Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hamad Rashid Mohamed (kushoto) katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wakati alipowasili katika Ukumbi kwa ajili ya kufuatilia Bajeti ya Serikali ya 2012/13.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka (kushoto) katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wakati alipowasili katika Ukumbi kwa ajili ya kufuatilia Bajeti ya Serikali ya 2012/13.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2012

    Naomba kwa anae elewa mtililiko wa vyeo vya jeshi letu la ulinzi Tanzania,anieleweshe:Nimekuwa nasoma magazeti mbalimbali,na pia ktk runinga na redio cheo cha Brigadia,kikitamkwa "Brigadia Generali.Ninavyo fahamu mimi,Brigadia ni rank yenye Nyota tatu zilizo pangwa ktk umbo la pembe tatu na Ngao,kisha inafuata rank ya Meja Generali,ambayo ni Ngao pamoja na Mkasi(alama ya bunduki na upanga),kisha inafuata rank hiyo hapo juu ktk picha ya mnadhimu mkuu wa jeshi letu,yaani ni Ngao na Nyota moja pamoja na Mkasi,na kwa jeshi letu,cheo cha juu kabisa ni Generali,ambacho rank yake ni Ngao na Nyota Mbili pamoja na Mkasi.Kumbe kuanzia Meja Generali,tunaona rank hizo zina ambatana na Mkasi.Sasa inakuwaje Brigadia ambacho hakuna Mkasi,na badala yake kuna Ngao,aitwe Brigedia Generali?Naomba kwa anayefahamu anipe ufafanuzi wa hilo.Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2012

    Hiki cheo cha Brig-Gen kimekuja siku hizi. Ndio maana Kenya, Uganda na Uingereza bado wanaitwa Brigadia basi!.
    Brigadia licha ya kuwa na triangle na ngao ni Jenerali wa nyota moja.
    Meja jenerali ni wa nyota mbili, na Luteni Jenerali, kama alivyo shimbo ni Jenerali wa nyota tatu, na Jenerali ni jenerali wa Nyota Nne kama alivyo Mwamunyange.
    Marekani wao wanatumia nyota. brig-Gen. anakuwa amavalia nyota moja kwenye kofia na mabegani, hadi nyota nne.

    Rwanda na afrika ya Kusini wao wanatumia mkasi na ngao ila katikati ya mkasi na ngao wanaweka hizo nyota. Mfano Brigadia general wa Rwanda ana Mkasi, nyota na ngao, Jenerali kamili ana Mkasi, nyota nne na Ngao.

    Hapa shimbo ana mkasi, ngao na nyota angekuwa Kenya an Uingereza, alivyovaa hivi angesomeka jenerali Kamili, yaani wa nyota nne, angekuwa Rwanda angesomeka Brigadia jenerali.

    Mi nadhani Mfumo wa Uingereza ndio mfano wa kutumia kwani tumeiga kwao.
    Angalia UK military rank insginia kwenye google.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...