Rais Jakaya Kikwete akiwa na Marie Frances ambaye ndie mwanzilishi wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon wakipokutana jijini Washington DC,Marekani.

Mwanzilishi wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Marie Frances alie mji wa Bethesda nchini Marekani amemsifu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama kiongozi anayependa nchi yake na anayeona mbali. Marie Frances ametoa sifa hizo hapa mjini Moshi wakati Rais Kikwete akikutana na viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania (AT) kupanga mikakati ya kufufua riadha nchini hivi karibuni.

Frances ambaye aliwahi kukutana na Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa jengo la Tanzania House katika jiji la Washington DC amesema kuwa ni nadra sana kuona kiongozi wa nchi akikutana na viongozi wa chama cha mchezo wowote kuzungumzia maendeleo yake. Hii ni miujiza hata katika nchi kama Marekani.

Marie Frances amemuelezea Rais Kikwete kama mtu wa haiba ya kipekee mwenye akili na maono ya kuiendeleza Tanzania kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya Millenia. “Nilimpenda sana nilipokutana naye jijini Washington. Ni kiongozi mwenye haiba ya kipekee” alisema Frances ambaye aliombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za marathon nchini Tanzania mwaka 1990.

Marie Frances ambaye alikuwa mkuzaji (producer) wa Miss Universe pamoja na vipindi vya television huko Hollywwod nchini Marekani alihamia nchini Misri mwaka 1984 kuafanya kazi ya ABC kama mwandishi wa bahari. 

Akiwa nchini Mirsi, Marie Frances alianzisha mbio za Pyramid Marathon pamoja na Miss Universe ambazo ziitangaza sana nchi ya Misri. Ni wakati wa matamasha haya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo alipomwomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon ili kuitangaza Tanzania.

Frances alikuja Tanzania mwaka 1990 na kutaka kuanzisha mbio za Mt. Meru Marathon lakini alipofika tu mjini Moshi alivutiwa sana na mlima Kilimanjaro na hivyo kuiamua kuanzisha mbio za “Mt. Kilimanjaro Marathon” mwaka 1991. Mbio hizi hukimbiwa kila jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita na zitatimiza miaka 22 tarehe 24 Juni mwaka huu.

Mt. Kilimanjaro Marathon zimeshapewa tuzo mbalimbali kama mbio za kimataifa. Gazeti la Wonders of the World lenye wasomaji zadi ya million 5 limezipa nafasi ya 2 kama mbio nzuri za kushiriki. Wakati jarida la kimataifa la Forbes limezipa nafasi ya kwanza kama mbio nzuri za kukimbia! 

Marie Frances pia ameanza kuwapeleka wanariadha wa Tanzania kukimbia nchini Marekani kwa kuwasaidia fedha za Visa za Marekani pamoja na tiketi za ndege kama inavyoonyesha picha ambapo mkimbiaji Nelson Brighton anapewa pesa na Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Benadetta Kinabo kwenda nchi Marekani mwezi ujao kwa ufadhili wake.Kwa sasa mbio hizi hufadhiliwa na shirika la ndege la Ethiopia.

Ni katika juhudi zake za kuutangaza mlima Kilimanjatro ndipo Manispoaa ya Moshi ikaipa jina la Marie Frances Boulevard barabara ya zamani ya Bustani Ale.

Mt. Kilimajaro Marathon itaanzia Moshi Klabu tarehe 24 Juni saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42, 21, 10 na 5 zitashindaniwa na watalii toka Marekani pamoja na wakimnbiaji toka Moshi na Arusha.

Wakimbiaji wanajiandikisha kwa wingi Bristol Cottages hotel iliyopo mkabala na benki ya Standard Chattered karibu na Kilimanjaro Hospital katika Manispaa ya Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2012

    Sasa inabidi tuboreshe ili
    tuweze kuwa na marathoni pamoja na michezo mingine

    Mji wa Moshi unatakiwa kuwa na kiwanja chenye hadhi ya ubora wa kimataifaili watalii pamoja na wenyeji waweze kutumia mda fulani kwenye kujiburudisha na michezo.
    Utalii wa michezo unaweza kuingiza Taifa kipato kikubwa ukilinganisha na utalii wa kupanda mlima tu.

    Tunaweza kuwa wenyeji wa michezo mikubwa Afrika ikiwemo riadha Kama tutakuwa na viwanja vya kisasa (sport center) kwenye miji yenye mvuto.
    Utalii si kupanda Mlima tu hata kuangalia na kuwepo kwenye mazingira yake yenye mvuto ni utalii inategemea na mazingira yenyewe si hatarishi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...