Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Ndg. Symthies E. Pangisa (Kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma wakati wa kupokea Mwenge huo kutoka Mkoa wa Ruvuma
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Cpt. Honest Mwanossa akitoa maelezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa soko la samaki la kisasa katika Manispaa ya Mtwara/Mikindani, huku akisikilizwa kwa makini na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani Mhe.Mtalika na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Magreth Nakainga
 Cpt Honest Mwanossa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akipanda Mti kama ishara ya utunzaji wa mazingira katika mojawapo ya Shule za Sekondari Wilaya ya Newala wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Mtwara
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akikagua shughuli za useremala zinazofanywa na kikundi cha vijana wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtwara (mwenye kofia nyeupe)


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Ndg. Hipson Kipenya (mwenye kofia nyeupe) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mtegu Mkoa wa Lindi. Picha na Habari na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara

Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mtwara zilianza rasmi tarehe 03/06/2012 ambapo Mwenge ulipokelewa kutoka Mkoa wa Ruvuma katika Kijiji cha Lumesule, Wilaya ya Nanyumbu na kukimbizwa katika Halmashauri 6 za Mkoa wa Mtwara.
Ukiwa Mkoani Mtwara Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa umbali wa Kilometa 588 na kupitia jumla ya miradi 63 yenye thamani ya shilingi bilioni 6.1 iliyo katika sekta ya Elimu, Afya, Vijana, Ushirika, Kilimo, Mazingira na Uvuvi. Katika Miradi hiyo Mwenge ulifungua miradi 13, umeweka mawe ya msingi miradi 10, umeona/kukagua miradi 27 na umezindua miradi 13.
Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiongozwa na Kiongozi wao Capt. Honest E. Mwanossa waliweza kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara ambapo kwa Mwaka huu ujumbe maalum wa Mwenge wa Uhuru ukiwa Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu chini ya kauli mbiu Shiriki Kuhesabiwa tarehe 26 Agosti 2012.
Pamoja na ujumbe huo maalum wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu uliowasisitiza wananchi umuhimu wa kuhesabiwa, pia wananchi wa Mkoa wa Mtwara waliweza kupata elimu juu ya kujitokeza kutoa maoni yao kwa Tume ya Katiba, mapambano dhidi ya Ukimwi, dawa za kulevya na rushwa.
Mwenge wa Uhuru ulihitimisha mbio zake Mkoa wa Mtwara tarehe 09/06/2012 kwa kuukabidhi kwa Mkoa wa Lindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...