JINA LANGU NINAITWA AGUSTINO ANDREW, MWALIMU WA CHUO CHA UALIMU NACHINGWEA MKOANI LINDI.
NIMEIBIWA LAPTOP PAMOJA NA VYETI VYANGU VYA TAALUMA KAMA CHETI CHA KIDATO CHA NNE, SITA, TRASCRIPT RESULTS NA CHETI CHA KUZALIWA NIKIWA FRISHA SALOON MAENEO YA TABATA CHANG’OMBE
TAFADHALI NAOMBA YEYOTE ATAKAEVIONA VYETI HIVYO ANITUMIE KWA ANUANI IFUATAYO:
AGUSTINO ANDREW,
C/O VERONICA KAZIMOTO,
S.L.P 76079,
DAR ES SALAAM.
MOB. NO: 0719 – 876 433 AU
0753 – 986 541.
Ulikuwa na hiyo laptop ndani ya hiyo saloon au uliiacha nje kwenye gari?
ReplyDeleteWAKUJA KALIZWA HUYOOOOOO.
ReplyDeleteDalili ya utoro Kazini!
ReplyDeleteSasa Mwalimu Augustino Andrew hilo rundo la nyaraka nyeti kama hizo kuwepo Dar Es Salaam wakati kituo chako cha kazi ni Nachingwea Lindi, OK inawezekana ni wakati wa Likizo lakini kwa nini ubebe vitu vyote hivyo safarini Dar?
Vitu vingine unaweza kuvipata hata kwa kurejesha au kununua, lakini vitu vinavyoitwa Cheti cha Form 4 na Form 6 kamwe huwezi kupata vingine utabaki unatumia Results Slips kutokana na Policy mbovu za Baraza la Mitihani la Tanzania kuhusu Vyeti!
Unaweza kupoteza vyeti vya Elimu ya Sekondari vya CAMBRIDGE au OXFORD vya Uingereza ukaagiza vingine ukatumiwa lakini vya hili Baraza letu ndio imekula kwako!
POLE SANA!!!
Nilijaribu kuuliza wahusika wa frisha wakaniambia huyu jamaa hakuwa salon, alikuwa yuko bar ambayo iko pembeni tu ya salon hiyo na gari aliipaki sehemu iliyo kama mita 50 kutoka alipo ila sehemu amabayo haiko chini ya uangalizi wa mlinzi wa Frisha.Niliingia shaka baada ya taarifa hizi maana na mimi ni mteja katika salon hiyo, hivyo nilitaka kujua hizi tabia za wizi wanazishughulikiaje, jibu ni kwamba hawahusiki. Pole mdau ila tangaza clouds kipindi cha jahazi maana glob kama hii twasoma wachache.
ReplyDelete