Pambano la masumbwi kati ya bondia Francis Miyeyusho na Mmalawi John Massamba lililokuwa lifanyike ijumaa juni 22,limeahirishwa mpaka hapo tarehe itakapotajwa tena kuwa Miyayusho atacheza na nani, lini na wapi. 

Haya yamekuja kutokana na bondia John Masamba toka Malawi akiwa hana hadhi ya kucheza na Miyeyusho na wasiwasi wa afya yake,bondia huyo toka Malawi mwenye rekodi ya mapambano ya kupigwa mawili na kushinda mawili,inaonekana ni mbovu na rekodi yake ya utata ukilinganisha na miyeyusho mwenye mapambano 42 ya kueleweka.

Kutokana na utata huo wa bondia wa Malawi na kutokamilisha malipo na vibali vyote toka Utamaduni na michezo, Hivyo mpambano umesitishwa mpaka taratibu zitakapokamilika za upande wa vibali na kumleta bondia mzuri wa kucheza na Francis Miyeyusho.

Mapambano mengine yatakuwepo kama kawaida katika ukumbi wa dar live kati ya Francis Cheka na Jafet Kaseba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2012

    Matumla amekimbiwa na Mrusi !

    Miyeyusho anakimbiwa na Mmalawi !

    Je ndio kusema sisi Tz ngumi jiwe?

    Je ndio kusema mtaji Tz tunao?

    Je au ndio mipango mipango tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...