Mkutano wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola ukiendelea katika hoteli ya Doubletree Hilton jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mhe. Zitto Kabwe(Tanzania), Mhe. Seneta Winnie Nxumalo Magagula(Swaziland),Mhe. Meja Generali Mstaafu Moeng Pheto( Botswana), Mhe. Elijah Okupa(Uganda), Bw. George Seni (Mhasibu Mkuu wa CPA Afrika), Mwenyekiti wa Kikao ni Mhe.Request Muntanga (Zambia). Kutoka kushoto ni Bi. Elsie Simpamba, Afisa wa Sekretarieti ya CPA kutoka Zambia na Ndugu Demetrius Mgalami (Katibu Msaidizi wa Kanda - Tanzania). Mkutano huo umemalizika mwishoni mwa wiki na kupitia taarifa ya hali ya fedha kwa nusu mwaka Jan- June,2012, Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2011. CAG ndio Mkaguzi wa Nje (External Auditor) wa Jumuiya hiyo. Aidha, mengine yaliyojadiliwa ni kupitia maombi ya msaada wa fedha (grants) kwa taasisi mbali mbali zilizochini ya CPA na pia kupokea taarifa za miradi mbali mbali inayotekelezwa na taasisi. Kamati hiyo iliipongeza Sekretarieti ya CPA iliyoko nchini Tanzania kwa kuweka utaratibu mzuri wa kifedha na hivyo kupata hati safi toka kwa CAG na pia kuwasilisha mapendekezo mazuri ya namna ya kuwekeza ada za wanachama ili kupata fedha za kuendeshea miradi mbali mbali ya CPA. CPA Kanda ya Afrika hupata fedha zake kwa kupokea ada za uanachama toka kwa Mabunge ya nchi 19 na mabunge ya majimbo 45 barani Afrika. Fedha hizo husimamiwa na Sekretarieti iliyoko Tanzania.
PICHA ZOTE NA SAIDI YAKUBU,MRATIBU WA PROGRAMU, CPA KANDA YA AFRIKA
Katibu wa Kanda wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA), Dr. Thomas Kashililah ambae pia ni Katibu wa Bunge akipata maelezo toka kwa watendaji wake kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola kilichofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.Chama hicho kina jumla ya wanachama 18,000 duniani ambao ni wabunge walioko katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola. Makao Makuu ya Chama hicho ni London, Uingereza na uendeshaji wake umegawanyika katika Kanda tisa ambapo Bara la Afrika ndio kanda kubwa kuliko zote ikiwa na matawi 63 kati ya 170 ya Jumuiya hiyo. Bunge la Tanzania ndio Makao Makuu ya Jumuiya hiyo kwa Bara la Afrika na Katibu wa Bunge ndio huwa Katibu wa Kanda akisaidiwa na watumishi anaowateua kumsaidia katika majukumu yake. Wengine pichani ni Ndugu George Seni(kulia), Mhasibu Mkuu wa CPA Barani Afrika ambae pia ni Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge. Kushoto ni Nd. Demetrius Mgalami, Katibu Msaidizi wa Kanda ambae pia ni Mkuu wa Itifaki Ofisi ya Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...