Mji Mkuu (Opp. Nashera Hotel).
Mi sielewi maana ipo ipo barabarani tena karibu na na shule, sasa ina dosari gani mpaka ikatwe yote kubakiza visiki? Nilitembelea Udzungwa nikakutwa magogo yanakatwa, kuuliza nikajibia Hii mimi inaua vyanzo vya maji (Kwamba inanyonya Maji Sana). Nikajiuliza : Hii miti (Udzungwa) ni natural Forest, ilikuwepo pale muda mrefu na maji yalikuwa mengi tu - WHAT HAPPENED, MPAKA IANZE KUTUMIA MAJI MENGI 2011?
Najiuliza na hii ya Boma Road (Michongoma) nayo inatumia maji mengi?
Ushauri : Kama hakuna sababu ya kukata bora wapunguze matawi, hizo dili za kupeleka kuni viwandani zitatungharimu baadae, maana miti ikiisha tutanza kutoa vitanda vyetu.
2. UCHAFUZI WA MAZINGIRA / HASWA MAJI YA KUNYWA.
Ukifuatilia mabasi yaendayo mikoani, yaani utafikiri nyuma yake kuna Shimo la Taka. Mimi si msafi kivile lakini hii sio jamani. Hebu tuchukulie Dada Dina yupo kwenye kipindi Clouds / Fred War yupo RFA pamoja na presenters wengine wambao wanakuwepo asubuhi. Kati ya Saa Tatu Hadi Saa Saba wanatangaza - KILA MTANZANIA ALIYESHIKA CHUPA YA MAJI AITUPE HAPO HAPO ALIPO. Naomba tusaidiane Tanzania yetu itakuwaje ndani ya kipindi cha Wiki Moja? Najua tutasema kisingizio ni kuwa hakuta Tank za Taka.
ANYWAY THIS IS NOT A POLITICAL PLATFORM AND I AM NOT BWANA AFYA, NAOMBA NIISHIE HAPO.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.



Tatizo wenye viwanda vinavyotumia kuni kama tuko karne ya 11,hawataki kutumia makaa ya mawe ambayo yapo bongo tele,wahajari kabisa athari za kukata miti wao wanajari faida tuu.Pili Muozo wa Watawala wetu[Mawaziri,wakuu wa Mikoa nk]ambao ni mzigo tuu ambao hawaoni kukata miti na kiwanda kutumia kuni si jambo zuri.Miembe hiyo ilipandwa na Mjerumani na Muingereza na barabara hiyo ilikuwa inaitwa Morning Side.
ReplyDelete