Wananchi wakishuhudia moto ukiteketeza maduka eneo la Uhindindi kata ya Miyomboni usiku huu
Mali zilizookolewa eneo la tukio ambalo pia ni makazi ya watu
Mali mbali mbali zikiwa zimeteketea kwa moto
Simu zikiwa zimeokolewa katika moja kati ya maduka ya simu Uhindini ambayo yameteketea kwa moto
Wananchi wa Iringa mjini wakishuhudia moto mkubwa ukiteketeza maduka eneo la Uhindini usiku huu
Askari polisi wakiweka ulinzi eneo la tukio.

Na Francis Godwin, Iringa
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza zaidi ya maduka 10 eneo la Miyomboni katika Manispaa ya Iringa usiku huu.

Moto huo ambao chanzo chake bado kufahamika umezuka majira ya saa 2 usiku huu katika eneo hilo la Uhindini kata ya Miyomboni mjini Iringa.

Baadhi ya wafanyabiashara waliokumbwa na tukio hilo la moto na kuteketeza maduka yao wamesema kuwa moto huo umeanza katika chumba kimoja wapo cha duka na kuwa wanahisi ni hitilafu ya umeme.

Hata hivyo wamesema kuwa baada ya moto huo kuanza kuwaka walipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa kikosi cha zima moto Manispaa ya Iringa ambao walifika ila waliishiwa maji kabla ya kuuzima moto huo.

Pia walisema wakati gari la zima moto limekwenda kuchota maji mengine mto Ruaha, vibaka walitumia nafasi hiyo kupora mali mbali mbali na kujikuta wakiishia katika mikono ya polisi ambao walitanda eneo hilo.

Diwani wa kata ya Miyombini kitanzini Jesca Msambatavangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na kukipongeza kikosi cha Zimamoto mjini Iringa kwa kufika kwa wakati eneo la tukio huku akiwataka wananchi kuacha kulaumu kikosi hicho kwa kazi kubwa waliyoifanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...