Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kulia) akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Klause Peter Brandes wakisaini mkataba kwa niaba ya Serikali zao wa kuwaruhusu wenza na wategemezi wa wanadiplomasia katika Balozi kuweza kufanya kazi wakiwa katika nchi hizo. Mkataba huo ulisainiwa jana Wizarani.

Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Tanzania na ya Ujerumani zimeweka saini Mkataba ambao utaruhusu wenza na wategemezi wa wafanyakazi katika Balozi kuweza kufanya kazi wakiwa katika nchi hizo.

Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam tarehe 8 Juni, 2012 kati ya Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mhe. Klause Peter Brandes, Balozi wa Ujerumani hapa nchini kwa niaba ya ya Serikali yake.

Katika maelezo yake baada ya kusaini mkataba huo, Bw. Haule alisema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo kutatoa fursa kwa wenza na wategemezi wa wanadiplomasia kufanya kazi wakiwa katika nchi hizo na kuwasaidia kuendeleza taaluma zao na kuongeza kipato katika familia zao.

“Dhumuni kubwa la kusaini mkataba huu leo ni kutoa fursa kwa wenza na wategemezi wa wanadiplomasia wetu katika Balozi kuweza kufanyakazi katika nchi hizi mbili na kwa mantiki hiyo wataweza kuendeleza taaluma zao na pia kuongeza kipato kwa familia zao” alisema Bw. Haule.

Aidha, aliongeza kuwa, Tanzania inakuwa nchi ya pili kwa Afrika kupata fursa hii ya kusaini mkataba na Ujerumani ambapo nchi nyingine ni Zambia. Vile vile, Tanzania imekwisha saini mkataba kama huu na nchi za Marekani na Canada.

Kwa upande wake Balozi Brandes alisema kuwa kusainiwa kwa mkataba huu ni kielelezo cha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani na kwamba ni moja ya mafanikio makubwa ya ushirikiano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    MKATABA HUU HAUFAI KABISA TENA UNA UBAGUZI !Umelenga upande moja tu!

    Mkataba huu ni mbaya sana tena umelenga upande moja tu,upande wa waume au wake wa madipromasia wanaoishi ujerumani !?
    Sheria zilizowabana wenza au wake au waume wa wafanyakazi wa Ubalozi wakigeni nchini Ujerumani ndizo zinazo wabana pia Watalaamu wengine wa kitanzania wanaofanya kazi Ujerumani,wakiwemo maporofesa,waadhiri wa kitanzania nchini ujerumani,pia wanahabari wa Radio kama DEUTCHE WELLE ! kuwa mke au mume wa mtaalamu yeyote mgeni harusiwi kufanya kazi hata ya kusafisha choo nchini ujerumani.
    Sasa Serikali ikiwa inalujua hili na kukubali kutia saini mkataba kama huu ,haikutenda haki! kwa imewaponya njaa wafanyakazi wa balozi za Tanzania na Ujerumani.
    Mkataba lazima utazame masalahi ya watanzania wote sio madipromasia

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Mambo hatua kwa hatua. Huu ni mwanzo. Tutasonga mbele tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Ufafanuzi:
    Mkataba huu unalenga katika kuwaruhusu kufanya kazi pasipo kufungwa na masharti ya ajira kwa watu wasio raia. Watakaofaidika ni wenzi (spouses: mume au mke) na wategemezi (yaani watoto mpaka kufikia umri fulani) wa wanadiplomasia katika nchi hizi, yaani wanadiplomasia wa Ujerumani walio Tanzania au Wanadiplomasia wa Tanzania walio Ujerumani.
    Utaratibu huu ni wa kawaida katika 'diplomatic practice' na nchi huwa zinasaini Makubaliano haya pale zinaporidhika kufanya hivyo. Hivyo una maslahi kwa nchi zote na si upande mmoja tu.
    Kama nilivyoeleza hapo awalim ni kuwa utaratibu huu ni wa kawaida katika diplomatic practice, nchi nyingi duniani hufanya hivyo sio Tanzania tu. "... utazame masalahi ya watanzania wote sio madipromasia..."pengine hili linaweza kujadiliwa katika namna nyingine, wataalamu wa masuala ya ajira wanaweza kulizungumzia, lakini katika nyanjab ya diplomasia hili linawezekana na ni la kawaida.
    Kwa kusaini Mkataba huu 'spouses na dependants' wa wanadiplomasia walio Ujerumani watanufaika kwa kupata ajira na vilevile hapa Tanzania tutanufaika kwa utaalamu wa spouses na dependants wa wanadiploamsia wa Ujerumani.
    Kwa sasa Tanzania ina Makubaliano kama haya na nchi mbalimbali ikiwemo Canada na USA.
    MDAU

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    njoeni UNITED KINGDOM!!Amtokufa njaa nyie..

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2012

    naomba nimfahamishe mwenzetu kuwa hakuelewa mantiki ya mkataba huu, kisheria chini ya mkataba wa vienna kuhusu uhusianao kwa kidiplomasia ni kuwa wenza wa maafisa wa kibalozi popote pale hawaruhusiwi kufanya kazi hadi kuwe na mikataba ya kijamii, kiufupi hata mjerumani akifunga ndoa na mwana diplomasia yeyote hatoruhusiwa kufanya kazi kutokana na kuwa na hadhi ya kidiplomasia kupitia mumewe, mikataba kama hii inaweka ukomo fulani wa hadhi hizi za kidiplomasia ambazo mwenza wa mwana diplomasia anakuwa nazo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2012

    Tatizo ni kuwa watoa maoni wengi,hawaelewi Sheria za kaazi nchini ujerumani,wengi wetu hapa wanazungumuzia vitu vya ki diplomasia bila kuelewa sheria ya ajira ya ujerumani.
    (A) Shera ya ajira ya ujerumani kwa familia za watalaam wote wa kigeni ni hivi,kama mtaalamu uwe diplomasia au daktari,mkunga n.k kama umeenda ujerumani kikazi basi mke au mume wako hana ruhusa ya kufanya kazi,
    ndio maana wataalamu wengi wa IT waliopewa GREEN CARD za ujerumani waondoka ujerumani,maana wake au waume zao wana ujuzi fulani lakini wamejikuta hawana ruhusa ya kufanya kazi.
    (B) Kuna wataalam wa kitanzania nchini Ujerumani wakiwemo,madaktari,mapadre,maprofesa,waadhiri wa elimu ya juu,na wengi ni pale Radio DW Bonn,wake au waume wa wataalamu hao hawana ruhusa ya kufanya kazi,sheria inawafunga,
    SASA KAMA SERIKALI LEO IMETILIANA MKATABA KAMA HUU NA UJERUMANI ni kuwaongezea walio nacho na kuacha familia za wataalamu wengine wafe njaa
    KWA NINI? KABLA YA MKATABA HUU KUTIWA SAHINI WASITAFUTWE WATALAAMU
    WAUZIJUA NCHI ZOTE MBILI

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2012

    JAMANI MIMI NAONA MKATABA HUU UKO SIMPLE SANA NI KWAMBA KAMA BALOZI WA UJERUMANI ANAKUJA HAPA BONGO NA MUME AU MKE BASI YULE AMBAYE HANA KAZI KAMA NI MUME AU MKE ATAWEZA KUFANYA KAZI BILA PINGAMIZI LOLOTE HALI KADHALIKA KWA MTANZANIA BALOZI MKE AU MUME ANAKUWA BALOZI KUFANYA UJERUMANI BILA PINGAMIZI ATAFANYA KAZI AKIWA UJERUMANI JAMBO AMBALO KWA ZAMANI ALIKUWA HARUSIWI KUFANYA KAZI,
    MIMI KWA MAWAZO SIONI PALIPO NA UBAYA WA MKATABA HUU INGEKUWA INAKUBALI HAPA NA INAKATAZA UJERUMANI KWANGU NINGEONA KUNA TATIZO, NAONA KAMA WADAU WENZANGU WAMEELEZA HISTORIA

    MZEE WA KIPEPEO

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2012

    Tuache mizengwe
    kwanini ? pawepo na mizengwe hapa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2012

    Jamani naona watanzana tumezoea kulalamkia maisha na kuchanganya siasa na ukweli,
    Mungu kama kafungua mlango huu wa heri kuwa mke au mume wa diplomasia
    aruhusiwe kufanya kazi,sasa faraja kwetu.
    Sisi watanzania yunaoishi ujerumani ndio tunao zijua tamu na chungu za huku,kwa kweli ugenini hakuna mazoea,
    na kama mungu kafungua mrango huu.
    tufurahie.
    Mdau Ras Makunja

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2012

    Wandugu kwa idadi au asilimia Wana Diplomasia wa Tanzania na familia zao waliopo mfano waliopo huko Ujerumani sio zaidi ya 0.01% (yaani sio zaidi ya 4500 ya Watanzania wote 45 Milioni).

    Kwa maana hiyo Mkataba huu unasainiwa baina ya Tanzania na Ujerumani kwa kuwapa Maslahi watu Tanzania wasiozidi (4,500 tu) !!!

    Huku ikieleweka ya kuwa kwa vigezo vifuatavyo :-

    1.IDADI YA WATU:
    Tanzania na Ujerumani.

    Ujerumani 81,777,000 World Bank report March 2012.

    Tanzania 44,841,000 World Bank Report.

    2.KIWANGO CHA ELIMU NA TAALUMA:
    Ujerumani 87% ya Raia wanazo Taaluma na kazi za taaluma

    Tanzania 5% ya Raia wanazo Taaluma na kazi za taaluma.

    3.UKOSEFU WA AJIRA:(UNEMPLOYMENT RATE)
    Ujerumani 7.4% na Tanzania 10.7%

    Hii ni kwa Maslahi ya Kidiplomasia kwa (Ujerumani fu) na sio kwa maslahi ya Wananchi wengi wa kawaida nchini Tanzania.

    KWA MAANA YA VIGEZO HIVYO VITATU (3) HAPO JUU NA UNDANI WA MKATABA HUU ITANUFAIKA ZAIDI UJERUMANI KULIKO TANZANIA !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...