Kaka issa pole na kazi ya ujenzi wa taifa kupitia blogu yetu ya jamii!!
Ninaomba msaada wa kimawazo kwa wadau wote ndani na nje ya nchi ya Tanzania!
Kaka issa,mimi ni Kijana wa kiume nina umri wa miaka 31 ya kuzaliwa.Nina elimu ya ngazi ya uzamili[digirii 2].Sijaoa na wala sina mtoto!
Nina mpenzi wangu[miaka 23] ambaye nilimshirikisha kwa nia njema na mapenzi ya dhati kabisa kuwa ninamuomba awe mke wangu wa ndoa ndani ya mwaka 1 ujao[akakubali],tumekuwa wapenzi ndani ya miezi 3 na wala hatujafanya tendo la ndoa.
Mpenzi wangu huyu ni muelewa na ni msomi,kwa sasa anamalizia digirii yake ya kwanza chuo kimoja hapa nyumbani!
Kaka issa,mapenzi ni jambo linalohitaji kila aina ya uelewa na control ili kuliimalisha na kujenga misingi na nguzo imara hadi kuja kuwa na familia bora.
Sasa basi,kwa muda wote niliopendana na mpenzi wangu huyu,tumekuwa na mawasiliano ya karibu sana,zaidi ya kuchati na kupigiana simu.
kusema kweli mpenzi wangu huyu ninampenda na yeye ananipenda.
Kisa na mkasa umeanza pale ambapo nilimuomba password ya e-mail yake na face book.Kimsingi alinipa na akaniuliza unavitaka vya nini?
Kwa kuwa nina malengo mazuri juu yake,sikumwambia ni kwa nini ninavitaka!!
Baada ya kunipatia,nilichokifanya nilimnyima access ya facebook na email.
Cha kushangaza,amenitangazia kuvunja urafiki na mapenzi kwa kusema kuwa uamuzi atakao ufanya nisimulaumu!!!akanipa condition ya kumpatia hizo password ndani ya masaa 24.
Wadau ninaomba ushauri! wa kweli na wa uhakika.
Ushauri ninaouomba je mimi nifanyeje????
Mdau wa kufa na kuzikana blogu ya jamii!!
kaka issa mail weka kapuni!!tafadhali!!


Wewe unaonyesha hata ktk ndoa utakuwa dictator, kama amekubali kukupa password zake umefunga ya nini. kwani huyo ni mtoto mdogo? Umemfanya mjinga. Watu wengine mnapotezaga vitu vizuri kwa kutotumia busara. Yumkini kwa kuongea nae tu angeweza kuwa ameacha fb kwa kukupenda tu, email unamfungia ya nini? Hatakuwa na mawasiliano hata ya kiofisi? Apologize ujipange upya,hii ni karne nyingine. Ongea na mwanamke sio kumpelekesha.
ReplyDeleteMapenzi yanajengwa na misingi 3, kuaminiana, kuheshimiana na kupendana sasa naona kuna kilicho kosekana katika mahusiano yenu, ili muweze kuelewana tafuta ni kipi kati ya vitatu nilivyo vitaja kimekosekana, halafu ndio mtaweza kuendelea hatua zinazofuatia.
ReplyDeleteKingine jaribu kumpa mpenzi wako madaraka ya kufanya mambo ayatakayo usiwe unataka kumdhibiti kwa kila kitu kumbuka sio mwanao bali ni mpenzi wako, avoiding being a control free and sometime try to give each other space.
kwanini umnyime access to her mails na facebook? zinauhusiano gani na mahusiano yenu?
ReplyDeleteShe is actually more civilized and educated than you are because firstly, she gave you her password bila kusita na ukaulizwa ni zaninii?
U are 31, tumia busara za kiutu uzima...kumnyima password ya emails zake haisaidii wala kukuguarantee chochote! Jiamini!
Kwa nini ulimnyima access ya email na facebook yake. Tena alikuheshimu sana kukupa hizo password. Kila mtu anahitaji privacy hata kama mme na mke.Ina maana you don't trust her. Mimi sijafurahishwa kabisa na kitendo hicho ulichomfanyia. Unasema anasoma, hivi wewe huelewi umuhimu wa email/facebook na social netwworking katika karne hii. Huwezi kujua ni taarifa ngani anazozikosa. mimi naona ni sawa nakumnyanga'nya mtu simu yake. Kitendo ulichomfanyia ni kibaya na ingekuwa mimi nisingekuelewa kabisa kabisa!!!!
ReplyDeleteAisee pole ndugu yangu, kweli mapenzi ni mlima mrefu. Kuna kupanda na kushuka. Kweli ulikuwa unaweza kuangalia facebook yake kabla hujamuomba password? Maana najua mtu anaweza kumuangalia mtu ambaye hajamblock pale facebook. Kama ulikuwa na access ya kuiona fb yake sasa kwanini unataka hata password yake? Basi itafika siku utataka akupe access ya account yake ya benki na utataka kumkomoa kama akikufanyia jambo ambalo hulipendi huko mbeleni mkioana. Yeye ni mtu mzima kwahiyo kwanini unamfanyia hivyo? Mapenzi ya kidikteta hayadumu ktk zama tunazoishi sasa. Kwa definition yangu naona umeonyesha kutomrespect. Inabidi umuamini na kumheshimu mchumba wako, na kama atakuwa na mambo ya vuvuzela na ikawa ndio sababu mkaachana. Basi labda ndio ikawa heri kwako maana labda mungu anataka kukukinga na mabalaa mengi zaidi na labda utampata anayekufaa zaidi. Mapenzi ya kuforce na yenye wivu wa kupindukia huwa yanaishia pabaya sana. Tuambie hasa nini kilitokea mpaka ukataka umnyime access ya hiyo email na fb yake. Sioni logic ya wewe kudai access ya fb yake na sio lazima akupe na hata kwenye katiba na vitabu vya dini na katiba ya nchi hawajaandika akupe fb access.
ReplyDeleteMdau Bremen
Kikiliza ndugu yangu wewe ni mwanaume lakini ukumbuke ndoa salama ni ya kuoana sio wewe kuoa.
ReplyDeleteKama unaamini kweli mnapendana basi kuwa wazi na nenosiri hizo ili nawe umfaham basi naye akufahamu.kama unaona kuna vitu ambavyo hatakiwi kuviona wewe ni mwanaume diliti hivyo unavyotaka asivifahamu.
Grow up buddy!!! She should not have given you her passwords to start with.Have you ever heard of privacy? why would you want her passwords anyway? You are a control freak, this girl must run away from you as fast as her legs could carry her.
ReplyDeleteDr Gangwe.Bitozi
Wewe ulianza vizuri kwa kutueleza kiwango kizuri cha elimu uliyonayo, lakini inaonyesha hii elimu haijakusaidia.
ReplyDeletepersonal e-mail access ni confidential issues, so iweje unataka akupatie. Mbona yeye hajakuomba zako. Alafu mbaya zaidi unakwemba ku-block access yake. Huu ni ushamba sana, acha ushamba aisee.
Kwa mwenendo huu ulionao within 3 months unaanza tabia hizi, je mkioana itakuwaje? Si utakuwa unamnusa harufu aliyoondoka nayo asubuhi ili ulinganishe na aliyorudi nayo jioni.
Naona elimu uliyonayo haijakusaidia, unahitaji elimu zaidi kuhusu mahusiano na mapenzi.
Kwa mwenendo huu hutakaa upate mke unayemtarajia
Mimi naona kama umeandika UPUUZI tu! Labda TUKUTUKANE lakini hamna cha kuchangia. Alikupa password na email, kwa hiyo ukabadili password ili uendelee kuimiliki wewe, na kwa makusudi gani? Au unamanisha nini? Maana haueleweki vizuri. Ulivyoandika na kiwango cha ELIMU ulichokitaja havifanani
ReplyDeleteSasa unaleta ubabe,mtu kakupa password unamnyima access wakatie mail na Fb ni vyake.Angekuomba password zako halafu akunyime access ungefanyaje?
ReplyDeletekwa kweli mm binafsi sijaona sababu zote za msingi za kumnyima access ya e-mail na facebook, especially e-mail, kuna sababu gani ya msingi? mm nakushauri ni haki yake, kwani anauwezo wa kufungua kwa address nyingine, but amekuwa mtiifu na akakupa kwa nia njema, dont break her heart
ReplyDeletePole kaka kwa yaliyokusibu
ReplyDeletenaona hukutumia ustaarabu maana kuomba password ya mtu ila maana humuamini.
Kama ni wako ni wako tu
Pamoja na kuwa wapenzi, lakini personal privacies ziheshimiwe. Sidhani kama ulikuwa sahihi kuchukua password zake na kumzuia kutumia facebook na kusoma e-mails. Sana sana ungemshauri aachane na wengine aelekeze mawazo yake kwako. Ulichofanya sio sahihi. Je, wewe uko tayari kumpa password zako? uko tayari akuzuie usifanye mawasiliano.
ReplyDeleteMapenzi hujengwana kuaminiana. Umeshaonyesha dalili za wivu mkubwa sana na atakapokuwa mkeo si ajabu ukafanya mambo ya ajabu pindi utakapogundua kuna dalili za mahusiano mengine. Du...mkae pamoja muyamalize na upunguze wife ndugu.
Una wivu wa kijinga mdogo wangu,unakaba hadi penati.
ReplyDeletetwo words. control freak
ReplyDeleteWewe inaonyesha una wivu na humwamini huyo mpenzi wako. Wewe kuomba password zake na kuzibadilisha bila idhini yake na kumnyima hiyo passwords mpya hiyo inonyeha wewe mwenyewe huna nia njema kwa huyo mpenzi wako. Na mimi namuunga mkono 100% kwa hatua alioichukua na kama anataka ushauri wangu ni bora atafute mchumba mwingine kuliko kukaa na wewe mtu ambaye itakua hamuaminiani. Mtu kama ulikua na malengo mazuri juu yake na nia jema kama ulivyosema basi ni lazima umueleze na umfahamishe kwa nini umebadilisha na kwanini hutaki kuumpa hizo new password ili na yeye apate kukuelewa na kufahamiana.
ReplyDeleteNo wonder your marriages never last. her Facebook is her own private thing. What right do you have to take her password and DENY her access to her own ACCOUNT??
ReplyDeleteHio ni sawa nakumuuliza mpenzi wako for her account details and bank card halafu you refuse kumrudishia. Its crazy. This draconian behaviour has to stop. Its so disgusting.
If you don't trust your wife to be with a Facebook account, then you you dont deserve to marry her.
What happened to freedom and presonal space?? Why dont you respect that??
Your own INSECURITIES are causing you to suspect ur wife to be cheating if at all she is. Its very clear that you are the isecure one. I think its because you have not made love to her is what is upsetting you.
Ndoa za siku hizi za kibongo ndo watu wanacheat sana coz partners dont trust each other. Mara simu unampigia... 'Hallo... UKO WAPI??" Absolute disgusting behaviour.
I wish she gave you 4 hours instead of 4 days.
You dont know a good thing until its gone. Have a stress free weekend.
'Koprah StressFree'
umechemsha
ReplyDeleteWewe kweli hufai kumuoa huyo mwanamke?umemuomba password kakupa hlf una block acceess ya account yake?we mzima kweli?na kama nia yako ni kumchunguza huyo mwanamke njia uliyoitumia sio sasa,na inaonyesha yeye anajiamini ndio maana akakupa passowrd yake.km una wasiwasi nae muache binti wa watu awe huru.hujaoa unakua na za kidingi je ukimuoa si utamfanya kama mtumwa wako.
ReplyDeleteUmeyatafuta mwenyewe kwanini utake password ya mtu wakati hicho ni kitu cha mtu binafsi. Hapo ulianza mapema mno kutaka vitu vya binafsi kwa mwenzako yaani ndani ya miezi 3 unataka kumtawala. Je wewe unavikatalia vya nini si nawe ungempa. Una matatizo wewe!
ReplyDeleteyou are stupid.
ReplyDeleteKama nimalaya malaya tu mpe password yake haraka kwani yeye alichukua yako akakufungia!! unaonekana unataka kushurutisha kabla hata ya ndoa ulitakwa uzungumze nae kwa upendo na kwamba pengine face book huipendelei mngejadiliana na si kutumia udiktata.
WE JAMAA INAONEKANA UMEANZA MAPENZI UKUBWANI...ACHA USHAMBA WEWE, KAMA KAKUPENDA KAKUPENDA TUU HAUNA HAJA YA KUMCHUNGA MPAKA UFUNGE ACCOUNT YAKE YA FACEBOOK, YANI HAPO HAJAWA MKEO WA NDOA UNAKABA IVO!!!!!!ZINDUKA WEWE...WE LIVE IN IPOD GENERATION NOW.....CYO CASSETE TENA
ReplyDeleteWewe kaka:
ReplyDelete1: Mbona huyo binti umempita sana kiumri? kwa nini usitafute wa miaka 26 hivi? wewe umejipatia uzoefu sasa unataka kum control yeye? wewe inaonekana unataka easy going person!!
2: Ulimwengu wote unataka uwe na control ya taarifa na conectivity kupitia computer wewe una m block? ina maana wewe huna email wala network yoyote? kumbuka huyo ni binti wa kileo na kwa hilo huna hoja na hiyo masters yako naitilia shaka!
3: Kwani una mashaka gani wewe? si ulimkuta ameji connect tayari na mtandao? angekuwa anasaka wanaume humo hata wewe usingempata jinsi ninavyokuona bonge la mshamba maana kwenye net kuna wakali sana zaidi yako. sasa kwani wewe ulimpata kwenye net?
4: Wanaume kama wewe hukawii kumuonea wivu asisome hata digrii ya pili. kusoma siku hizi ni mtandao eti
5: Ahsante kwa kuni boa sana nawatakia muachane salama kwani wewe una short mind utatuharibia msichana wetu hovyo sana katafute kijijini kwani hata kuwasha redio tu hawajui.
Hi, Huyo hakuna na nia nzuri kwako maana si mwaminifu kwa nini afike passward na kama ukimfungia kwa nini ahamaki kiasi cha kutishia amani.
ReplyDeleteHapo kaka hujapata kabisa.
Ukitaka kuishi kwa amani na upendo kuwa na imani na demu wako iwe facebook au email upaswi kumyima haki yake ya kuchat wala kuwasiliana na maisha yake,unapomyima access ya mail yake wewe hapo umevuka mipaka tena ur luck huko africa ukiwa ulaya wewe ni utaweza shitakiwa kwa kuchukua vitu sio vyako na hapo unaitwa mwizi wa mambo ya mtu iwe mkeo au rafiki ,upaswi kuchukua na kumyima mtu access,huo ni mtazamo wangu na kwa kifupi umepoteza imani kwa mpenzi wako na kujenga tena hiyo inataka moyo sana iwe anakupenda na aweze kukusamehe,mjomba na digrii mbili mambo haya madogo unashindwa?umekalia kuti kavu.
ReplyDeleteBy
Duke wa kimbiji
Pole sana kaka,inaonekana pamoja na shahada ya uzamili bado hujaelimika;si ajabu lakini kwani mapenzi hayasomewi.
ReplyDeleteMume na mke (hatua ambayo hamjaifikia) huwa ni watu wawili huru. Mkeo ana haki ya kuwa na maisha yake,si mtumwa wako. Kukupatia password zake ilikuwa ni ishara ya kukuamini na kukuheshimu,alikua na haki ya kukataa. Kuna haki ya usiri kaka,inalindwa na katiba ya nchi. Sasa ulichokifanya wewe,kumzibia facebook sijui na nini ni kosa kubwa sana,na akiamua kufuatilia unaweza pata matatizo makubwa tu. Hivyo ushauri wangu kwako ni kwamba 1. Mrudishie mawasiliano yake haraka sana na umwombe radhi, 2. Kama unampenda unatakiwa kumwamini na kumheshimu, 3. Jiamini katika mapenzi, 4.Mapenzi hayalazimishwi. Mwisho jiulizi, Je yeye angekufungia wewe hizo facebook zenu ungelichukuliaje? Au unajidanganya kwamba una haki juu yake kwa vile yeye ni mwanamke? UMETIA AIBU!
Wewe ni contro freak. Mimi nimeolewa mwaka wa nane huu; mume wangu ana password ya e mail yangu na mimi nina yake; tulipeana vipi sikumbuki; we were (and still are) crazy in love.
ReplyDeleteNimemuona mchumba wako mstaharabu na hana cha kukuficha baada ya kukubali kukupa password zake; japo sijuhi na hujasema kama umempa zako.
Nakushangaa ni kwa nini unahijack access yake kwenye mitandao ya jamii na e mail (lord Have Mercy). Ukimuoa si utamfungia ndani
Hata mimi huyo angekuwa ndugu yangu ningemwambia akimbie na asiangalie nyuma. Mwanaume gani wewe unaogopa hata kivuli???
mabwepande !
ReplyDeleteWewe ulifanya makosa makubwa sana kumuomba mwenzako hizo password,kwani unafikiri mtu ukimuomba p.word ndo utakuwa unamdhibiti kama anataka kufanya mambo yake?
ReplyDeletemimi mwenyewe sipendi mtu kuniomba password yangu,na hasa kama hajakuoa,,ungekuwa umeisha muoa sawa,,hayo mambo yamewatokea wengi,,hasa vijana wenye umri kama huwa mnapenda kuomba p.word....Mimi kidogo nimuache mchumba wangu alivyoniomba pw...
Nakushauri ukamuombe samahani yaishe maana ulimbore kwa kitendo hicho
mdau UK
kaka pamoja na uelewa wangu mdogo lakini najua kuwa hivyo vitu na personal! hicho unachokifanya ni controlling freak unaingilia uhuru banafsi wa binadamu mwenzako kwa kisingizio cha uchumba? not fair na hapo ni wachumba ukimuoa si utamkataza hata kutoka nje wewe? ningekua mie usingeniona tena sipendi kabisa aina ya wanaume kama wewe.
ReplyDeleteWewe mchikozi! Kwa nini umemuomba access ya FB na email zake? Email ni kitu personal, wewe unaweza kufungua ya kwako. FB hivyohivyo - fungua ya kwako, omba urafiki naye na muendelee kama kawa!
ReplyDeleteKama mpo kwenye mapenzi kuna vitu ambavyo mtaweza kufungua kwa pamoja au kuwa navyo kwa pamoja. Bank account, hati za kiwanja/nyumba, gari, shamba etc lakini email na FB?
Halafu hii barua ya kweli hii au fwamba......?????
sasa kwanini umnyime kutumia facebook na email wakati umemkuta nazo na vile vile wewe mwenyewe nahuakika unatumia facebook na email, inaonyesha kwamba humuamini hapo hamta weza kutumu kabisaa ina bidi mbadilishane usiangalie upande wako tuu kama yeye kakupa password zake na wewe basi mpe za kwako..
ReplyDeleteyaani umenishangaza sana ndio kwanza mna miezi 3 umeshaanza kum control je ukimuoa si ndio itakuwa balaa?? wacha ushamba ukitaka mdumu ktk mapenzi yenu basi jenga uaminifuu yaani muamini inaonekana unawasi wasi sana
wacha ufala na utindiga hiyo ni kumnyanyasa na utaachwa kama vile umesimama...wacha unyanyasaji unafikiri ukichukua password ndio hawezi kuku cheat?? mtu akitaka kuku cheat anaweza at any time
Usiwe fala wewe elimika haki sawa kwa wote....
Mdauu.....
Wewe una matatizo, why umnyime pin ya mail na fb yake, wewe unadhani kwa kumnyima atashindwa kufanya hicho ulichodhani unamzuia? Mbona huja mnyan'ganya na simu ili asi'text?
ReplyDeleteKwa kumpenda kwako siyo garantii kuwa utakuwa naye kama mkeo, kwani wengi hudanganya madada na kuwaacha solemba bila kujali muda na watu aliowapoteza kwa ahadi hewa. Wewe ulishampaga pin za email na fb? Angekaa nazo ungejisikiaje? Je, ni wote unaowasiliana nao ktk mitandao hiyo ni wapenzi wako?
Ushauri wangu ni kuwa, kamwombe msamaha kwa upumbavu uliomfanyia. Kama una nia ya kuwa naye mkeo, mfanye ajielewe hivyo huku mkimwomba mungu. Mwelimishe mabaya yatokanayo na mitandao ya kijamii (FB) ili mwenyewe aamue kuiacha.... beside, binadamu hachungwi.
Una muda woote huo na yeye.... halafu unaleta mapenzi ya akina kemcho ya msg na simu, huna ulichofanya kisha unakuja hapa unadai mnapendana sana ....tehe teh teh...! Hujui unataka nini...!!!
Kibanga Msese
We jinga kweli unajiita umesoma na una mambo ya kijinga hivi na ya kizamani, wanaume kutaka kuwatawala wake zao.. maambo ya kaaale unaishi dunia ipi ww?
ReplyDeleteUmmemnyima access kwenye fb na email yake ili iweje, lol kama ningekuwa mm ndo sababu kubwa ya kukuacha, huna uaminifu, na usikute we ndo kicheche unadhani na mwenzio hivyo hivyo.. mtoto wa watu ana busara kakupa passwords bila kusita kukudhihirishia kwamba mwaminifu..
Lol tafuta jinga mwenzio mwachie huyo aolewe na mtu mwenye sifa kama zake anayejua kwamba mapenzi yanaendana na kuaminiana.
Usitupotezee muda na kuuliza ujinga humu ebo!!
Utakuwa una matatizo wewe..mwenyewe amekupa password zake kwa nia njema wewe umejidai kidume kum-block mwenye mali yake..unaakili kweli wewe??wacha ushamba wako..sasa ndio unakosa mwali huyo..una masters lakini haikusaidii kupambanua maisha..shwain...utaishia kupiga kono mpaka uzeeke..huwezi tena pewa vyombo wewe..
ReplyDeleteMsomi wa Digrii Mbili (2).
ReplyDelete1.Wewe ni Msomi kwa Shahada mbili.
2.Wewe ni mtu mzima sasa unayajua maisha vizuri.
3.Elewa Ujenzi wa Mapenzi unakutegemea wewe na mwenzio, kwa kuwa 'no one is perfect' mnatakiwa mjitengeneze na mapema zaidi kwa kujengana.
4.Elewa wazi ya kuwa huyo Mwanamke hukumkuta chekechea au kutoka kwa wazazi wake hivyo huwezi kukataa ukweli ya kuwa hakuwa anafahamiana na watu wengine hapo kabla ya wewe(ikiwezekana wanaume tena wengine wenye sifa zaidi yako)+(vivyo hivyo hata wewe mwenyewe inawezekana umeshawahi kuwa na wengine hapo kabla), pia huwezi kukataa ktk umri wake yeye na wewe itakuwa ndio mara ya kwanza kuwa na mahusiano.
5.Kuchukua vidukuzi nyeti kama passowrd za e-mail na contact za simu sio njia za kumfuatilia mtu ama kumdhibiti mtu kimapenzi.
6.Mahusiano yenu yanajengeka na kuimarika kwa vile mtakavyo wekana wazi kuhusu undani wake na hivyo mkajengana ili kuleta mahusiano hadi kufikia Ndoa yenye mafanikio.
7.HIVYO BASI UAMUZI WAKO WA KUMTAKA MPENZI WAKO AKUPE PASSWORD ZA E-MAIL NA FACEBOOK NI KUMWINGILIA KTK UHURU BINAFSI 'PRIVACE' KWA KIWANGO CHA UMRI NA ELIMU YAKO, NA UMRI WA MAHUSIANO WA MIAKA MITATU (3) HUKUTAKIWA UKURUPUKIE HUKO KWA SASA BALI ULITAKIWA UMPE MUDA ILI MUWEZE KUJENGANA KWANZA.
INAONEKANA WEWE UNAMSHUKU SANA MWENZIO, KWA NINI?
JE KWA NINI YEYE (MWANAMKE) HAJAKUTAKA WEWE UMPE YEYE ZA KWAKO?
Mwanaume Msomi kwa nini kama wewe unataka password na simu ya mwenzio (Mwanamke)?.
ReplyDeleteJe wewe uko tayari kutoa za kwako, kwa nini usiombe za kwake na wewe muda huohuo utoe za kwako?.
Mpeane ingawa wewe unaependekeza suala hilo utakuwa na nafasi zaidi inawezekana utakuwa umesha futa ushahidi (wa mahusiano mabaya na watu wengine).
Kwa nini unamshuku sana mwenzio?
ha ha ha hapo tu bado haujao, ukimweka ndani huyo bibie si utashika hadi funguo ya kabati lake la chupi !!, ji amini mpe uhuru wake.
ReplyDeleteNijambo lakushangaza sana kuona umeingilia mawasiliano na mpenzi wako ingawa hukuweka wazi nikwanini umeamua kufanya hivyo zaidi ya wewe kusema eti kwania nzuri nionavyo mimi yeye ndiye
ReplyDeleteanakupenda zaidi kumbuka ulichokifanya nikuingilia uhuru wa mtu bila ridhaa yake tena ningetegemea awe amekuacha zamani sana
sasa wewe na huyo wote jinga,wewe unaweza vipi mnyima access na yeye kashindwa vipi ku reset password???
ReplyDeleteWe bwege kweli, mapenzi ya kuombana password za facebook na email ndio mapenzi gani? huko ni kuingilia uhuru binafsi wa mtu.
ReplyDeleteKama humuamini, muache yaishe. Mwone, ungekuwa karibu ningekutia makwenzi
Mkuu hata mimi namuunga mkono huyo dada!
ReplyDeleteHiyo mambo ya kuchukua passwords za mpz wako ni mambo ya zamani kweli yaan hlf hayalingani na elimu yako kam ulivyosema!
Ukitaka uwe na mapenz ya amani na furaha muamini mpz wako na wala usijaribu kum'badilisha kwa namna yoyote ila maana hivyo ndivyo ulivyomkuta na ukijaribu kum'badilisha believe me atakua anapretend sana an u knw what might come out of that!
umefanya kosa sana kuchukua password zake na hutakiwi kumnyima. kimsingi hata mke na mme bado kuna mambo yana mipaka yake. acha wivu utakufaa na wivu. kwanza unauhakika gani kama ana hiyo e-mail moja tu? mjini hapa
ReplyDeleteWewe Mwanaume unaonekana wewe ndio dhaifu zaidi kuliko mwenzio ambaye muda wote wa mahusiano yenu amekuwa akikuamini hajakutilia shaka wala kukujengea hofu.
ReplyDeleteMara zote wewe unayemshuku mwenzio na unayepedekeza mambo hayo inawezekana wewe Mwanaume ukawa ndio mchafu zaidi kuliko yeye!
1.Kiumri wewe ni mkubwa hivyo umepitia vingi.
2.Umekaa zaidi maisha ya mchanganyiko kama Vyuoni ulimopitia.
3.Kumbuka mahusiano thabiti yanategemea kujengana na kutengenezana kwa kurekebishana makosa pande zote mbili LIKIWEMO HILO UNALILITILIA SHAKA ZA YEYE KUHUSIANA NA WENGINEO!
UTASUMBUKA SANA NA UTAJIKUTA UTASHINDWA HATA KUMPATA WA KUMUOA KAMA UTAKUWA UNAFUATLIIA SANA MAMBO YA WENZIO KWA KARIBU NAMNA HIYO.
WEWE UMESOMA UNATAKIWA UYACHUKULIE MAMBO KWA MTAZAMO WA JUU TOFAUTI NA MTU ASIYESOMA!
NDIO NINYI UNAEZA KUVUNJA MAHUSIANO KWA MISS CALL YA NAMBA USIYOIFAHAMU ETI HUYU ALIYEKUWA ANAKUPIGIA HALAFU AKAKATA NI NANI?
KUMBE INAWEZA KUWA NI WRONG NUMBER MTU ALIKUWA ANAPIGA AKABAINI NAMBA SIYO,,,HUKU WEWE UNAKUWA UEFIKIA UAMUZI WA KUVUNJA MAHUSIANO KWA TUKIO LA KIJINGA KAMA HIYO MISS CALL.
Heshimu uhuru binafsi wa mwenzio!
ReplyDelete'Privace' ???
Ungenza kutoa za kwako kwanza kabla ya kutaka za kwake!
Inaonesha wewe pamoja na kuwa na degree mbili lakini bado una akili za kitoto. Sasa passwork zake za email na facebook ulizitaka za nini? Au ili umfungie? Unadhani kumfungia ndiyo nini? Inaonesha wewe una akili za kuja kumchunga chunga mwanamke. Kwa taarifa yako mwanamke hachungwi, anajichunga mwenyewe. Au hujiamini?
ReplyDeleteBe a man!
Sijaelewa vizuri unaomba tukushauri nini hasa hapo, ila ninachoweza kukushauri ni kuwa JIAMINI na AMINI kuwa unaweza kupendwa pasina kusalitiwa. Epuka sana kuchokonoa mambo yasio ya msingi kama kufatilia/kuchunguza chunguza mambo binafsi ya mtu (email, msg, facebook n.k) ambayo yanaonesha kutokuwa na imani na mwenzio. Kitendo cha yeye kukupatia hizo passwords inatosha kukuonesha kuwa hana mambo mabaya.
ReplyDeleteNasisitiza, JIAMNI na AMINI unaweza kupendwa bila kusalitiwa!
mmh ww ni aina ya wanaume wanaoitwa "Slave husband' meaning
ReplyDeleteu treat a wife like a slave..sasa access umepewa.(Ningekuwa mm sikupi coz ni personal)but still unablock..u r so selfish..hizi ni zama za utandawazi kimawasiliano..safi sana kama amefanya hayo maamuzi sahihi..
Mimi ni mwanaume kama wewe lakini kitendo ulichokifanya sio cha kiungwana hata kidogo. Kwa nini umzuie kutumia email na facebook tena bila hata ya kumpa taarifa kwanza. Wewe unadai ni msomi je huelewi umuhimu wa email? Je yeye angefanya hivyo kwako ungekubali? Unaanza kufanya hivyo katika uhusiano wa miezi mitatu je utakapomuoa si utamfanya mtumwa wako? Inabidi ubadilike kaka.
ReplyDeleteWewe ni control freak. kwanini uchukue password zake? Huyo mwanamke anatakiwa akukimbie kadiri anavyoweza. Email, facebook ni personal! Hakutakiwa kukupa password, mapenzi ya kiafrika saa nyingine ni taabu tupu. By the way mimi ni mwanaume and I dont ask mwanamke wangu hata simu ikipigwa, nothing ana uhuru na maisha yake
ReplyDeleteYeye Msichana ndiye aliyestahili akutake wewe umpatie za kwako!
ReplyDeleteKwa Vigezo gani?
1.Umri wako ni mkubwa kuliko yeye,
hivyo unaweza kuwa umeshapitia kwingi kimahusiano kabla ya kufika kwake.
2.Idadi ya miaka yako ya masomo:
-Form 1 hadi Form 4 miaka mi 4
-Form 5 hadi Form 6 miaka mi 2
-Digriii ya kwanza miaka 3-4
-Digrii ya pili miaka mi 2
hivyo kwa miaka hiyo hapo juu 11-12 ya masomo yako wewe Mwanaume hadi Digrii ya Pili utakuwa umeshatengeneza mahusiano na wengi pamoja na kujifanya kwako Mlokole/Mujahidina kuwa hadi sasa hukumtaka mkutane kimwili !
Sasa kwa nini yeye asikutake wewe kwa mlolongo huo wa miaka 12 masomoni umpe za kwako ili akuchunguze?
Watu kama wewe ndio wanakuwa rahisi kupigiwa kwa kujifanya kwako unamfuatilia mtu kwa karibu.
ReplyDeleteNani alikwambia mwanamke anadhibitiwa kwa password ya facebook, e-mail na kontact anazopigiwa na kupiga za simu yake ya mkononi?
Kilichokufanya uombe password ya email yake na facebook ni nini? Hizo ni sawa na simu yake ya kiganjani hupaswi kuvigusa.
ReplyDeleteKuna vitu ni private hata kama ni vya mkeo au mumeo. katika ulimwegu wa sasa ukitaka uishi maisha ya amani na mkeo/mumeo au mpenzi wako usiguse simu, email au facebook password.
Wewe unamdhibiti kwenye facebook ,e-mail na simu watu wanakupigia kupitia kwenye mabanda ya Chips kuku na Maduka ya Vipodozi na mavazi!
ReplyDelete'Killing softly' wataalamu hawatumii facebook, e-mail hata simu huwa hawapigi kwa mademu!
Upo hapo?
Mimi naona ulikosea, maana kutaka password yake ya facebook, si sawa na endapo you wanted her to see that you are clean ilibidi nawewe umpe access yako, that could bring about harmony ila kama umechukua yake na shukurani yako ukamblock you must be nut.
ReplyDeletekila la heri.
sasa kama unampenda saana kabla ya kumrudishia access zake mpe password yako then uombe msamaha baada ya hapo. ni kama vile ungemwambia unataka 5000 akakupa ATM card yake ulipokuta kuna pesa nyingi kuliko unazotaka ukakomba zote................... pls consider yourself wrong na uapologise hata akikuacha uwe umeomba msamaha
Msomi na wanaume wafuatiliaji wa Mademu kama wewe huwa wanapigiwa mizigo yao na Machinga wapaka rangi za kucha na waosha miguu Mademu!
ReplyDeleteUnakuta Chinga boy anakuburuzia mzigo wako kiulaini, eti ohhh hatuingiliani kimwili ,huku unataka kumfuatlia mwenzio kwa karibu, mbona yeye hajataka umpe za kwako?
Hayo masaa 24 kazi anayoifanya ni kufuta e-mail zote mbaya na kuwa block ktk fb utakaohisi vibaya kwako!
ReplyDeleteYaani umeniharibia siku,wewe si rafiki mwema, regardless ya chochote email na facebook ni ya kukutana na marafiki zake, sasa kama unamzuia kuwasiliana na marafiki zake akiwa ndani ya nyumba si itakuwa hatari hata ingekuwa mimi nakubwaga mbali sana. Hebu fikiria angekufanyia hivyo wewe ungejisikiaje. Umeniudhi sana!!!
ReplyDeletewewe wa kupigwa kibuti tu. you are a control freak. unamtreat mwenzio kama mtumwa hata hujamuoa, ukimuoa si ndiyo utamuwekea mguu usoni kabisa!
ReplyDeleteemail na facebook ni njia za communication these days, unamzuia mtoto wa watu unataka afe na msongo wa mawazo au! umeniboa sana ungekuwa karibu sijui tu
SOUND LIKE YOU R JEALOUS, ENVY, ZUMBUKUKU, WHO WANTS TO CONTROL SOMEONE LIFES BY USING WORD "LOVE"... OR WIFE TO BE AKA FIANCEE.
ReplyDeleteWHY DID YOU ASK HER FACEBOOK/EMAIL ADDRESS WHICH HONESLTY SHE GAVE YOU WITH BOTH HANDS.
TO ME, SOUND LIKE YOU HAVE CHANGED IT (PASSWORDS) AND SHE CAN'T GET ACCESS INTO HER OWN EMAILS/FACEBOOK.
AM NOT BIG FANS OF SOCIAL NETWORKS AS IT DESTROY PEOPLE'S LIFE AND SPEND MOST OF YOUR TIME IN FRONT SCREEN.
IT ALSO USED BY PAEDOS, CHEATERS LOOKING FOR VALNURABLE WIVES/HUSBANDS IF NOT FIANCEE LIKE WUT YOU DID YOURSELF BY TAKING HER MIND OFF OTHER SUBJECT AND FEED YOURS WITH WORD..."I'M GONNA MARY YOU"!
BARE IN MIND, NOT A MAN OR WOMAN, EITHER MARRIED, IN RELATION OR LOOKING FOR ONE, CAN BE FOLLOWED THEIR BACK IN ORDER TO CATCH THEM WITH SOMEONE ELSE AKA..CHEATING.
IF YOU LOVE SOMEONE AND WANT TO HAVE RELATION, JUST DO IT AND DON'T EVER EXPECT YOU ARE ALONE!!!
THERE MUST BE SOMEONE EITHER BEFORE YOU/AFTER YOU WHO TOOK HER MIND BUT NOT 100% WILL HAVE SECURED HER LIFE OR WANT TO LIVE WITH HER!!!
THOSE PEOPLE ARE CALLED "RELATION DESTROYERS" WHO HAVE MAGNET IN THEIR HANDS TO GRAB ANYTHING EITHER METAL OR NON METAL MATERIALS.
THUS, THEY TURN TO BE MARRIED BUT, ALWAYS THERE'S SHADOW OF YOU SOMEWHERE ELSE.
IMO; IF YOU WANT TO MARRY JUST GO FOR IT BUT DON'T EXPECT YOU ARE THE ONLY ONE. GO FOR IT, START A FAMILY WHICH IS MORE IMPORTANT THAN THINKING OF BEING CHEATED!!! that's human nature and can't be changed...not at all. trust me.
IF YOU NEED MORE ADVICE, GO TO WWW.CHEATERS.COM WHERE YOU'LL FIND MORE DETAILS....OR WWW.JEALOUSLIFE.COM FOR MORE INFO.
ALAMSIKI
JAMANI JAMANI JAMANI TU MSALIE MTUMEEEEEEEEEE.
ReplyDeleteNIMEKOMAAAAA JAMANI SIRUDIIII TENA.
KWELI NIMEKOSEA HUU WOTE JAMANI NI ULIMKUKENI MWENENU MIMI NI MWANAUME BIKIRA SIJUI HATA HUKO CHINI KWA MWANAMKE KUKOJEE.
NISAMEHENI WAJAMENI ITABIDI NIOMBE BINTI MSAMAHA MANAKE KILA MTOA MAONI KAANGUSHA RUNGU LA NGUVU KWENYE KICHWA CHANGU.
NISAMEHENI JAMANI. PLEASE. NIMESOMEA MAMBO MENGINE LAKINI SI MAMBO YA MAPENZI. IIII WAJAMENI NGOJA NIKUGAMBIRE ILIVYOKUWA.
Mtu na msomi mzima hovyo! Tutake radhi na uachane na huyo dada utafute bibi kizee cha kizungu, hufai!
ReplyDeleteAaah acha kutuzingua,wewe demu miaka yote hiyo hujambandua?mlikuwa wapenzi vipi?huwezi kumwita msichana mpenzi huku hujambandua.Hatuna ushauri unatuzingua.
ReplyDeleteI swear, you must from Mara.
ReplyDeleteKuomba password hujafanya kosa, umefanya kosa ulipoibadili maana umeonyesha wewe si mwaminifu a liar and you r sick as dog.I will tell you one thing today kwamba if you need back this girl don't u ever do that shit again and my guess is that she already made up her mind and gone for good. Tokea nizaliwe sijaona bwege kama wewe, unahitaji some Relationship Counseling maana i guarantee kwamba hata awe demu gani kwa ulivyofanya lazima akupotezee and next time remember this, for relationship to work there are two rules, rule number one is No lies and rule number two is No secrets apparently you violated both of them. Umemuomba password lakini umemdanganya kwa ku trick ukazibadili na pia kwa nini usimpe na za kwako what r u hiding from dummy ass? una Bahati huyo demu simjui ningekunyang'anya mbele ya pua yako kenge wewe.Au demu ni mzuri sana kiasi kwamba hujiamini kwamba amekubali kuolewa na fala kama wewe?
ReplyDeleteU need to change your approach my friend may be in future you will find the type of woman u deserve,
Mdau washington dc the Home of us Supreme court Baby
Kama una Degree 2 kwa umri wako wa miaka 31, elewa wapo waliokuzidi kwa hiyo elimu na umri ,mfano mwenye umri wa miaka 40+ atakuwa ni Dakitari (hata kama Kisomo hana ila kwa uzoefu wa mahusiano kukuzidi wewe kulingana uamuzi uliomfanyia mwenzio na mtazamo wako huo wa Kibwege)!!!!
ReplyDeleteZaidi ya hiyo Elimu na umri huyo wa 40+ atakuwa na pesa zaidi yako!
Hizo mbinu zako za udhibiti ni za under 20- wakati wewe ni 30+ !!!
Hapo demu wako huyo wa miaka 23 'anatafunwa' na huyo man 40+ (Dakitari/Mzoefu) tena bila kupigiwa simu, kutumiwa e-mail wala FB yako hiyo!
Demu anafuatwa kona, anaingizwa katika gari tinted anakwenda 'chapwa kiufundi' vitendo bila makosa!
Sasa wewe utabaki na simu ya demu, FB, e-mail na password zako,,,Je demu wako 'hajachambuliwa kama karanga' hapo?
Mwenye Digirii 2 wewe ndio Bwege mtozeni kweli!
ReplyDeleteUnafikiri 'Masanja Mkandamizaji' atatumia Facebook, e-maiol na simu kukubabulia mzigo wako?
Bandugu, Bandugu anayekupigia demu wako hatumii hivyo vitu kabisa!
Eeeeh kaga baho!!!
Achilia mbali password za fb na e-mail!
ReplyDeleteKama vipi, Demu wako mchongee chupi za bati na kumfungia kwa kufuli za solex!
Labda ndio utaweza kumdhibiti!
Ama kweli Dikteta wa Mapenzi ni wewe!
ReplyDeleteYaani mahusiano ya ndani ya miezi mitatu (3) tayari umemshuku mwenzio vibaya, unamwingilia masuala yake binafsi!
Sasa ukimuoa sio ndio utamfunga kamba au mnyororo wa kiuno kama Mtumwa?
wewe mjinga sana kwahiyo hujamuoa na unataka asiwe na mawasiliano na watu achana na watu yaani hata ndugu zake.
ReplyDeletekalale mbele, mnyama wewe nyie ndo mnaopika wake zenu na kuua.
duh kweli shule sio akili na u gentemani
umeniuzi sana.
Ndani ya miezi mitatu (3) tu ya mahusiano!
ReplyDeleteUkiona mijitu ya hivi inakuwa yenyewe ndio michafu kama nini.
Bwege wewe mwenyewe una usafi gani wa kuanza kumtuhumu mwenzio na kumwingilia ktk masuala yake binafsi?
mi naona jamaa yupo sahihi tu, ameomba msaada wa mawazo, kwani si wote tupo sawa, sasa mkianza kumwita zumbukuku, mjinga, hajaelimika na mengine kibao. Naona hamtakuwa mmemsaidia.
ReplyDelete1. Wapo wanaofanya hivi wengi na hawasemi, mwishowe wanaleta madhara makubwa hadi kuuwa.
2. Anatakamaoni yenu ili ajue nini afanye kwani hakuna binadamu kamili.
3.NAASHANGAA SANA KWA HUYO MSICHANA, KUVUNZA UHUSIANO KIRAHISI NAMNA HIYO.
'''Wapenzi wapendano kwa dhati'' kwa kuvunza ndoa mwanamke kwasababu umemnyima pasword tu kaka, haki ya mungu, hata kama ukimpa ata kublackmail kwa kila utakacho mnyima.
Kaeni chini, fikiri mara ya pili, mtambue kama mnapendana kwa dhati kama unavyosema.
Ila nachokusifu umeweza kuwa mwazi, wapo kibao wanashindwa kuwa kama wewe, naamini hutashindwa kusonga mbele kwa sababu ya mapenzi,
Wengine wanatumia maneno ya dharau hapa, ila kwao yapo kibao..hata kama si kwa style hii ni style nyingine.
MWOMBE MUNGU SANA KUHUSU NDOA YAKO, KAMA UTAFUNGA PINGU ZA KUFUNGUA SIKU YA KIFO, BASI HUYO MSICHANA UKIMLAZA NJAA SIKU,AU UKIONYESHA UDHAIFU WOWOTE ATAZIFUMGUA KIRAHISI TU KAMA HIVI ANAVYOTAKA KUFANYA.
BADO SIAMINI KAMA HUKUMU YA WEWE KUTOKUTOA PASSWORD NI KUACHANA.
WAPO WANAFUMANIANA, BABA HAJARUDI NYUMBANI,WANAPIGANA LAKINI WANASAMEEANA NA KUISHI KWA FURAHA.
KAKA, MPE PASSWORD ZAKE NI HAKI YAKE, NA SI VIZURI KUZICHUKUA.
LAKINI JIULIZE MARA MBILI, ''HUKUMU ALIYOTOA INAENDANA NA KOSA ULILOFANYA''
JIULIZE JE? INGEKUWA NI SCAMMER WAMECHUKUA PASSWORD ZAKE,NA WAKABADILISHA INFORMATION ZOTE NA AKASHINDWA KUTUMIA FB AC YAKE ANGEJIUA?
TUMIA AKILI SASA USITUMIE MAPENZI HUTAPATA JIBU.
Una tatizo kama langu aisee ila we umenizidi kidogo maana hapo ni sawa na kumchungulia bafuni au chooni haina tofauti. Pia umeamua kujiumiza roho bila sababu ya msingi kwa kuangalia jinsi vidume wengine walivyokua wakijaribu bahati zao. Kikubwa ni kua muwazi kwani kwa umri wako ushakutana nazo nyingi sana na ushatendwa sana ndio maana hadi leo upo single kama mimi sio kosa letu wakati mwingine pia ni kosa letu mimi na wewe pia . Kwani mahusiano yanaharibika kirahisi sana kama hivi inavyokutokea wewe sasa hivi.
ReplyDeleteMi nakushauri kwa sasa muombe tu msamaha mrudishie password yake ila muache aamue kama anataka kua na wewe au la sababu kwa sasa ni wewe unayemhitaji zaidi kuliko anavyokuhitaji wewe(kwa upande wetu) na pia kwa umri wake ni wazi binti anaona bado ana nafasi ya kupendwa tena umri bado unamruhusu hivyo mpe yeye uhuru wa kuamua kama kweli bado anaupendo na wewe tena.Ila akikataa muache kwa roho safi kabisa wala usilazimishe
tena ingekuwa mimi hata password nisingekupa kwanza inaonekana huyo binti anakupenda na kukuheshimu ila wewe ndio unaonekana dikteta hahaha kaka mapenzi hayaendi hivyoooo mpe email zk acha ushamba sisi wanawake tunaona fahari kuolewa na watu wazima kumbe na nyie ndio mnatudikteti hutopata mwanamke kwa stahili hiyo na hutokaa na mwanamke
ReplyDeletePamoja na elimu yako kaka, wewe una jina moja tu: 'mjinga'. Kama huyu dada ana soma hizi feedback, naomba tu aachane na wewe. Bado ni kijana ataolewa tu.
ReplyDeleteDaaaaa!! kwanza niwashukru wadau wote kwa kuonesha kuguswa na hili la kwangu na mpenzi wangu!!i see nimeyasoma maoni yenu yote na nimeupokea ushauri wote uliotolewa bila kujali ulikuwa hasi ama chanya,nitafanyia kazi yaliyosemwa na yaliyondani ya uhalisia wa akili yangu,moyo wangu na mawazo yangu.Ila kwa jinsi binafsi nilivyo na ninavyojifahamu na jinsi jamii inayonizunguka inavyonifahamu,nilishindwa kufanya maamuzi yasiyosahihi ya kuendelea kumnyima access za socialnetworks accounts za huyu mpenzi wangu.Nimeamua kumpatia na kuanza kufikria mambo mengine japokuwa ameonesha msimamo wa kuvunja urafiki na mapenzi yetu.Hata hivyo mke mwema utoka kwa mungu.asanteni sana kwa michango yenu wadau.
ReplyDeletemdau muomba msaada-Madrid-Spain.
Ama kweli kusoma si kuelimika!
ReplyDeleteBWANA MDOGO
ReplyDeleteSASA UMEINGIA KATIKA ELIMU NYINGINE KABISA YA MAPENZI KWA HIYO MTIHANI WA KWANZA UMESHA FELI JIPANGE UPYA KAMA UNAMTAKA HUYO BINTI.
tunasoma ili elimu itukomboe but nadhani wewe pamoja na kuwa na degree 2 bado hujakomboka.... mtu mzima hawi controlled hivyo km mtoto mdogo, acha ushamba. Mapenzi ya hivyo walifanya babu zetu, sikujua kama bado kuna watu wanayapractice, tena wasomi Loooh!! Aibu kwako!! Bora upigwe kibuti tu
ReplyDeleteYeye amekuwa muwazi kwako, na wewe je? Kwanza kabisa na wewe mpe password zako aweze kuona uliyokuwa nayo. Kisha kama mimi ndio ningekuwa huyo mdada, ningekumwaga tu. Mwanaume gani una wivu kiasi hicho? kila mtu ana historia yake huko nyuma, mmekutana mkiwa watu wazima tayari. Au wote nko virgin? Dont not pretend, maisha ya ndoa USHAFELI KAKA!!!!!!!!!
ReplyDeleteAskari Magereza?
ReplyDeleteKama huna sifa hiyo hapo juu labda utakuwa Jambazi wa Mapenzi au Gaidi wa Mapenzi!
Maana mbinu zako za kumdhibiti mwenzio ni za kama Askari Magereza wa Wafungwa wakorofi.
Ahhh wewe ni Jasiri na una hatari sana kwa kuthubutu fikra hizo.
Na kama ni mashitaka unafaa kupelekwa ICC kwa kukiuka Uhuru binafsi wa Mtu !
Utaona ukisha 'pigiwa mshipa' demu wako watu kama wewe huwa ni wepesi kuangua kilio!
ReplyDeleteMaana pamoja na udhibiti wako unakuta umezidiwa mabao na Wajanja!
Kama Mdau mmoja anavyosema hapo juu,
ReplyDeleteAina hii ya Wanaume wanatokea Mara na Kagera!
wewe ni pumbafu, kwa hizo tabia zako hata mwananke wa kijiji hatakuvumilia
ReplyDeleteJIANDAE KUISHA BILA MKE
Wewe Bwege ama kweli Kusoma sio kuvuka vidato!
ReplyDeleteYaani hata 'kumkata' bado unaleta mashariti yako ya kifala hayo?
Shauri zako, demu akijipindua akiangukia kwetu Wadau tutakusaidia 'kuvunja bucha' kwa niaba yako halafu wewe kwa ufala wako utabaki unazoa manyama !!!
Ohooo?
Zaidi ya 95% ya Maoni ya Wadau humu ndani Jamvini umewa boa sana watu wewe Jamaa kwa ufala wako huo.
ReplyDeleteSasa adhabu yako tutachunguza huyo Demu wako ni nani utasaidiwa kazi, wewe si unajifanya ehhh sijaomba mzigo elewa ya kuwa watu humu wanajua kubembeleza sio mchezo watakupigia 'mnemba' (wata kubandulia) kwa huyo demu ndio utakoma kulinga na utajifunza kuheshimu wenza ktk mahusiano!
Imewakera wengi humu jinsi unavyomfanyia demu wako,,,inahitaji usaidiwe kwa kuwa inaonyesha ni wazi kuwa huna uwezo,kipaji wala ujuzi wa kumbembeleza mwanamke wewe!
ReplyDeleteMwanamke wewe anapewa nyama ya ulimi!
Mwanamke analishwa mishikaki ya mbuzi wewe,,,ebo?
Mwanamke hapewi 'supu ya mawe' kama hizo kero hivyo unavyomfanyia!
Wewe una elimu zako tu za madigirii hayo mawili lakini huna elimu wala kipaji vya kumuenzi mwanamke!
Au ulisomea Boarding Secondary Schools za Mikoani O-Level na A-Level?
Wewe hujui kuwa mwanamke ni wa kubembelezwa daima?
Ulisikia wapi mwanamke anakerwa ?
Hivi utakapochukua hizo password halafu ukakuta demu wako aliandikiana e-mails na dada yako wewe wakipeana taarifa na dada yako akimwelezea matatizo yake ktk njia yake ya kikeni itakusaidia nini
ReplyDeleteHuoni hapo utakuwa umeaibika wewe?