Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii wa mtandao wa MO BLOG unaotisha kwa sasa, Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo.
MO BLOG: Kitu kingine ambacho MO BLOG ingependa kufahamu ni kuondoka kwako ITV, fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?
MILLARD AYO: Ningependa watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.Kwanza kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona na alipanga ndio maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine nilizo nazo maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na wasingenifuata.ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.
ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter. Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV. Kusoma mahojiano yote Bofya Hapa
ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter. Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV. Kusoma mahojiano yote Bofya Hapa
"BOFYA HAPA" hapabofyeki hapo yaani hamna link hapo.
ReplyDeleteSasa Milard Ayo sawa,
ReplyDeleteKama unatuhakikishia kuwa umeondoka vizuri sehemu yako ya kazi ya zamani,unasema pia utawatangaza vizuri kokote hizo ni DALILI NZURI KUWA huna kinyongo na mtu wala nia mbaya dhidi ya yeyote!, ila hizo TWEET kutoka sehemu yako ya awali ya kazi ndio vipi tena?
Millard ukumbuke Msemo wa Kiswahili ya kuwa 'mtumikie kafiri upete mradi wako'!
ReplyDeleteBepari anapopata ng'ombe wa kukamua maziwa ng'ombe akichomoka hivi Mchungaji wa ng'ombe au mwenywe Bwenyenye kama awali ataweza kulala usingizi?
Millard Ayo umesahau waliokutangulia jinsi walivyoondoka ktk Shirika hilo hilo?
ReplyDelete1.Kundi la Ze Comedy ?
2.Jerry Muro ?
3.Na Wanahabari kibao ?
Milard Ayo,
ReplyDeleteShirika la Kichagga hilo,ulimuuliza mama Razia Khan akueleze?
Jamani punguzeni choko choko. Hana haja ya kukashifu sehemu iliyomfanya kufika hapo alipo ni sehemu ya maisha. Millard anaweza hitaji information muhimu sana kwa future plan yake kutoka management ya ITV,ivi akianza kuongea ovyo itamsaidia nini!!!!! naamini kila shirika lina mapungufu yake na kila mtu anaustarabu wake. Cha msingi ni kusonga mbele na kuchukua mazuri unayojifunza, mabaya unawaachia wahusika. direct Advise always appreciated. millard kuwa strong na choko choko,usiongee,nothing will change from your life. Goodlucky on your way forward.
ReplyDeleteBig up bro.. una God Fearing the most I like from you. Shut your mouth and step forward.
ReplyDelete