Leo jijini Arusha katika pitapita zake Globu ya Jamii imeshuhudia kwa mara ingine tena mtindio wa kuheshimu alama za pundamilia barabarani maeneo ya Sanawari ambapo kinadada hao pichani ilibidi wasimame takriban dakika tano nzima kusubiri magari yasimame ili wavuke.
Katika magari kama kumi hivi yaliyopita kutokea huko kulia, ni hilo semi-trela peke yake lililofuata sheria hiyo na kuwaruhusu wapite. Ila upande wa pili nusura wagongwe na gari dogo alilokuwa akiendesha mwanamama ambaye alisimama miguuni kabisa ya wavukaji. Katika uliza uliza inasemekana ajali hutokea mara kwa mara sehemu hii kwa madereva kutofuata sheria.



Sheria ya hizi Zebra inasemaje hasa.Dereva unatakiwa usimame au uchukue tahadhari.Ebu tuelimishane hapa hapa kwenye blog ya jamii.Nikiwa kwenye highway wakati ni mwingine huwa naona Zebra crossing kwenye sehemu zenye shule,huwa naangalia saa haraka haraka saa nikiona muda wa shule umeshaisha"nanyooka",kama ni jumapili huwa nachukulia watoto hawapo shule kwa hiyo huwa sijali sana.Lakini nahisi huwa ninafanya makosa makosa.Au kuna Zebra za mjini na maporini huko Kintinku?
ReplyDeleteDavid V
Zebra inaashiria kuwa ni eneo la kuvuka waenda kwa miguu. Kwa maana hiyo kama dereva anazijua vizuri sheria za barabarani inatakiwa anapoona alama ya zebra lazima upunguze mwendo kama. Na ikitokea kuna watu wamesimama wanataka kuvuka ni lazima yeye asimame ili wavuke. Dereva akimugonga mwenda kwa miguu sehemu yenye alama za zebra, moja kwa moja hilo ni kosa lake na ni uzembe wa kupindukia. katika nchi za wenzetu, unanyang'anywa lesseni na hutaruhusiwa kuendesha gari.
ReplyDeleteLakini Bongo ndio hivyo, madereva hawajui sheria, kama wanajua macho hayaoni, kama yanaona yanapuuza na hawajali watumiaji wengine wa barabara
Zebra ni alama ya tahadhari kuwa kuna uwezekano wa wapita njia kuwa wanavuka.
ReplyDeleteZEBRA isiyokuwa na mataa ya kuruhusu magari na watembea kwa miguu, ni LAZIMA dereva kusimama pale anapomkuta mtembea kwa miguu awe ameanza kuvuka au hajaanza kuvuka. Na hapa mtembea kwa miguu anaweza kuvuka tu hata bila kuchukua tahadhari. Maana yeye ndo mwenye haki.
Lakini ZEBRA yenye mataa ya kuongoza magari na wapita njia, hapa inatakiwa yafuatwe mataa.
Mdau-Sweden