Habari ya kazi kaka Michuzi,

Mimi naitwa ISAYA CHAULAnakuomba uniwekee ujumbe huu ili wana Blog yetu pendwa waweze kunisaidia.

Tarehe 29 May 2012 nimepotelewa na Cheti cha kuhitimu elimu yangu ya chuo katika mazingira ya kutatanisha,Cheti hicho kilikuwa kikisafirishwa kwa njia ya Bus liitwalo Dar Express Kutoka Arusha Kwenda Dar es Salaam.

Ninawaomba wana Blog hii pendwa endapo wakikiona cheti hicho kilichotolewa mwaka 2011 na Chuo Cha Uhasibu Arusha (Institute of Accountancy Arusha).

Naitaji msaada wenu wadau,Natanguliza shukrani zangu.
kwa mawasiliano
+255757300022 au +255715300027
Bahasha iliyokua na cheti iliandikwa Isaya Chaula (Dar), Andrew Mwakaje (Arusha)
Ahsanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2012

    Kama ulisafirisha na Dar Express, hao Dar express wana leseni ya Courier au ulisafirisha kienyeji tu.
    Kama wamkupatia risiti inabidi huyo msafirishaji awe mdaiwa na anatakiwa akupe maelezo yatakayokusaidia. msitume vitu kama hivi hovyohovyo hizo ndio kazi za Posta kama hamjui.
    Pole.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2012

    pole kwa hilo lakini kwa kweli hainiingii akilini.kimepotelea kwenye gari au ofisini baada ya kufika?.wafanyakazi wa dar express ndio msaada wako wa kwanza kufanikisha hilo maana wanajua walikokiweka.

    ni mtazamo tu

    hsm

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2012

    Baba Isaya,

    1.Bandugu sasa tunajua Dar EXPESS ni wabebaji wa kulipwa sasa kama mzigo wako uliusajili na uliulipia kwao kwa nini usiwawajibishe wao?

    2.Kama alikabidhiwa mtu (bahasha haiwezi kuwa peke yake bila mbebaji) kwa nini usianzie kake huyo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    Mazingira ya kutatanisha!!! Fafanua ili tukupe ushauri wa kisheria

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2012

    Ushauri wangu si jambo zuri kusafirisha vyeti or any important docs kwa bus. Kuna EMS, DHL etc. Wamekiuza hao! Mdogo wangu alikuta mtu anatumia cheti chake kilichopotea!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...