Ankal pongezi nyingi kwako kwani blog ya jamii inaelimisha na kupashana habari mapema sana kuliko nyinginezo.
Juma lililopita kuna mdau alieleza kinachoendelea kwenye mji wa Arusha.Kama ni mambo ya kisiasa kweli Arusha imerudishwa juma kama miaka thelathini iliyopita. Nasema hivi kwa kuwa inatia uchungu kuona Arusha iliyokuwa ikisifika kama mji wa kimataifa,leo hii umekuwa mji mchafu usiokuwa na sheria,ninamaanisha kila mtu anafanya atakavyo na hakuna wa kumwuliza au kumkataza.
Biashara zinafanywa popote na bila mpangilio,unakuta mama lishe pembeni ya barabara ambayo ndio barabara kuu ya hapa Arusha wanapika chakula na majiko yao,kuna barabara hazipitiki kwa kuwa wauza viatu wametandaza biashara zao.
Jambo lingine linalozidi kwa kasi sana ni matangazo ya waganga wa kienyeji. Kila baada ya nguzo tano au saba za Tanesco kuna tangazo la mganga na namba zake za simu. Vibao imekuwa havionekani kirahisi kwa wapitao kwa magari, sasa wanaweka mabango makubwa ya vitambaa.
Hivi Arusha imekuwa haina uongozi au siku hizi
rukhsa kufanya chochote na popote ili mradi upo mjini?


Mtaiweza nchi nzima ninyi?
ReplyDeleteHaya Chadema Arusha inawatoeni kamasi!
Kushiriki Siasa za Kiushindani sio kigezo cha kuendesha mambo 'Kiswahili' Mazee mpo hapo?
Hiyo Arusha ni mji muhimu sana hapa Afrika ya Mashariki (sio tu kwa Tanzania) kama mnavyoona Makao Makuu yapo hapo na Katibu Mkuu Dr.Richard Sezibera ndio makazi yake.
Mkumbuke ya kuwa Mji anaotka huyo Katibu Mkuu wa EAC Balozi Dr. Sezibera hakuna mchezo !!!
Kila Jumamosi wakazi wanafanya usafi wa Mji wa Kigali bega kwa bega na Raisi Kagame !
Acheni masihara mkileta mchezo tutawaitieni Raisi Kagame aje kuwashikisha adabu kwa Wakazi wote Arusha kufagia mji kila Jumamosi muujue usafi wa jiji!
Ebo?
Haya sasa CDM mpo 'Lege lege' kuiendesha Arusha mji mmoja tu nchini!
ReplyDeleteNchi hamuipati ng'o !!!
Mkipewa wale Wakaanga samaki wa Feri mtawaruhusu wafanyie shughuli zao hadi Ikulu!
Si ndio watu watajisaidia hadi Ikulu?
UCHAFU ARUSHA,
ReplyDeleteMnaona Chadema mlivyo 'legelege'?
Mdau nakuunga mkono. Mimi nimezaliwa na kukulia Arusha. Nimefanya kazi Arusha miaka ya late 90's.
ReplyDeleteNinachoweza kusema ni HALI NI MBAYA. UCHAFU, VURUGU, MAJAMBAZI, MATANGAZO KILA KONA, BIASHARA ZA MIKONONI, BODA BODA, UJENZI HOLELA. NA KWASABABU BARA BARA KUU INAYOPITA MJINI KATI NI MOJA [SOKOINE ROAD BASI FOLENI BALAA.
Chadema mnaiteketeza Arusha!
ReplyDeleteUmahiri wa Kisiasa sio kuendesha mambo kiholela!
Mnatakiwa mfunge mkanda mambo yaendeshwe kwa mpangilio!
Hivi Mji ulipokuwa chini ya CCM ulikuwa katika hali hiyo?
John Mnyika kazi kwako!
ReplyDeleteHaya kawapange Machinga Arusha kwa kuwa Chama chako kimekuwa legelege!
Hata kama Ubunge wa Godbless Lema umebatilishwa na Mahakama, Baraza la Madiwani la Manispaa ya Arusha lipo mikononi mwenu na ndio mambo yamevunda.
ReplyDeleteMsitafute pa kutokea, acheni kuendesha mambo Kiswahili!
Si ndio hapa sasa?
Mlishasikia Siasa zaidi kuliko Sayansi?
Utakuja kuona masufuria ya supu ya vichwa vya mbuzi na mtori mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha !
ReplyDeleteUkiuliza kwa nini?
Utajibiwa,,,,''mbeeee chalii hii ndio ile Uhuru kwa mazee Chadema inatoa'' !
sio sababu mnapenda kuwajengea watu na imani zisizokuwa na msingi mara amani mara...... rekebisheni mambo muhimu msitafute umaarufu mwepesi Arusha tu inayotakiwa kuwa hivyo ni miji yote Tanzania hawana sheria tofauti sasa mtashika bango hiyo kitu kama mnyika na udhaifu Dar hipo safi
ReplyDeleteNaona wadau wote hapo juu nadhani hamjui mnachokisema.... fanyeni utafiti kabla ya kukurupuka na maneno ya ovyo ovyo tu.
ReplyDeleteManailaumu Chedema kwa lipi??
Serikali ya manispaa ya Arusha iko 100% chini ya sisiemu!
Chadema iliwafukuza madiwani wake nadhani watano au sita.
Na waliobakia 6 wamegomea kuhudhuria vikao vya manispaa kwa kile wakiitacho kuchaguliwa kusiko kuwa halali kwa meya.
Mbunge ambae pia ni mjumbe wa halmashauri ni Lema ambae kapokonywa manyanga...
Sasa Chadema wako wapi hapo katika kuendesha manispaa ya Arusha?
Quorum ya vikao vyote ni 100% CCM. Maamuzi yanapitishwa kama kawaida bila upinzani wowote wa Chadema. Cahama tawala ndicho kinacho endesha mji wa Arusha muda wote huu.
Uozo uliopo unatokana na uzembe wa chama tawala.
Kilichopo manispaa ya Arusha ni kupata hati chafu toka kwa Auditor General, uwizi wa fedha za uma uliokithiri, uchafu na disorderliness ya kutisha.
Mkurugenzi na vigogo wenzake wanne wako mahakamani wakishutumiwa uwizi.
Jamani sio mnalaumu tu.....fanyeni utafiiti hata mdogo tu.
Soma magazeti na habari za matukio na keep abreast with what is happening in our beloved Tanzania.
Kweli arusha sasa imeharibika vibaka nao wameongezeka sanaa wenyewe wanajiita machalii ar.
ReplyDeleteTafadhali rudisheni hadhi ya arusha.
Zungumzeni hoja ya msingi sasa mambo ya chadema na usafi wapi na wapi.Kama wananchi wamewakataa ni wamekataa .Hapo arusha nawaambia hata kama chadema mkisimamisha jiwe na chama cha mapinduzi tutalipigia jiwe tushachoka na siasa za kitoto.Wote mliochangia naona mmetoka chama cha mafisadi .hamna lolote zaidi ya chuki zisizo na msingi.Arusha hatudanganyiki tena.
ReplyDeleteArusha hamdanganyiki kwa hiyo mmeamua kuishi kwenye uchafu? Mimi nilidhani utakuja na hoja ya msingi kumbe na wewe ni wale wale tu. Hivi Arusha mmelewa nini? Mnadhani hizo siasa mnazoshabikia ndizo zitawapa maendeleo? Mimi ninaloliona Wana wa Arusha wanapoteza muda mwingi kushughulikia siasa na maandamano na wameacha kufanya kazi matokeo yake ni haya.
ReplyDeleteTusiwalaumu Chadema wala CCM bali wanaohusika ni wote! viongozi muda mwingi siasa, vyama muda mwingi siasa, wananchi muda mwingi siasa kazi zitafanyika saa ngapi?
Matokeo yake ndiyo hayo.......
kweli watz hatunazooo ndugu zangu chadema ndio manispaa inayotoa vbali vya biashara au ujenzi mbona hicho chama chenu cha sisiemi kinawabrainwash jamani.. be realist angalieni mkoa wa moshi kwani ndesaaa pesaaa ni ccm??????mbona mji msafiii acheni kujinyima uwezo wa akili zenu kutofautisha usiku na mchanaa come on watz amkeniii hamna ktu kama chadema kua source ya hiii ktu inaendelea arusha CCM ndio chanzoo cha haya yote ngazi zote polisi tra mkoa wilaya manispaaa ni za ccm sasa hawa chadema mnawaonea nini mnataka wafanyaje y hamkucmoplain Lema akiwa madarakani y leo???yakowapi maisha bora ccm na jk alowahaidi hao wauza viatu na nyanya barabarani??yakowapi ndg zangu zko wapi zile ajira tuliadiwaaa...if u don knw nohting heri kukaaa kimyaaaa koz inatia uchungu sio kdg ths z ma homeland na ccm yenu ndo shdaaa hapaa... GOOD DAY WATZ tufanye kazi tuache kelele arusha muwaachie waarushaaa...what happens hia iz mo than wat u seee
ReplyDeleteChadema haiwezi kuchomoka hapo katika 'UOZO NA MARUNDO YA UCHAFU NDANI YA ARUSHA'
ReplyDeleteMtambue ya kuwa BARAZA LA MADIWANI NDIO LINALOHUSIKA NA USIMAMIZI WA JIJI NA WALA MSITAKE SABABU OHHH MBUNGE HATUNA KWA SASA!
Mnafiki tu wewe,eti miaka thelathini si useme tu kama yule mwingine aliyesema Miaka miwili iliyopita arusha ilikua haikaliki,nilidhani kwenye hitimisho ungesema nini kifanyike kumbe ndo unazidi kupandikiza chuki...
ReplyDeleteFukuza madiwani wote tufanye uchaguzi upya, ondoa Meya anayelalamikiwa tufanye uchaguzi upya, fukuza mkurugenzi wa mji wa Arusha, Fukuza Mkuu wa wilaya na Mkuu wa mkoa na teua wapya. Arusha ni Kioo cha nchi, ni Geveva ya Afrika, wameshindwa kazi wanatutia aibu.
ReplyDeleteUKITAKA KUJUA ARUSHA USAFI UNAWEZEKANA TEMBELEA ENEO LA MITAA YA NEW ARUSHA ILE BARABARA YA NJIRO,GYMKANA, NI KUSAFI NA KUNA MPANGILIO. SIJUI KWASABABU WANAISHI WAFANYAKAZI WA UN? BIASHARA ZIPO LAKINI ZIMEPANGILIWA, KUNA SOKO LA MATUNDA ENEO MAALUM. VIONGOZI NI WALE WALE KWANINI ENEO MOJA LA MJI LIWE SAFI MENGINE OVYO? BY THE WAY - WAULIZE WAKAZI WA ARUSHA DAMPO LIKO WAPI? WENGI WAO WANATOA TAKATAKA KWA WAKUSANYAJI HAIJULIKANI ZINATUPWA WAPI. MVUA KIDOGO TU KUNA MITAA HAIINGILIKI. JAMANI ARUSHA IMEHARIBIKA, HILI LIFANYIWE KAZI
ReplyDelete