Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa kwa niaba ya serikali amepokea sh 7.9 bilioni kutoka benki ya NMB ikiwa ni gawio la serikali kwa mwaka 2011 kama ilivoidhinishwa katika mkutano wake mkuu uliofanyika Juni 2, 2012.Gawio hilo lilitokana na serikali kumiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki ya NMB.




Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo jijini Dar es Salaam Dk. Mgimwa alisema, amefurahishwa na benki ya NMB kwa utendaji wake kwa kuwa mwaka 2010 iliweza kutoa sh bilioni 5.7 “Benki ya NMB inaonyesha dalili nzuri ya utendaji wake kwa kuwa ongezeko hili la mwaka 2011 la sh bilioni 7.9 kwa serikali ni ongezeko zuri na fedha hii iliyotolewa na NMB Imeweza kuichangia Serikali baada ya kupata faida kwa kuwa ni nyingi sana na itasaidia kuwalipa wafanyakazi wengi ” alisema Dk.Mgimwa”

Aidha, aliipongez NMB katika juhudi zake za kuisaidia serikali kupitia shughuli mbalimbali za kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya wananchi wenye mahitaji. Alisema anathamini mchango wa NMB katika ukusanyaji wa kodi unaofanywa kupitia matawi yake yaliyosambaa Tanzania nzimai.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema NMB itaendelea kuleta huduma nafuu za kifedha kwa jamii ya kitanzania katika maeneo yote ya vijijini na mijini “NMB imeweza kufikia wateja wake nchi nzima,pia imeweza kulipa kodi kwa serikali,ndio maana NMB ni benki bora kwa Tanzania

Tukio hilo muhimu lilishuhudiwa na manaibu wawili wa wizara ya Fedha na Uchumi, Katibu mkuu wa wizara ya fedha na manaibu wake watatu, mweka hazina mkuu, wakuu wa wizara zingine pamoja na wafanyakazi wa NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2012

    Je, Serikali imelipa kodi ya zuio (withholding tax)? kutokana na gawio hilo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2012

    Hizo zitaliwa na wajanja tu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...