NA ABDULAZIZ VIDEO-LINDI 

Mtoto Sofia Hamis mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la pili katika shule ya Msingi Litehu wilayani Tandahimba,Mkoani Mtwara ambaye alitoweka mwanzoni mwa MWEZI huu,amepatika akiwa katika shimo lililo katika msitu wa kijiji cha Mmeda wilayani humo huku akiwa hai baada ya jitihada zilizofanywa na Mganga wa kienyeji kutoka kijiji cha Mtama Lindi Vijijini.

Mtoto huyo alitoweka nyumbani kwa Mama yakeMzazi tarehe 08/05/2012 akitokea shuleni na toka siku hiyo hakukuwa na taarifa za kuonekana kwake na jitihada mbalimbali za kumpata mtoto huyo kutozaa matunda
huku siku zikisonga mbele.

Kufuatia kupotea kwa mtoto huyo kulizaa taharuki mbalimbali kijijini hapo hali iliyomfanya mama mzazi kuhangaika kutafuta kwa njia ya imani za jadi na kufanikiwa kujuzwa na mganga alietambulika kwa jina la Rukia Akili Salum mkazi wa Mihogoni-Mtama Lindi Vijijii kuwa mtoto yupo hai na anao uwezo wa kumtoa katika mazingira aliyokuwepo.

Mama wa Mtoto huyo alifanikiwa kusafirisha mganga huyo hadi kijiji cha MMEDA -kilichopo kata ya LITEHU Tandahimba ambapo baada ya kufanya shughuli zake alifanikiwa kwa pamoja kumkuta mtoto huyo akiwa shimoni akiwa hawezi kuongea vizuri huku mwili ukitawaliwa na upele.

Baada ya kufanikiwa kumpata mganga huyo alisafiri nae kwenda Mtama kwenye makazi yake ili ampatie tiba ambazo hadi Mimi namfikia mtoto huyo alikuwa tayari amerudi katika hali yake ya kawaida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Mtoto huyo katika kuzagaa zagaa porini alitumbukia kwenye shimo hilo akashindwa kutoka hadi wanakijiji walipoanzisha msako na kumkuta huko shimoni walikomuokoa. Wakati wanakijiji wanaendelea na msako, mama mzazi alikwenda kwa mganga huyo kupiga ramri, baada ya mtoto kupatikana mganga anadai ni yeye. alexbura,

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Inawezekana mtoto alitoroka nyumbani, hii habari ya msukule ni ngumu kueleweka

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Duuu! Hizi ndizo mila/imani zetu mnazotaka tuzirudie, tuachane na zile zilizoletwa na Wazungu pamoja na waarabu? Itakuwa ngumu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    Tanzania kila kitu kinawezekana. Sasa mnashangaa hii, je ile ya Babu Ambi a.k.a Mzee wa Samunge. Waulize Ma-Minister.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2012

    http://boston.barstoolsports.com/random-thoughts/dead-kid-wakes-up-asks-for-a-glass-of-water-then-goes-back-to-dead/

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2012

    Huyo mgamga lazima awekwe kitimoto huenda ilikuwa misheni yake kumtorosha huyo mtoto halafu baadae adai anajua yuko wapi ili apate kitu kidogo na umaarufu.Ushirikina ni mbaya sana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2012

    wajinga ndio wadanganywaooo

    ReplyDelete
  8. Anon. wa mwanzo kabisa hapo juu, nakubaliana na maelezo yako. Tujaribu kuwa more MATERIALIST kwa kukibaini chanzo cha tatizo, rather than being IDEALIST na kuendelea kujiendekeza kuamini na kushikilia hizi dhana za imani potofu za kishirikina,wakati chanzo cha tatizo kipo wazi kabisa, hiyo ya Msukule ni ngumu kuingia akilini. Mganga nae kadandia humo humo, hakuna lolote!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2012

    Mama yake anamtishiaga sana mtoto huyu hadi akaamua kutoroka na kwa bahati mbaya akadumbukia kwenye shimo kama hamuamini mnaojua mtoto alikuwa abused either kwa kupigwa, kufanyishwa kazi ngumu au kutopewa haki ya mtoto mtajua ninachomaanisha kwa kumtizama tu ktk picha. Alipodumbukia kwenye shimo akashindwa kutoka na kwa vile alikuwa hali walipompata alikuwa hawezi kuongea, mwanamke yeyote i mean female ana uwezo wa kuishi siku nyingi bila kula angekuwa dume angekutwa maiti.Pia iweni na macho mtoto wa miaka 12 yuko class 2 while angepaswa kuwa class 5, It means there is problems in her family. Beware my Tz msikubali kupotoshwa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2012

    ... hacha imani potovu za ushirikina!...mtoto alidumbukia shimoni, akashindwa kutoka, ngozi yake ktk self defence ikaota vipele, hawezi kuongea kwasababu alikuwa na ukosefu wa maji na chakula mwilini!!! Fungukeni macho, hacha kupotoka/kuptoshwa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...