Home
Unlabelled
mdau afanikisha harambee ya kutengeneza shule morogoro, msaada zaidi wahitajika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mkubwa na kushukuru na na kusifu kwa kufanya kitu ambacho wengi wetu hatutaki kufanya au tunajifanya kana kwamba hatuoni. cha msingi tu mkuu, jaribu kufanya dizaini ya madarasa yenye gharama nafuu. Hii picha hapa inaonyesha darasa hili limegharimu zaidi pasipo sababu, kwanza ,umetumia tofari za choma ambazo zinatumika nyingi na simenti nyingi sana inatumika kwa ujenzi huu. Kumbuka kwamba mfuko mmoja wa simenti unaweza kukupa tofari 35 imara sana na zikijengwa na fundi mzuri ,basi hata plasta siyo lazima. kingine ninachokiona kwenye picha ni madirisha yako ni makubwa mno na yako juu sana ,pia kuta zako ni ndefu mno pasipo sababu, je hao watoto watarefuka zaidi ya futi 5 au 6 ??? kwa kuupunguza urefu wa kuta zako ,utaokoa tofari,simenti,bati,na muda. Obeja baba. wako Zebedayo ,mna Badugu. Jamani tuchangieni mada kama hizi. Cha ajabu ,punde kukionekana -Ukristo na uislam -mama yangu weee,paka na panya-yaani umechokoza nyuki. Hebu elimikeni.
ReplyDeleteNapenda nimpongeze saaaana mdau aliyeona kero na mapungufu ya serikali na akaweza kuhukua hatua binafsi na kufanikisha kiasi hicho. hongera sana na naomba tuendelee, sisi tumetoka kuhangia millioni 50 kwa ajili ya mambo yanayowagusa wasiojiweza. ILA Mdau aliyetangulia 05:01:00 napenda nimfahamishe kuwa madarasa ni muhimu sana yawe makubwa ya kutosha na ceiling height kuwa ndefu ili room size iwe kubwa. pia madirisha yanahitajika kuwa makubwa hata zaidi na yawe chini. wanafunzi wanahitaji hewa ya Oxygen yakutosha kuweza ubongo kufanya kazi. kwa hiyo huo ni upungufu wa ufahamu wa mdau. ila sina uhakika na research yake kuwa kujengea matofali ya cement nirahisi kuliko ya kuchoma. Naamini kuwa kama ni kijijini wanachimba udongo na kuchoma wenyewe. ILA amenishtua na kusikitisha sana alipoingiza udini??? katika swala muhimu kama hili.
ReplyDeleteDUH !!!! yale yale . Huo ubongo unaohitaji oxygen yote hiyo,basi utakuwa umelala kama maziwa mtindi, kingine ,hata mimi nashangazwa sana na hao watu wanaokimbilia kuitoa maoni ya Udini,ndiyo maana nikalikataa jambo hilo-sasa wewe umeshitushwa na nini ??? au hukunisoma vizuri na kunielewa point yangu-hata wewe ulipoliona neno dini tu-hapo hapo ukashambulia ,ndo wale wale !!!! kingine , tembea uone mengi ,mimi nimekupa dizaini za madarasa za nchi nyingine -wenzetu wanavyojenga na oxygen imo madarasani na wanafunzi wanafaulu hadi kunyakua PHD,kipimo mtu mzima ukisimama ukinyosha mkono unagusa kwenye ceiling. Kingine tofari za choma zinazofyatuliwa huko vijijini, wengi huwa hawazingatii udongo gani,maadam ni mwekundu basi twende kazini,matokeo yake ni hafifu sana na baadaye zinahitaji simenti nyingi sana ya kujengea na muda mwingi . Nafikiri nimekusaidia .Asante,nipo bado jaribu tena.
ReplyDelete