Kaimu Mwenyekiti bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Jaji Thomas Mihayo (Katikati) akizindua utaratibu wa kutangaza zabuni kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya PPRA jana. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Push Media Mobile, Fredd Manento na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk Ramadhani Mlinga.
Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Jaji Thomas Mihayo (kulia) akielekezwa jinsi ya kujiunga katika utaratibu mpya wa zabuni kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Push Media Mobile, Fredd Manento.
Na Mwandishi wetu
KATIKA vita ya kuondoa rushwa nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imezindua huduma ya njia ya simu ya mkononi kwa waombaji wa zabuni mbali mbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.
Uzinduzi huo ulifanyika jana kwenye makao makuu ya PPRA chini ya Jaji Thomas Mihayo ambaye aliwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba zabuni hizo na siyo kulalamika zabuni hizo zinatolewa kwa upendeleo na zaidi makampuni ya nje ya nchi.
Jaji Mihayo ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa bodi ya PPRA alitolea mfano zabuni za kufua umeme hapa nchini na ile ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambazo zilileta usumbufu mkubwa na kuwa gumzo katika vyomo vya habari na jamii kwa ujumla.
“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau wetu na vile vile kutokana na watanzania wengi kushindwa kushiriki kutokana na kukosa taarifa kwa wakati muafaka, tumeingia makubaliano na kampuni ya Push Media Mobile na sasa kila Mtanzania anayetaka kupata taarifa za zabuni zetu anatakiwa kujiunga kwa kutuma neno PPRA kwenda namba 15332 na kuanza kupokea taarifa za zabuni popote Tanzania na njie ya nchi,” alisema Jaji Mihayo.
Jaji Mihayo alisema kuwa ili kuondoa tatizo hilo na kupanua wigo wa kutangaza zabuni hizo, wameamua kuweka utaratibu wa kutangaza zabuni hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi
Alisema kuwa kwa kutumia utaalam huo, kila mtu anaweza kupata taarifa kuhusiana na zabuni zetu na kuomba ili kushinda. Alisema kuwa hata kwa hata matokeo ya tenda hizo zitatangazwa kwa njia ya uumbe huo huo.
“Kila kitu hapa kitafanyika kwa njia ya mtandao bila ya upendeeleo wowote, tunaishukuru kampuni ya Push Media Mobile kwa kutuwezesha taalam huu ambao utaondoa mianya ya rushwa katika kupoke zabauni na kuchagua washindi,” alisema.
“Hii ni fursa pekee kwa watanzania kuomba zabuni zetu, lengo ni kumfikia kila Mtanzania hata aliyekuwa vijijini kwa wakati muafaka,” alisema.
Walichokosea ni kwamba utapata sms moja yenye tenda zote zilizotangazwa siku hiyo kwa ujumla, mfano stationary, kujenga barabara, insurance, ulinzi, consultancy nk. Itakuwa kero maana tenda ni nyingi sana kila siku na hakuna kampuni inayofanya shughuli zote hizo mbalimbali. Mfano Kampuni ya ugavi wa stationary haiitaji taarifa za tenda ya ujenzi wa barabara. Ingekuwa vyema kama taarifa hizi zingegawanywa, mfano kuwe na sms ya tenda ya Ugavi wa vifaa ofisini; pia sms tofauti ya tenda za Consultancy; na pia sms tofauti za tenda za Works. alexbura dar
ReplyDeleteBig up PPRA kwa kuanza kutekeleza e-goverment kwa vitendo
ReplyDeleteWell Done! Lakini nimejaribu kutuma text kama ilivyoelekezwa (kutoka nje ya nchi) lakini haikubali? Taf tujulishe ni nchi zipi na zipi utazoweza kuwa na ikawezekana.
ReplyDeleteKazi nzuri hiyo uncle Tom.
ReplyDeleteMdau California
Sio kweli kuwa utaletewa zabuni zone ndio sababu yako mafungu matano. Kama wewe ni contractor italics uletewe zabuni za ujenzi kwa kutuma PPRA works kwenda 15332
ReplyDelete