Warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha Miss Universe 2012 wakiwa katika picha za pamoja kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar.
Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumsaka Miss Universe Tanzania 2012 litafanyika Ijumaa hii kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai ambaye ndie muandaaji wa Shindano hili hapa nchini amesema le kuwa mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 20 kutoka katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.
Mikoa hiyo ni Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam na kuongeza warembo wote wanaendelea na mazoezi chini ya wakufunzi walioboea katika masuala ya urembo.
“Tunatarajia kuwa na mashindcano bora ili kuweza kumapata mrembo ambaye atatupa sifa katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata mwaka 2007 ambapo alishika nafasi ya saba katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico,” alisema Maria.
Maria aliwataja warembo hao kuwa ni Bahati Chando, Aisha Maulidi, Catherine Mpulule, Cecilia Moses, Consolata Mosha, Devotha Keregese, Doris Mollel, Doreen Mapunda na Edith Tesha.
Wengine ni Getrude Asanterabi, Jescha Tiba, Kundi Mligwa, Lilian Kolimba, Mary Joel, Naomi Joseph, Nyaso Malilo, Neema Mpanda, Susan Manoko, Theodora Msenya na Winfrida Dominic.
Maria alisema kuwa shindano hilo litaanza saa 1.00 usiku kwa warembo hao kupita jukwaani wakiwa katika aina mbalimbali za mavazi kama vile ya ubunifu na lile l;a usiku.
Alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa la urembo yamekamilika na kinachosubiliwa ni siku ya shindano hili kupata mrithi wa Miss Universe anayemaliza muda wake Nelly Kamwelu.
Alifafanua kuwa wameboresha mashindano ya mwaka huu na wanatarajia kuwa na mashindano bora kabisa tofauti na ya miaka ya nyuma.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...