KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wanachama wa CCM, tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya, katika mahafali ya kuwaaga, leo Juni 25, 2012, katika hoteli ya Paradise mjini Mbeya.
  Akikagua gwaride la Chipukizi
 Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimpa kadi ya CCM Aranora Msigwa wa mwaka wa  tatu, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) alipopokea wanachama wapya wa CCM, wakati wa mahafali ya wana-CCM tawi la Chuo hicho mjini Mbeya, leo June 25. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa  wa CCM Mbeya, Maganga Sengerema.

 Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza muziki wa mtindo wa 'Kwaito' wakati wa sherehe za mahafali ya wana-CCM  tawi ala Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) katika hoteli ya Paradise mjini Mbeya leo June 25.

  Wana_CCM tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya wakimpa zawadi ya picha yake, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye wakati wa mahafali ya wana-CCM tawi la chuo hicho.
 Nape akiifurahia picha yake baada ya kuzawadiwa na wanachuo hao.
 Wana-CCM tawi la TEKU wakifurahi wakati wa kwenye mahafali yao 

 Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema akimkaribisha nape kuzungumza kwenye mahafali hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tawi la CCM Chuo Kikuu cha TEKU  Boniface Paulo.
Nape akilakiwa na viongozi wa CCM alipowasili mjini Mbeya kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2012

    Bravo Nape. Well done. Keep it up.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2012

    Si nilisikia kwamba wanasiasa mwiko tena kukanyaga vyuoni siku Lema alipoenda UDOM sasa imefutwa ile warning? au ilimaanisha vyuo vikuu tu? aaah I LOVE YOU TANZANIA KWA MOYO WOTEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2012

    wakishakosa ajira na kuanza kula vumbi wote watajiunga na Chadema. Nape konsentret kwenye wakulima, sapoti ya wasomi haina garantii wakati ajira hakuna nchini.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2012

    Mh.inaonekana kwa kiasi gani huendi na wakati!!!Itawezekana kweli kuleta mabadiliko kwa staili hii????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...