Mhe. Naibu Spika Job Ndugai, akitoa mada ya THE STATE OF DEMOCRACY IN AFRICA - THE CASE OF TANZANIA katika Kitivo cha Uongozi katika Utumishi wa Umma (Graduate School of Public Administration) ya Seoul National University nchini Korea. Mhe. Naibu Spika alitoa mada hiyo mbele ya wanafunzi wanaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA) pamoja na wanafunzi wa Korea wasomao katika kitivo hicho.
Mhe. Naibu Spika akiwa na mwenyeji wake Prof. Kim Pong Su ambae ni Mkuu wa Graduate School of Public Administration) katika chuo kikuu cha kitaifa cha Seoul baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa jengo la kitivo hicho.
Mhe. Naibu Spika akizungumza na watumishi wa Bunge wanaosoma nchini Korea Kusini kwa ufadhili wa KOICA, kushoto ni Bi. Lina Kitosi na Nd. Athumani Kwikima.
Mhe. Naibu Spika akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanaofadhiliwa na KOICA pamoja na Makamu Mkuu wa Kitivo cha Graduate School of Public Administration, Prof. Huk-ju Kwon (tatu kulia) ambae pia ni Mkuu wa Kituo cha Maendeleo katika Bara la Asia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Proud of you Lina na Kwikima

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2012

    2015,itabidi na mimi nigombee Ubunge.Haipiti wiki bila kusikia wabunge wako 'mamtoni'usipime.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2012

    Picha tunaiona na tunataka mkirudi nyumbani mtumie mlichofundishwa kuleta maendeleo ya kweli ,tumechoka na blah-blah ,tunaomba muisaidie jamii ya watanzania kama mlivyosaidiwa na serikaliyetu na sio kuanza kujinufaisha kama viongozi waliowengi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...