Habari za leo Ankal na timu yako nzima.

Naomba unipandishie lalamiko langu kuhusi usimamizi mbovu uliopo pale Kivukoni,Kiukweli kabisa mimi sina tatizo na Dk. Magufuli kupandisha nauli za Kivuko,ila tatizo langu ni yeye Mh. kuacha usimamizi mbovu pale kwani nini nasema hivyo kuna watu wamefanya wenyewe ni maalwatani wenyewe hawapangi foleni wanapita bila kulipia sisi ambao sio maalwatani tunawai asubuhi tunakaa kwenye foleni tunalipia ila wakija wao hawakai kwenye foleni hawalipi yaani inaboa sana.

Halafu wale walinzi wamekaa kama pambo pale kwenye geti lao,Maana linatumika vibaya sio kwa makusudi yaliyoweka na Walinzi wa suma jkt watu na magari yao wanapita no entry.

Mi naomba Dk Magufuli hilo aliangalie.

Mdau wa Kigamboni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Kweli hili ni tatizo kubwa sana kigamboni, na lile geti la jeshi wanaopita ni kina nani? siku hizi geti hilo asubuhi lina foleni mpaka chuo cha mwalimu nyerere na ni magari binafsi. Inaboa sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Kwa kweli hapo mahali panaboa sana.Inawezekanaje watu wachache pamoja na magari yao wanapita bila kupanga foleni na bila kulipia nauli ya kivuko.Hivi kweli ukiwa na nyadhifa yeyote ya chama tawala ndo usilipia ushuru wa kivuko.Mnaowakamua ni wale wale wananchi wa hali ya chini ambao wamewawezesha kufikia hapo mlipo.Tufike mahali watanzania tudai haki yetu.Wanyonge wamekuwa ndo wanaolipa kila kitu.Walipe kodi mpaka wawalipie nauli kwa ajili ya kuendeshea gharama za kivuko?Kwa kweli inauma sanaaaa..............................................

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Duh namsupport huyu mdau aliyeleta hii kero hapa kwa asilimia zote. Nikiwa mkazi wa Kigamboni kuna mambo yanatendeka pale ferry ambayo hata mbele za Mungu ni dhambi kubwa sana. Wapo wenye magari ambao wanafuata utaratibu uliowekwa, waenda kwa miguu, wasukuma mikokoteni, maguta, wapanda baiskeli, pikipiki, hawa wote LAZIMA walipe na usipolipa utadhalishwa vibaya sana. Hao niliowataja hapo juu ndio wanaowezesha vivuko hivyo kufanyakazi bila kugharamiwa na serikali. Inashangaza sana mtumishi wa serikali analipwa mshahara mzuri, posho mbalimbali, gari zuri, dereva wa serikali, mafuta ya serikali, kweli jamani hawezi kulipia kivuko mpaka alipiwe na mlalahoi, mwanafunzi au Mama anayekwenda kununua samaki sokoni ferry na kurudi kuokoteza? Hivi hapo haki ipo kweli jamani??
    Mhe Magufuli, hawa wengi wasiolipa wamegawanyika kwenye makundi tofauti sana na wanasababisha mamilioni ya fedha kupotea.
    Kuna geti la emergency upande wa kigamboni, yupo askari ambaye habadilishwi huyo ndio anatajirika. Sipendi kuongea sana bila kuweka ushahidi hapa, ila jaribu kutuma mtu wako asb kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa tatu, huyo atakupa taarifa kamili ya idadi ya magari yanayopitia geti hilo bila kulipa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    Hehehe WENZAKO WANAHONGA WAKIWA NA HARAKA ZAO WEWE SI BAHILI USIWE MBAHILI Tehteh! ILA TURUDI KWENYE MADa.

    1. TABIA ILE IFE
    2. MANTONI KUBWA KWANINI WANALAZIMISHIa MAGARI MPAKA KWENYE MIGUU YA VITI? WALEMAVU NA WAZEE WAKAE WAPI? JUU? WAPANDE NGAZI?

    3. KWENYE KIDIRISHA WAFANYAKAZI KIBAO WENGine WANAWEKA KIJIWE WAKATI WA KaZi SIELEWI MIE.

    4. TUTAANZA KUVUKA NA NGALAWA WACHA WARINGE. MZ

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...