Mstaiki meya wa manispaa ya Ilala,Jerry Slaa (pili kulia) akipata maelezo toka kwa Bw.Ronny Snellman (kushoto) wa Kampuni ya utengenezaji wa nyama ya Snellman alipotembelea machinjio yao yaliyo katika mji wa Jakobstad.Wengine katika picha ni Afisa biashara Bw. Nicas na Afisa mifugo Bw. Juma mwengine ni Bw. Stefan Jungell wa kampuni ya Kosek ambayo ni kampuni ya maendeleo ya jiji la Kokkola.Halmashauri ya manispaa ya Ilala imeunga udada na jiji la Kokkola Finland ambalo linaisaidia Ilala katika maeneo ya utawala bora,biashara ,usindikaji matunda,usindikaji maziwa,nishati mbadala,utengenezaji wa boti na usafi wa mji.Ujumbe wa msatiki Meya unajumuisha Mhe.Godwin Mbaga ambaye anaratibu ushirikiano huu katika ofisi ya meya,Bw.Sigfid Valentine ambaye ni mkuu wa Idara ya uchumi na mipango wa halmashari na mratibu wa ushirikiano,Bi.Tabu Shaibu afisa uhusiano,Afisa mifugo Juma,Afisa biashara Nicas na Afisa Teknohama Matilda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2012

    UKIRUDI HUKU KWETU HAIWEZEKANI KUFANYA HAYO ULIYOONA MAKE BAJETI HAITOSHI LABDA BAADA YA MIAKA MITANO TENA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2012

    Hawa jamaa wakienda huko sijui huwa ni kwa faida ya nani,sijawahi ona kiongozi karudi na mawazo mapya alopata huko na kuyatekeleza hapa kwetu kwa faida ya watu wake. (ukiacha mzee wa mvua ya Thailand ambae nae aliishia njiani!)

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2012

    Serikali imepitisha sera ya PPP yale yanayoishinda serikali,sekta binafsi iachiwe ifanye.
    Nakuhakikishia kabla ya December tutaweka jiwe la msingi machinjio ya kisasa.
    Umeona beautification kwa kushirikiana na sekta binafsi(mfano round about ya Ngazija) unavyoenda vizuri.
    Nikirudi nazindua mpango mpya wa usafi wa manispaa,ambao sekta binafsi inaplay 60% na 40% halmashari kwa kutumia vifaa vya kisasa ambavyo ingekuwa ndoto serikali kununua.
    Taratibu tatafika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2012

    USIIZISHE KUANGALIA TU, UJE NA MABADILIKO KIDOGO, VINGUNGUTI OYEE!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2012

    nafurahi sana kuona wenzetu wamefikia wapi na sisi tuji kongoje angalau.ila hapo nafikiri uondoke na mawili tu.la usafi na usindikaji wanyama katika hali ya usafi sio zile za kwenye vumbi mabuchani zimekauka.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 15, 2012

    You are wasting our money for these visits how many have you made fpor this year alone i do not see any changes even to things which does not need a penny
    Kariakoo mitaro yote imeziba imejaa matakataka wafagiaji kila siku wanaonekana barabarani wanachofanya hakieleweki, nyie watu mnasahau kwamba hizo positions sio kwa kustarehe ni uwajibikaji , hatuhitaji politics hii sio mara ya kwanza hawa watu wanasafiri ataonyeshwa kila kitu akirudi anaishia kutuwekea picha kwenye mitandao kama hivi we are not interested aende hata Moshi tu akajifunze wamewezaje!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...